Friday, May 24, 2013

Timu mbili zote za ujerumani Kupokelewa Kesho katika Uwanja wa Wembley tayari kabisa kwa Faina ya Ligi ya mabingwa Ulaya

Shirikisho la soka nchini Uingereza Kesho itakuwa ikiwapokea wageni wa ujerumani, wakati wakijakupiga faina ya mabingwa Ulaya The Champions league uwanjani Wembley hapo siku ya jumamosi.

Jumamosi  ndio itakuwa siku ya mwisho wa kumwonyesha mbabe wa ulaya na ujerumani.hayo yanajiri pale timu mbili za Ujerumani kuingia fainali ya mabingwa ulaya.mechi itakayo chezwa katika uwanja wa wembley.Hiyo ni fainali ya kwanza kabisa kuwahi kuzileta pamoja timu mbili za Bundesliga katika historia ya Champions League.Ni miaka miwili tu iliyopita tangu Barcelona walipothibitisha hadhi yao katika soka la Ulaya kwa kuwabwaga Manchester United katika uwanja huo huo waliposhinda dimba hilo mwaka wa 2011,lakini mwaka huu ilikuwa ni tofauti na miaka yote baada ya timu zote hispania kubanduliwa na timu hizi za bundasliga kwa mabao mengi.

Katika nusu fainali iliyochezwa nyumbani na ugenini iliwakutanisha Real Madrid vs Bor..Dotmund ambapo timu hizi ziliweza kufangana jumla ya mabao nne kwa moja..Pia katika nusu fainali iliyokutanisha Barcelona vs Buryern Munchin ilkuwa hali mbaya kabisa kwa Barcelona kwa kupigwa magoli saba kwa sifuri katika mechi zilizochezwa nyumbani na ugenini..

Bila kujali matokeo ya mechi ya leo, bila shaka utakuwa usiku wa kihistoria kwa soka la Ujerumani, lakini timu hizombili zinashuka dimbani zikiwa na motisha tofauti. Bayern, hiyo ni fursa ya kujikomboa kutokana na machungu waliyopata katika vichapo vya fainali za mwaka wa 2010 na hasa mwaka wa 2012 wakati walishindwa na Chelsea katika mikwaju ya penalti.fainali hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Alianz Arena uliwaacha watu wengi vinywa wazi kwani watu wengi waliamini Buyern ndio washindi wa mwaka huo wa 2012.Nathani ni wakati mzuri kwa Buyern kupunguza machungu hayo kwa kuwaadabisha vijana hao kutoka Dortmund.

Dotmund nao si rahisi kwani walishawahi kufika faina ya kombe hili mwaka 1977,wanalenga kuwasababishia Bayern mashaka zaidi,hawa Dotmund ndio wamekuwa mahasim u wa Buyern kwa mda sasa kwa kuwachukulia nyota wao wazuri na kusajili wachezaji wanaotisha na wenye kuleta mabadiliko katika soka la Ujerumani.

Tumaini kubwa la dotmund katika mechi ya jumapili ni mshambuliaji wao hatari mpoland Robert Lewandowski ambae kwa sasa amebaki kuwa gumzo katika maisha ya soka baada ya kuwafunga timu kubwa kama Real madrid magoli manne peke yake katika mechi ya nusu fainali ya kwanza iliyochezwa katika uwanja wa nyumbani.

Melfu wa mashabiki wanatarajiwa kufika katika uwanja huo wa England kushuhudia fainali hiyo,pia kuna watu maarufu kama zilivyo dai vyombo vya habari za kimataifa kuwa kutakua na ujio wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.Kwa hiyo siku hiyo mashabiki watafurika katika uwanja huo mkubwa nchini Uingereza.

Pia onyo kali limetolewa na rais wa shirikisho la soka Uefa Michel Platini, kuwa kuwataka mashabiki kuwa na nithamu katika fainali hizo zitakazofuta hisia za watu wengi duniani,.Akizungumza katika kongamano la UEFA jijini London jana, Platini amesema tatizo kubwa ni kupanga mechi na kuwekeana dau kwa sababu linawahusisha makundi makubwa yenye fedha.Pia Katibu Mkuu wa UEFA Gianni Infantino amesema vilabu vitakavyopatikana pia na hatia hiyo vitafungiwa viwanja vyao kwa sehemu Fulani kwa tukio la kwanza la ubaguzi wa rangi utakaofanywa na mashabiki wake.

Pia katika maboresho yalivyanywa na Uefa ni hivi hapa " Imekubaliwa kuwa washindi wa taji la Europa LEAGUE watafuzu moja kwamoja kuanzia mwaka wa 2015 katika Champions League katika msimu utakaofuata. Uamuzi huo mpya unalenga kuimarisha na kuifanya Europa League kuwa yenye kuvutia kwa vilabu. Pia imekubaliwa kuwa timu 16 kutoka nchi 12 zitapewa vibali vya moja kwa moja vya kuanza katika awamu ya makundi ya kinyang'anyiro hicho. Kwa sasa timu sita kutoka mataifa sita hufuzu moja kwa moja katika awamu ya makundi ya Europa league.



Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score