Wednesday, March 12, 2014

Buyern Munchin Kulimwa Zaidi Ya £50,000 Baada Ya Kuonyesha Bango Linalosomeka Kuwa Ozill Ni Shoga..

Bayern Munich huenda ikaadhibiwa vikali na Shirikisho la Soka Ulaya, Uefa baada ya mashabiki kuanika bango lililodai kuwa Mesut Ozil wa Arsenal ni shoga.


Hili ndilo bango waliloweka mashabiki wa Munchin Wakimtukana Ozill Picha kwa msaada wa 
Kalbu hiyo ya Ujerumani huenda ikakumbana na rungu la Uefa kwa kupigwa faini itakayofikia Euro 50,000 baada ya mashabiki wake kuonyesha bango linalomtusi kiungo huyo wa Arsenal..

Bango hilo lililoanikwa katika uwanja wa Allianz Arena katika mechi ya kufuzu robo fainali ya Uefa lilikuwa na maandishi 'Gay Gunners’ na mchoro wa kiungo wa Arsenal, Ozil kando yake akiwa ameinama.Licha ya kupewa kipaumbele na kocha wake katika kikosi cha Ujerumani, viwango vya soka vya Ozil vimetiwa shauku na mashabiki na vyombo vya habari nyumbani tangu alipohamia Emirates kutoka Real Madrid.


Mnamo Disemba, Uefa ilipiga Celtic faini ya Sh6 milioni baada ya bango lililokuwa na maandishi tata kuanikwa uwanjani Celtic Park katika mechi dhidi ya AC Milan.

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score