Wednesday, July 9, 2014

Brazili Wanyolewa Bila Maji Wembe Uliotumika Ni Chuma Cha Ujerumani.

Brazili Imeondolewa Hapo jana Katika Mechi Ya Nusu Fainali Kwa Kichapo Cha Mbwa Wa Sokoni Pale Ilipokandamizwa Mabao 7:1.
Timu Hiyo Iliyoandaa Kombe La Dunia Kwa Mbwembwe Nyingi Iliweza Kubanduliwa Na Wajerumani Usiku Wa Jana.

Umakini wa vijana wa Joachim Low ulikuwa wa kupigiwa mfano walipoiadhibu Brazil na kuwa timu ya kwanza kuwahi kushindwa kwa mabao mengi zaidi katika hatua hiyo ya nusu fainali ya kombe la dunia.
Kabla ya mechi hiyo vyombo vya habari vilikuwa vimemulika mfumo wake Luiz Felipe Scolari vikidai alikuwa ameumba timu yake kumtegemea Neymar.
Kujeruhiwa kwa Neymar Ijumaa iliyopita ilimlazimu Scolari kubadili mfumo ambao sasa haukuwa na nyota huyo.

Hebu Fuatilia Linki Ifuaatayo Kuweza Kutazama Magoli Yalivyokuwa Yakiminika.
http://www.fifa.com/worldcup/videos/highlights/match=300186474/index.html

Monday, July 7, 2014

Angalia Hali Ilivyo Katika Jiji La Nairobi Hivi Leo 7/7/Day

Wanausalama Wakimsachi Mfuasi wa CORD Kabla Ya Kuingia Uwanjani

Vijana Wa CORD Wakiandamana Kabla Ya Mkutano Kuanza


Wanausalama Wakiwa Kila Kona Kuhakikisha Usalama Katika Uwanja Wa Uhuru Park
Kwa hapa Chini Jaribu Kuangalia Video Ya Vijana Walioandamana Kabla Ya Mkutano Wa Cord Kuanza Hii Leo.
Zaidi Ya Maafisa Usalama 15000 Waliwekwa Katika Mwa Jiji Kwa Ajili Kulinda Usalama.

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score