Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kitaifa ya
kupambana na matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya (Nacada)
amekashifu vikali matukio yaliyoshuhudiwa wikendi katika Kaunti ya
Machakos na kuyataja kuwa maovu kuliko yaliyoshuhudiwa Sodoma na Gomora.
“Siwezi hata
kueleza...hayawezi kuelezwa na binadamu yeyote mwenye akili timamu. Yale
yaliyotendwa mchana peupe na vijana kwenye uwanja wa kanisa ni mabaya
zaidi ya yaliyoshuhudiwa Sodoma na Gomora,” alisema.
Maelfu ya vijana
walimiminika Machakos Jumamosi kuhudhuria mchuano wa raga, maarufu kama
Masaku 7s, na kujistarehesha mjini humo usiku kucha hadi Jumapili.
Hata hivyo,
yaliyoshuhudiwa yalibaini vijana wengi hawakuwa na haja ya kushuhudia
mchezo huo bali walivutiwa na uhuru wa kutenda anasa ambao umekuwa kama
kawaida wakati michuano hiyo ya raga inapoandaliwa.
“Baada ya
kulewa, kulingana na habari nilizopokea, waliingia kwenye uwanja wa
kanisa na kutishia kuchoma kanisa kama hawangeruhusiwa kufanya maovu yao
ndani ya uwanja wa kanisa,” akasema Bw Mututho.
Unywaji wa
pombe kupita kiasi pamoja na utendaji wa ngono kiholela huwa ni kati ya
anasa zinazovutia vijana wengi kwenye hafla hiyo.
Wakati
mwingine, mtu yeyote hujitolea kuwa 'mhubiri’ ambaye 'hufunganisha ndoa’
watu wawili, ili kuwawezesha 'kuishi kama mume na mke’ japo kwa usiku
mmoja tu.
Ingawa
michuano hiyo imewahi kuandaliwa katika miji tofauti ikiwemo Nakuru na
Nairobi, vituko vya Machakos vilishangaza wengi kutokana na jinsi
viliangaziwa pakubwa hasa kwenye mitandao ya kijamii.
Kuvua nguo
Baadhi ya waliokuwepo Machakos walionekana wakijitokeza na kuvua nguo zao mbele ya hadhara.
Bw Mututho
alieleza wasiwasi wake kuwa huenda kulikuwepo watoto wenye umri wa chini
ya miaka 18 mahali hapo, na kuongeza tabia hiyo haitaruhusiwa kwenye
hafla zingine zilizopangiwa kufanyika Nakuru, Meru na Kakamega baadaye
wiki hii.
Alisema
ingawa Gavana wa Machakos Dkt Alfred Mutua alikuwa na wazo zuri
alipoandaa hafla hiyo, kuna walioingilia na kuitumia kuuzia watoto
pombe.
Alitoa maoni
hayo siku moja baada ya Tume ya Kitaifa ya Huduma za Watoto (NCCS) kutoa
wito kwa serikali ipige marufuku disko za mchana, maarufu kama 'jam session’ ambazo hulenga wanafunzi wanapofunga shule.
Tume hiyo
ilisema disko hizo hutumiwa kuuzia watoto pombe na dawa za kulevya, huku
wengine wao wakishawishiwa kirahisi kushiriki ngono na watu wazima.
Maoni Ya Blogger/Mwandishi
Naomba wasomaji wa blogu hii ambao hamjazoea kuyaona maneno kama haya hapa na picha za kutisha kama itakavyoonekana.. Nimelazimika kuonesha picha kadhaa ambazo nadhani ndio jambo kila mtu anatakiwa kulikemea, Pia lakini nilijaribu kufanya hivyo ili jamii ijue hatari iliyoko mbele yetu.. Kwani tukifichiana maofu kama haya kifo itatuuumbua..
Naomba Chukua Mda kidogo kuangalia baadhi ya picha/taswira ilivyokuwa usiku huo kwenye hafla hiyo.Kama uko karibu na under 18 please usifungue...
Kumbuka Sii Haiba Yetu kuandika Habari kama hizi lakini tunataka kukemea tabia kama hizi katika jamii.
0 maoni:
Post a Comment