Thursday, June 19, 2014

Jela: Jela Ni Mahali Kila Mtu Anaogopa Lakini Kwa Wakazi Wa Hindi Lamu Iliwabidi Wakimbilie Kutafuta Usalama Hapo Jana

HALI ya taharuki ilighubika kijiji cha Hindi hapo
Jumanne baada ya uvumi kuenea kwamba watu
wasio wa kawaida walionekana wakizurura mjini
humo.
Wengi wa wakazi walilazimika kuhama majumbani
mwao na kukimbilia katika jela ya Hindi wakitafuta
usalama.
Shughuli za kibiashara
zilisitishwa kwa takriban
masaa sita huku wenye
maduka na vituo vya
mafuta wakilazimika
kufunga biashara zao kwa
kuhofia usalama.
Chifu Mkuu wa eneo hilo,
Bw Abdalla Shahasi, alilazimika kuitisha mkutano
wa dharura mjini Hindi ili kutuliza hali.
Vikosi vya askari wakiwemo GSU na askari tawala
ilibidi wasambazwe mjini Hindi na viungani mwake
ikiwemo Ndeu na maeneo ya karibu ambapo
wavamizi walidaiwa kuonekana.
Baadhi ya wakazi pia walihama mijini mwao na
kukimbilia misituni na familia zao mara tu baada ya
taarifa za kuonekana kwa wavamizi kuwafikia.
“Watu walianza kuhama wakihofia usalama baada
uvumi kuenezwa eti watu wasio wa kawaida
walionekana karibnu na Hindi. Maduka yalifungwa
kwa muda. Ilibidi niitishe mkutano. Ninawasihi
wakazi wasiwe na shaka. Tayari polisi wameshika
doria na Hindi ni salama,” akasema Bw Shahasi
kwa njia ya simu.
Wakazi aidha wametakiwa kuwa makini na kupiga
ripoti haraka iwapo watashuhudia tendo au mtu
yyeyote wanayeshuku kuwa tisho kwa usalama.
Aidha wageni wote wanaoingia Hindi na viungani
mwake pia wametakiwa kujisajili kwenye afisi ya
chifu kwanza huku wakionywa kutopuuza sheria
hiyo.
Eneo la Hindi ni takriban kilomita 45 kutoka
Mpeketoni ambapo watu zaidi ya 50 waliuawa
katika shambulizi la Jumapili usiku huku zaidi ya
nyumba 30 na magari zaidi ya 20 yakiteketezwa.

Tuesday, June 17, 2014

Kauli Ya Rais Kenyatta Baada Ya Mashabulizi Mfululizo Lamu

Kauli ya Rais Kenyatta inakuja kupitia kwa
televisheni siku moja baada ya kundi hilo kukiri
kufanya mauaji yaliyotokea Mpeketoni Jumapili
usiku.
Kenyatta emesema kuwa kuna ushahidi kuonyesha
kuwa shambulizi hilo lilipangwa vyema na kwamba
wanasiasa walihusika nao.
Al Shabaab lilikiri katika taarifa kwa vyombo vya
habari kuwa ndilo lilifanya mauaji hayo Jumatatu
jioni.
Alisema kuwa ujasusi ulitolewa kuwa mashambulizi
hayo yangefanyika lakini hawakuchukua hatua
zozote kuzuia mashambulizi hayo.
Rais amesema kuwa maafisa waliohusika tayari
wameachishwa kazi na kwamba watashitakiwa.
Wmaesema kuwa wanachunguza wanasiasa
waliohusika na mauaji hayo.
Mauaji zaidi yalifanyika usiku wa kuamkia leo licha
ya taarifa ya Al Shabaab kusema kuwa
washambuliaji walioshambulia Mpeketo walikuwa
wamerejea salama nchini Somalia.
Uharibifu mkubwa ulishuhudiwa katika mji huo huku
washambuliaji wakichoma hoteli na kituo cha polisi
pamoja na kuteketeza magari waliyoyatumia kwa
usafiri wao.
Kenyatta amesema kuwa kuna baadhi ya
wanasiasa wanaochochea uhasama miongoni mwa
jamii.

Monday, June 16, 2014

Simanzi Kenya, Al-shabab Yashambulia Mpeketoni Lamu Watu Kadhaa Waripotiwa Kuuwawa

Kuna Habari Ya Simanzi Iliyotokea Usiku Wa Jana.

Wanamgambo Wa Al-shabab Waliuteka Sehemu Ya Mji Wa Lamu iitwayo #Mpeketoni.
Habari Kutoka Huko Ni Kwamba Watu Wafikao 26 Wameaga Baada Ya Kushambuliwa wakiwa Hotelini.

Majamaa Wenye Risasi Walivamia Hoteli Mbili huko #Mpeketoni na Kuwaua watu hao.
Hayo Yalisemwa Na Deputy Commissioner Wa Eneo Hilo.

Poleni Sana Wakenya Na Mungu Awatie Nguvu Familia Za Jamaa Walioaga.

Kwa Habari Zaidi Zitakujia Kupitia Mchimbariziki.com


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score