Saturday, January 11, 2014

Seneta Wetangula Ashambuliwa Jijini Nairobi.

Moses Wetangula, seneta mteule wa Kaunti ya Bungoma, alinusurika kuuwawa siku ya Alhamisi (tarehe 9
Januari) pale watu wenye bunduki wasiojulikana walipomfyatulia risasi kwa gari lake jijini Nairobi.

Wetangula alikuwa akiendesha gari kurudi nyumbani kwake Karen kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA),ndipo pale risasi alipovurumishiwa risasi kadhaa kutoka kwenye gari iliyokuwa imeegeshwa ng'ambo ya barabara ya Mbagathi Way.

Aliandika maelezo kwenye kituo cha polisi cha Kilimani baada ya mkasa huo, akisindikizwa na waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga, na
msemaji wake, Maseme Machuka.

"Nachukulia hili kuwa ni jaribio la mauaji. Polisi wanapaswa kufanya haraka kufanya uchunguzi
juu ya jambo hili," alisema Wetangula.

Mkuu wa Polisi wa Kaunti ya Nairobi, Benson Kibue, alikiambia kituo cha Capital FM kwamba
polisi watachunguza tukio hilo.

"Hatulichukulii jambo hili kirahisi, maafisa wetu wanafanya kila liwezekanalo kuwakamata washambuliaji," alisema.

Mchimba Riziki

Al-shabab Yakanusha Taarifa Ya KDF

Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) lilisema siku ya Ijumaa (tarehe 10 Januari) kuwa ndege zake za
kivita zililenga kambi ya mafunzo ya al-Shabaab katika mkoa wa Gedo siku ya Alhamisi, na kuua
angalau wanamgambo 30 wa al-Shabaab, wakiwemo makamanda wa juu.

"Mamia ya wengine walikimbia wakiwa na
majeraha mengi.

Zaidi ya magari matano na
zana muhimu viliharibiwa," ilisema KDF kupitia Twitter.
Msemaji wa Al-Shabaab Abdiaziz Abu Musab alikanusha madai ya KDF.

"Hatuna majeshi yaliyopo hapa. Hakukuwa na wapiganaji wa al-Shabaab katika eneo hilo na
hakuna mtu wetu yeyote aliyeuawa," Abu
Musab alisema.

Friday, January 10, 2014

AFUFUKA HOAPITALINI BAADA YA KUNYWA SUMU

Wananchi wa Kenya wameshangazwa na
taarifa ya mwanamume mmoja aliyedhaniwa kuwa mfu kufufuka kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali moja mjini
Naivasha umbali wa kilomita tisini kutoka mji
mkuu Nairobi.

Mwanamume huyo Paul Mburu mwenye umri wa miaka 24, alipelekwa hospitalini kwa matibabu baada ya kunywa sumu kwa lengo la kujitoa uhai,kutokana na ugomvi wa kinyumbani na babake ingawa alisemekana kufariki Jumatano usiku wakati akipokea matibabu.

Wafanyakazi wa hospitali hiyo walipigwa na butwaa na hata kutoroka walipoona mwili wa mtu aliyedhaniwa kufariki ukisonga na kuonyesha dalili za kuwa hai katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Afisaa mkuu wa matibabu katika hospitali hiyo ya wilaya, Dokta Joseph Mburu, alisema kuwa
dawa iliyotumiwa kumtibu Mburu hufanya moyo
kupiga polepole hali ambayo huenda ilimfanya
muuguzi kudhani kuwa mgonjwa alikua amefariki.

Mwanamume huyo alisikika akimtaka mmoja wa
wafanyakazi katika chumba cha kuhifadhia maiti kumsaidia kwani alikuwa anahisi baridi kali na
hapo ndipo mmoja wa wafanyakazi alipotimua mbio kwa hofu.

Nusura Mburu awekwe kwenye jokovu la kuhifadhia maiti.

Jamaa za mwanamume huyo akiwemo babake walikuwa wametembelea chumba cha maiti siku ya Alhamisi ili kujiandaa kwa mazishi , lakini baadaye mchana walifahamishwa kuwa Mburu
alikuwa hai.

Source BBC

Wednesday, January 8, 2014

Zitto ashinda kesi yake ya kutojadiliwa

Mh. Mbunge Z.Z.Kabwe

Aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ameshinda
maombi yake dhidi ya chama hicho
mahakamani.
Katika maombi hayo namba 1 ya mwaka 2014,
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, aliiomba Mahakama Kuu, Kanda ya
Dar es Salaam kuizua Kamati Kuu (CC) ya
Chadema kumjadili au kuchukua uamuzi
wowote kuhusu uanachama wake.

Zitto kupitia kwa Wakili Albert Msando
alikuwa akiiomba Mahakama itoe zuio hilo la
muda hadi kesi yake ya msingi
itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Katika uamuzi wake jana, Mahakama Kuu
ilikubaliana na maombi na hoja za Zitto na
kutoa zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema na au
chombo chake chochote cha uamuzi kumjadili
na kutoa uamuzi wowote kuhusiana na
uanachama wake, hadi kesi yake ya msingi
itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Awali, Mawakili wa Chadema wakiongozwa na
Mwanasheria Mkuu, Tundu Lissu na
Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za
Binadamu, Peter Kibatala walipinga maombi
hayo wakidai kuwa hayajakidhi matakwa ya
kupewa zuio la muda.

Katika uamuzi wake, Jaji John Utamwa
alikubaliana na hoja za Wakili Msando kuwa
maombi hayo yametimiza matakwa yote ya
kupewa zuio hilo.

Matakwa hayo ni pamoja na kuwapo kwa
mgogoro baina ya pande mbili, hasara au
madhara yasiyoweza kufidiwa na usawa
katika athari kwa pande zote.

Jaji Utamwa alikubaliana na hoja za Wakili
Msando kuwa iwapo Mahakama haitaingilia
kati na kutoa zuio hilo, mtoa maombi
ataathirika zaidi kuliko wajibu maombi.

Akijibu hoja ya Wakili Lissu aliyepinga hoja
ya mtoa maombi kuathirika pamoja na
wananchi wa jimbo lake kwa kukosa
uwakilishi bungeni, kuwa hata akipoteza
ubunge kwa kuvuliwa uanachama utaitishwa
uchaguzi mdogo, Jaji Utamwa alisema
uchaguzi mdogo huwa unachukua mchakato
mrefu.

Baada ya kurejea vifungu mbalimbali vya
sheria, kanuni, amri na uamuzi wa kesi
mbalimbali za Mahakama Kuu, Mahakama ya
Rufani na za nje, Jaji Utamwa alisema
anakubaliana mtoa maombi.

“Kwa hiyo ninatoa zuio la muda kwa Kamati
Kuu ya Chadema na au chombo chake
chochote cha uamuzi kwamba kisimjadili na
kutoa uamuzi wowote dhidi ya mleta maombi
kuhusiana na uanachama wake kusubiri
kusikilizwa na kuamuriwa kwa kesi yake ya
msingi,” alisema Jaji Utamwa.

Kabla ya kufikia uamuzi huo, Jaji Utamwa
alitupilia mbali hati ya kiapo kinzani ya
Chadema iliyotolewa na Wakili Kibatala baada
ya kuwekewa pingamizi na Wakili Msando
ambaye alidai kuwa katika hati hiyo, kuna
taarifa za kusikia ambazo hakueleza
alipozitoa.

Mchimba Riziki

KIONGOZI WA UPINZANI MBARONI KWA KUMCHAFULIA JINA RAIS.

Rais Satta

Kiongozi mmoja wa upinzani nchini Zambia,
amekamatwa na kufunguliwa mashitaka ya
kumchafulia jina Rais wa nchi hiyo Michael
Sata baada ya kumfananisha na Viazi.

Frank Bwalya anadaiwa kumtaja Rais Michael
Sata kama "chumbu mushololwa" kupitia kwa
Redio siku ya Jumatatu.

Katika lugha ya Bemba, tamko hilo lina
maanisha viazi vitamu ambavyo humegeka
vinapopikwa , maana ya ndani ikiwa mtu
ambaye hasikilizi ushauri wa wengine.

Bwana Bwalya anakabiliwa na kifungo cha miaka
mitano jela ikiwa atapatikana na hatia.

Aidha Bwalya ni kasisi wa zamani na mfuasi wa
zamani wa Rais Sata, ingawa sasa anaongoza
chama cha muungano wa vyama vya upinzani
(Alliance for a Better Zambia (ABZ).

Naibu waziri wa mambo ya ndani, Stephen
Kampyongo alisema kwamba, bwana Bwalya
alikamatwa kwa kutoa matamshi ya kumharibia
sifa Rais Sata.

''Rais Sata ni yule yule aliyekuwa anasikika
kwenye vyombo vya habari akiwachafulia
sifa marais wa zamani, Banda na Mwanawasa
na hakuna aliyemkamata,'' alisema katibu mkuu
wa chama cha ABZ Eric Chanda.

Viongozi wa upinzani wametaka Bwana Bwalya
aachiliwe wakisema kuwa yeye ni mwanasiasa
asiyemuogopa mtu.
'

Waliongeza kuwa matamshi ya Bwalya, "chumbu
mushololwa" hayakuwa matusi.
Mnamo mwezi Sepetamba mwaka jana Nevers
Mumba mwanasiasa mwingine wa upinzani,
alihojiwa na polisi kwa kusema Rais Sata ni
muongo.

S. BBC SWAHILI

MCHIMBA RIZIKI

Tuesday, January 7, 2014

Leo ilikuwa ni siku ya Mh.Raila Amolo Odinga


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score