Wednesday, June 12, 2013

Hekalu la Freemasons Lavunjwa na vitabu kuchomwa na watu wasio julikana nchini kenya..

Hekalu la Freemasons Lavunjwa na vitabu  kuchomwa na watu wasio julikana nchini kenya..POLISI mjini Nyeri wanachunguza kisa ambapo watu wasiojulikana walivunja na kuchoma vitabu vya kidini katika Mt Kenya Masonic Temple Jumatano asubuhi

Mwangalizi wa hekalu hilo Bw Daniel Gachanja alisema kuwa alikuwa anaenda kuzima stima za usalama alipoona moshi ukitoka ndani ya hekalu.
“Nilizunguka uwanja hadi saa kumi na moja kaso robo nilipoenda kulala. Niliamka saa kumi na mbili kuzima stima na ndipo nilipoona moshi mwingi ukitoka ndani ya hekalu,” alisema.
 Bw Gachanja alielezea kuwa alizunguka hekalu alipoona mlango mmoja ukiwa umefunguliwa kisha akawapigia wanachama huku akizima umeme.
 Alisema kuwa alishuku kulikuwa na mtu aliyekuwa akichunguza mwendo wake wakati wa usiku ambaye aliingia ndani na kuchoma vitabu na vyombo vingine vya kidini.
 Naibu wa OCPD wa Nyeri Zacchaeus Ng’eno alisema kuwa waliongia hawakuwa na nia ya kuiba kwani hakuna chochote kilichoibiwa.


“Nadhania aliyetenda kitendo hiki ni mtu ambaye ameshawahi kuingia ndani wakati mmoja,” alisema aliyekuwa mkuu wa hekalu ya Nyeri Jogginder Sokhi. Akiongea na waandishi wa habari leo hii katika hekalu hilo Bw Sokhi alisema kuwa vitabu ambavyo vilivyochomwa ndani ya saduku kubwa la chuma havikuwa na dhamani.
 Walioingia walitumia ngazi ambayo iliwachwa ikiwa imeegezwa kwa ukuta kando na dirisha na kiuvunja.
Polisi wanashuku kuwa waliongia waliingilia kupitia kwa shamba la jirani kwani lango kuu halikuwa limefunguliwa.

“Watu wengine husema kuwa sisi humuomba shetani lakini tunasoma Biblia na vitabu vingine vya dini zingine,” alisema Bw Sokhi akionyesha kipande cha Bibilia iliyochomwa. Bw Sokhi aliongezea kuwa hakuna mtu ambaye sio mmoja wao ambaye anaweza kuingia ndani.

 Alisema kuwa alishtuka jinsi watu walivyoingia ndani akiongezea kuwa wenyeji waliojenga jengo hilo hawajawahi kuingia tangu walipomaliza kulijenga mwaka wa 2008.

 “Hatujui kama kuna mtu wa nje ambaye ameshawahi kuingia wakati hatuko lakini hawezi kuwa mmoja wetu kwani huo sio undugu,” alisema.

 Polisi walifanya uchunguzi wa kina baada ya habari hizo kupata chupa moja ya kileo cha whisky iliokuwa imetumiwa ikiwa imeondolewa na kuwekwa karibu na jikoni.

Hekalu ya kwanza ilichomwa kama miaka kumi iliyopita na watu wasiojulikana kabla hatujajenga hii mwaka wa 2008.
 Wakati huo mwingine walichoma hekalu wakidhani tuko ndani,” alisema Bw Sokhi.

Isipokuwa ukumbi wa Nairobi, kuna hekalu zingine za Freemason mijini Nakuru, Kisumu, Kitale, Kericho, Naivasha, Eldoret, Nyeri na Mombasa.


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score