Sunday, March 24, 2013

NENO LA LEO JUMAPILI

HABARI ZA MWANADAMU
Tusome Isaya 40:6-8 na Zaburi 8:3-8. Sikiliza sauti ya mtu asemaye, “Lia kwasababu wote wenye mwili ni majani ambayo hukauka na maua yanayonyauka, bali Neno la Mungu litasimama milele.”
Mwanadamu maisha yake ni mafupi, kwahiyo acha maringo, majivuno, kujisifu kwaajili ya pesa yako au mali zako, bali jisifu kwaajili ya utukufu wa Mungu.
 
 Mwanadamu ni mavumbi, na kumbuka tutarudi mavumbini. Huu ni muda wako wa kufanya kazi ya Mungu kabla hujarudi mavumbini kwani hujui ni saa ngapi na lini utakuwa mavumbi.
 
 Kuna watu baada ya kupata mafanikio wanaanza kujidai na kuringa kutoka na kidogo ambacho Mungu amempa. Mafanikio yako siyo kwaajili ya wewe kuonyesha kiburi na kuwalingia wengine. Mungu amekupa hayo mafanikio ili ufanye kazi yake.
Kumbukeni wanadamu kuwa tulizaliwa uchi na tutarudi uchi. Unapozaliwa duniani unakuwa huna nguo yoyote kutoka kwa Mungu na baada ya kuzaliwa unapata nguo kutoka kwa ndugu na jamaa zako ili zikusitiri. Unapofika muda muda wako wa kutoweka hapa duniani nguo zako na mali zako unaziacha na wengine wanaaza kuzitumia. Kwahiyo tuache kujivunia na vinavyoonekana hapa duniani havitatusaidia lolote siku ya hukumu. Vitu vyako vifanye kazi ya Mungu Baba.


Mungu alikupenda wewe mwanadamu na kukupa upendeleo mkubwa ukifananisha na wanyama wakubwa kama tembo na simba aliowaumba. Iweje leo umsahau Mungu na kuona wewe ndio kila kitu hapa duniani. Kumbuka upo kwa neema ya Mungu.
 
MASENGENYO MAKANISANI
Makanisani na majumbani kumejaa masengenyo, ambayo yanataka kudondosha kanisa na kuwavunja moyo watu kufika kanisani. Maneno magumu yamekuwa yakizungumzwa na wanadamu makanisani yenye kuleta machafuko ya kutenganisha kanisana. Makanisa yamekuwa yanakosa waumini kutokana na maneno yako machafu.
 
 KUTOMLILIA MUNGU BAADA YA MAFANIKIO
Watu hawapendi kumlilia Mungu baada ya kupata mafanikio. Mungu amewabariki kwa kumiliki magari, kujenga nyumba nzuri, kuwa na ofisi nzuri, kuoa au kuolewa, lakini wamemsahau Mungu aliyewapa. Waswahili wanasema hujafa hujaumbika. Kumbuka kulikuwa na watu wenye majina makubwa sana kama Price Diana lakini sasa hayupo dunia na historia yake inasaulika. Untafika muda wako wa kutoweka hapa duniani na watu watakusahau, na kama hukufanya kazi ya Mungu, naye Mungu atakusahau katika ufalme wake.


ACHANA JEURI NA DHARAU
Ewe mwanadamu achana na jeuri, kiburi havitakusaidia lolote na kumbuka ni wapi Mungu amekuokota. Ulikuwa huna kitu na ulikuwa mwaminifu kwa Mungu, lakini leo unamdharau Mungu wako baada ya kufanikiwa. Na wengine wanamdaharau Mungu kutokana na kutopata kile ambacho walikuwa wakikiomba kwa muda mrefu bila mafanikio. Kumbuka uvumilivu wako unaweza kukuwezesha kufanikiwa kwa kile unachokihangaikia. Duniani na mahali pa kupita, ukae katika hofu ya Mungu

KUTUMIA KIPAWA CHAKO KATIKA KAZI YA MUNGU
Mungu anataka kutumia kipawa alichokupa kwaajili ya kazi yake. Mungu amegawa kipawa kwa kila mtu, na anatamani kitumike katika kazi yake. Unaweza ukawa ni mzuri katika uandikaji, uimbaji, utungaji, mbunifu, uombaji, mshauri, mtu wa kucheza na kompyuta n.k. Kwahiyo Mungu antaka hivyo vipawa katika nyumba yake.
 
 MANENO MAKALI MAKANISANI
Watu wamekuwa wakihama makanisa kutokana na maneno yako makali yenye kuvunja moyo. Umekuwa ukiwasengenya waumini wenzako na kuwasemea maneno mabaya kwa marafiki zako. Msichana akipendeza kanisani, yanaanza maneno kuhusiana na kupendeza kwake. Maneno hayo yanapomfikia mhusika yanamvunja moyo na kuamua kuhama kanisa na wengine kuacha kabisa kufika kanisani. Unavyofanya hivyo unamkosea Mungu wako.
 
 KUWAONEA WAPOLE MAKANISANI
Tusome Isaya 54:17, Kuna watu wamekuwa wakionewa kutokana na upole wao. Kuna watu ambao ni wapole na hawawezi kuongea maneno mabaya na wwamekuwa waaminifu katika kazi ya Mungu. Kutokana na upole wao, kuna hawa wanadamu wanakuja na kuwasemea maneno mabaya na kuwarudisha kiimani.
 
WANADAMU NI MAREHEMU WATARAJIWA
Mwanadamu ni nani mpaka Mungu akukumbuke. Sisi ni marehemu watarajiwa au walemavu watarajiwa. Kuna watu wanapata maumivu makali sana majumbani mwao na wengine wako mahospitalini, lakini wewe bado uko hai na huna tatizo lolote, sasa kwanini unapenda kumuuzi Mungu wako ambaye anauwezo wa kukufanya lolote na usimfanye lolote.
 
 
MSHUKURU MUNGU NA KAA KATIKA UWEPO WAKE.
Unapaswa kama mwanadamu kumshukuru Mungu na kukaa katika uwepo wake na kuwa na hofu ya Mungu. Kukaa katika uwepo wa Mungu ni kumtafakari Mungu kwa yale anayofanya kwako na kwa wengine. Kukaa katika hofu ya Mungu ni kujaribu kufanya yale Mungu anataka ufanye na kuachana na maovu yote kwa kumuogopa Mungu wako.
 
 
USIDHARAU HUDUMA YA MTU KATIKA KAZI YA MUNGU
Kila mtu ana njia yake ya kumtumikia Mungu kwahiyo usimseme mtu katika huduma yake anayofanya kwaajili ya utukufu wa Mungu. Wewe angalia huduma yako kama inaenda sawasawa na mapenzi ya Mungu. Kusiwe na masengenyo, kuvunjiana mioyo, wivu, mashindano katika kazi ya Mungu.
Wimbo, “Dunia ni maua, hunyauka, utaacha vya dunia, utaenda peke yako”
 
 TUJIADHARA KATIKA NYAKATI HIZI ZA MWISHO
Tupo katika nyakati za mwisho, ambazo ni hatari tujiadhari. Kuna vikwazo vingi vinavyosababisha wanadamu kutotamani kazi za Mungu na pengine kupuuzia pale tunaposikia habari njema kutoka kwa Mungu. Kama mwana wa Mungu na unayetamani kufika mbinguni, usiangalie ya wanadamu bali weka mawazo yako yote na akili yako kwa Mungu, utaona matokeo yake.
 
TENGENEZA KIROHO CHAKO
Unatakiwa kutengeneza kiroho chako kwa kuhudhuria ibada zote, kuimba, kusoma Neno la Mungu. Tusiwe watu kama wa mataifa ambao hawamjui Mungu.
 
 HOFU KWA WATOTO WA MUNGU KANISANI
Watu wanakuwepo katika nyumba ya Bwana lakini wanakuwa na hofu na maneno mabaya yanayotoka katika nyumba ya Bwana. Kanisa sio kila mtu ni mwema, kuna wengine ni wabaya sana na wapo kanisani. Kazi yao ni kuhakikisha jina la Kristo linarudi nyuma kwa kuwakwaza watu wa Mungu.
 
FAIDA ZA UNYENYEKEVU
Kila mtu anayemnyenyekea Mungu na kufanya vile Mungu anataka hubarikiwa. Hakuna cha kujivuniania duniani. Hapa duniani kuna habari mbaya sana kwa mfano kifo. Kuepuka na hofu hiyo ni kufanya yaliyo mema ili hata ukifa siku ya mwisho utamuona Mungu na kufurahi naye.
Roho zetu ziko mikononi mwa Mungu, kwahiyo tusiangalie ya kesho ila tuseme, “Mungu akipenda, tutaonana kesho”
 
 
Wimbo: “Sio mimi ninaishi, bali Yesu ndani yangu, Yu hai Yu hai Yu hai”
 
 Tumwabudu Mungu, Tumtukuze Mungu, Tumtumikie Mungu.
 
 Wimbo, “Tengeneza maisha yako, utakufa utaviacha”
 
 MUNGU AKUBARIKI
 
KWA MSAADA WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD
NA MCHUNGAJI  DR.GETRUDE RWAKATARE....... 
 
 
 
 

 

KENYA YAFANYA KWELI YAIBANA NAIGERIA NYUMBANI

Kenya yaibana Nigeria nyumbani kwao

Harambee Stars ya Kenya licha ya kupata mateso tangu wawasili nchini Nigeria kucheza na Super eagles katika mechi ya kutafuta kuingia katika kombe la dunia Jumamosi nusura wawaaibishe mabingwa wa Afrika kwa kutoka sare ya 1-1 huko mjini Calabar , Nigeria.
Timu ya Harambee Stars
Kenya ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga kupitia mchezaji Francis Kahata katika dakika ya 36 kipindi cha kwanza.
Licha ya Sduper Eagles kuwateremsha miamba yake yote kama vile John Obi Mikel na Victor Moses wa Timu ya Chalsea ya Uingereza lakini hawakufua dafu kwa kenya hadi katika dakika za majeruhi ya kipindi cha pili.
Katika dakika hizo za majeruhi mcherzaji Nnamdi Oduamadi aliiondolea Super Eagles aibu kwa kufunga bao na punde tu firimbi yamwisho kumaliza mechi ikapulizwa.
Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ni katika mechi ya kirafiki mwezi Machi ,2011 Mjini Abuja ambapo Super Eagles ilifunga 3-0.
Wakati ambapo harambee Stars ya Kenya ilikuwa karibu sana kuifunga Nigeria ni katika mechi iliyochezwa Januari 12, 1997 wakati timu zote mbili zilitoka sare ya 1-1 mjini Nairobi. Lakini katika mechi ya marudio iliyochezwa Nigeria Juni 7 .1997 Nigeria iliizaba Harambee Stars 3-0. Hii vile vile ilikuwa ni mecchi ya kutafuta nafasi ya kucheza Kombe la Dunia la mwaka 1998.
Miaka iliyopita Nigeria imekuwa ikiipepeta Kenya . Katika mechi ya kutafuta nafasi ya kucheza kombe la dunia mwaka 1986, Harambee Stars walifungwa na Super Eagles 3-0 hii ilikuwa Juni 7, 1985 na baadae kukamilishi kibarua chao na kufaulu kuingia kombe la dunia kwa kuichapa Kenya 1-3
Wachezaji Harambee Stars: Arnold Origi, David Owino, Mulinge Munandi, David Ochieng, Brian Mandela, Victor Wanyama, David Gateri, Johanna Omollo, Jamal Mohammed, Dennis Oliech and Francis Kahata. Coach Adel Amrouche
Wachezaji wa Super Eagles: Vincent Enyeama, Solomon Kwambe, Godfrey Oboabona, Kenneth Omeruo, Elderson Echejile, Sunday Mba, Mikel Obi, Eddy Onazi, Obafemi Martins, Victor Moses and Brown Ideye

Waamuzi

Referee: Joshua BONDO (BOT)
Assistant Referee 1: Meshack MEDUPI (BOT)
Assistant Referee 2: Moemedi MONAKWANE (BOT)
Fourth official: Kutlwano LESO (BOT

TAJIRI WA URUSI AFARIKI

Tajiri wa Urusi afariki



Polisi bado wanachunguza kilichosababisha kifo cha Berezovsky
Kilichosababisha kifo cha tajiri Boris Berezovsky, mwenye umri wa miaka 67, bado hakijajulikana.
Tajiri huyo alikuwa akisakwa mno nchini Urusi, na anafahamika kuwa mpinzani mkali wa Rais
Zamani alikuwa na mamlaka na ushawishi sana katika bunge la Kremlin, lakini yote hayo yalididimia mara tu alipoingia Bw Putin, na Berezovsky alikimbilia Uingereza kuanza maisha ya uhamishoni mwaka 2000.
Awali idara ya polisi ya Thames Valley ilitangaza kwamba ilikuwa katika hatua za kuchunguza kifo cha mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 67, katika eneo la Ascot, Berkshire.
Mwaka uliopita, Bw Berezovsky alishindwa katika kesi ambayo aliwasilisha madai ya kutaka kulipwa pauni bilioni tatu, dhidi ya tajiri anayemiliki klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich.
Bw Berezovsky alidai alitishwa na Bw Abramovich, kiasi cha kuuza hisa za kampuni kubwa ya mafuta nchini Urusi, Sibneft, kwa kiwango kidogo mno cha fedha, ikilinganishwa na thamani halisi ya hisa hizo.
Madai hayo yalikataliwa moja kwa moja na hakimu wa masuala ya biashara mjini London, na ambaye alisema Bw Berezovsky si shahidi wa kuaminika.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya kimataifa, Richard Galpin, alisema watu mbalimbali walimueleza kwamba Bw Berezovsky alisongwa na mawazo kufuatia kushindwa katika kesi hiyo, na kuandamwa na matatizo mbalimbali ya kifedha.
Tajiri huyo mkuu inasemekana alipoteza kiasi kikubwa cha mali katika miaka ya hivi karibuni, na akiwa katika hali ya kulipa gharama mbalimbali za kesi nyingi alizoziwasilisha mahakamani.


 

Rais Putin hakutaka urafiki wa Berezovsky.
Bw Berezovsky pia aliweza kujirundikia mali katika miaka ya 1990, akiuza magari ya Mercedes na vile vile magari mengineyo yaliyoundwa nchini Urusi.
Boris Berezovsky alikuwa kati ya kundi dogo la matajiri wakuu wa Urusi, na ambao walifurahishwa na kuangamia kwa siasa za kikomunisti, na wakitumia
 waliowafahamu katika madaraka ya juu kwa misingi ya kujitajirisha haraka.
 
 Huku mamilioni ya raia wa Urusi wakitumbukia katika umaskini, Berezovsky aliingia katika biashara, na kuuza magari, na pia kununua hisa katika kituo kikuu cha matangazo ya televisheni nchini Urusi.
Aliwekeza pia katika shirika la ndege la Aeroflot, na vile vile katika kampuni ya mafuta.
Vile vile wakati huo alikuwa ni rafiki mkuu wa rais wakati huo, Boris Yeltsin, na uhusiano huo ukampa mamlaka mno katika bunge la Urusi.
Lakini Vladimir Putin akawa ni rais tofauti kabisa, akiwa kiongozi wa Kremlin ambaye hakutaka hata kidogo kuelezewa namna ya kuiongoza Urusi.
Ndipo hapo Berezovsky alipopoteza ushawishi wake katika Kremlin, na kutoroka hadi mjini London.




Source BBC

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score