Thursday, August 29, 2013

AMANI MASHARIKI MWA CONGO BADO NI KITENDAWILI

Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mara ya kwanza kimeshiriki katika mapambano. Hiyo ni hatua inayoelekea katika lengo sahihi
                Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ni sehemu isiyokuwa na utulivu. Mapigano yanatokea mara kwa mara baina ya majeshi ya serikali na makundi ya wanamgambo. Kwa haki kabisa, sasa wakaazi wa eneo la mashariki mwa Kongo wanalitaka jeshi la Umoja wa Mataifa lichukue hatua ili kuyakabili makundi ya waasi.  

Wananchi wataka hatua thabiti:
                                                    Hadi sasa jeshi la Umoja wa Mataifa, Monusco, ambalo ni kubwa kabisa la kulinda amani, kuwahi kuwekwa popote pale duniani, likiwa na askari alfu 19, linakabiliwa na madai ya wananchi wa mashariki mwa Kongo kwamba linashindwa kuutekeleza wajibu wake kwa njia ya ufanisi.
Aghalabu jeshi hilo limekunja mikono nyuma na kutochukua hatua wakati waasi na hata majeshi ya serikali yakifanya vitendo vya kikatili kwa wananchi. Kwa mara ya kwanza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa kupitisha azimio namba 2098, mwezi machi mwaka huu, limefungua njia ya kupeleka jeshi lililopewa jukumu madhubuti la kuweza kupambana na waasi.  

Wanajeshi wa serikali watoa silaha kwa waasi: 
                                                                            Jeshi hilo la Umoja wa Mataifa lenye askari alfu 3 kutoka Tanzania, Afrika Kusini na Malawi sasa linapaswa kuthibitisha kwamba, linawalinda wananchi dhidi ya mashambulio ya waasi ambao baadhi yao wanapewa silaha na wanajeshi fisadi wa serikali. Jeshi la Umoja wa Mataifa linapaswa kuyazuia mashambulio ya waasi wakati mwafaka na pia linapswa a kuwanyang'anya silaha waasi hao ili hatimaye kurejesha amani.
Hakika hilo ni jukumu kubwa. Kwani pamajo na waasi wa kitutsi wa M23 wapo wanamgambo wa kihutu wa FDLR, pamoja na wengine kama vile wa Mai Mai Sambamba na harakati za kulinda usalama , jeshi la Umoja wa Mataifa pia linapaswa kuifanya hali ya kibinadamu iwe bora kwa wananchi. Maalfu kwa malfu ya wananchi walivikimbia vijiji vyao katika miezi ya hivi karibuni. Maalfu wanaishi katika mazingira ambayo mwanadamu hastahili katika kambi au wanajaribu kukimbilia misituni, kujificha ili kuwakimbia waasi .

  Askari wa serikali ni tatizo:
                                              Pana tatizo kubwa linalotokana na wanajeshi fisadi wa serikali,waanaobaka na kupora mali za watu.Sasa ni jambo la mashaka iwapo serikali dhaifu ya Rais Kabila itachukua hatua zinasostahili ili kuleta mageuzi katika jeshi la serikali, badala ya kulitegemea jeshi la Umoja wa Mataifa kuyatatua matatizo kwa niaba yake.

WATU WALIOFARIKI DUNIA KWA AJALI YA NAROK WAFIKA 41

WATU 41 wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa baada ya basi lililokuwa likielekea Homabay kutoka Nairobi kuanguka na kubingiria mara kadha karibu na mji wa Narok. Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu watu wengine 33 walijeruhiwa na wakakimbizwa hospitali ya wilaya ya Narok. Ajali hiyo ilitokea eneo la Ntulele mwendo wa saa saba usiku. Miongoni mwa waliofariki ni watoto wanne. Kamanda wa Polisi wa Trafiki Samuel Kimaru alisema eneo hilo ni hatari na ajali hutokea mara kwa mara. Alisema serikali imekuwa ikiweka alama za kutahadharisha watu lakini alama hizo huibiwa na watu na kuuzwa kama vyuma vikuu kuu. Aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga ameeleza kuhuzunishwa kwake na habari za ajali hiyo na kutuma rambirambi kwa jamaa za waliopoteza maisha. “Nawapa heko polisi na maafisa wa kutoa huduma za dharura kwa kasi yao katika kufika na kusaidia walionusurika, ” alisema kupitia akaunti yake kwenye Twitter. Katibu wa Baraza la Mawaziri Francis Kimemia pia alituma rambirambi zake na kusema “sheria lazima itekelezwe kikamilifu.” Mungu azilaze mahali pema peponi marehemu wote Na awaponye haraka majeruhi. Amen. Endelea kufuatilia muda baada ya muda tutaripoti kila tukipata taarifa zaidi.

Podolski Atia Dosari Sherehe Za Arsenal Kufuzu Kuingia Hatua ya Makundi

LONDON, Uingereza
SHEREHE za Arsenal baada ya kufuzu kwa kabumbu ya Ulaya, Uefa zilitiwa dosari kufuatia jeraha la straika wao, Lukas Podolski. Mjerumani huyo alitolewa nje katika mechi ya mkondo wa pili ya raundi ya kufuzu kwa dimba hilo dhidi ya Fenerbahce ambapo walishinda 2-0. Podolski alifunga bao katika mkondo wa kwanza wiki jana ambapo walishinda 3-0 na sasa vijana hao wameingia hatua ya makundi kwa jumla ya mabao 5-0. Alitolewa nje kwa machela katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili na atakosa mechi zijazo katika Ligi Kuu ya Uingereza. Kushinda mechi hiyo na kujikatia tiketi ya kabumbu ya Uefa kunapunguzia presha kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye amekuwa akishurutishwa na mashabiki kuwanunua wanasoka wapya. Kocha huyo alieleza wasiwasi wake kuhusu mfungaji wa bao katika mechi hiyo, Aaron Ramsey ambaye alimaliza akihisi maumivu kwenye kiuno huku kiungo matata, Jack Wilshere akigongwa kwenye mguu wake katika dakika za mwisho za mechi. “Hizo ndizo habari za kusikitisha usiku huu kwani licha ya kushinda, tumegharamia kwa kumpoteza Podolski kwa jeraha. Sijui kiwango cha jeraha la Ramsey na jinsi Wilshere atakavyopata nafuu na itabidi kuwachunguze zaidi,” Wenger alisema. Zimwi hili la majeruhi limewaandama wanasoka wa Arsenal mara nyingi, pia katika msimu uliopita majeruhi walikuwa wengi katika mwanzo wa Ligi kilichopelekea Arsenal kufungwa magoli mengi katika mzunguko wa kwanza..

Monday, August 26, 2013

MESSI ; JERAHA LINALOMKABILI MSHAMBULIAJI HUYO MATATA WAITIA TUMBO JOTO BARCELONA

Wasiwasi umewakumba mabingwa hao wa Hispania Barcelona kufuatia jeraha linalomkabili mshambuliaji wao matata Lionel Messi.
Mshambuliaji huyo raia wa Argentina ambaye ndie injin ya klabu ya Barcelona aliumia katika mechi ya Spanish Super Cup dhidi ya vijana matata wa Atlatico Madrid jumanne ambayo walitoka sare ya 1-1 .
Katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Vicente Caldeton, Messi alitolewa na nafasi yake kichukuliwa na kiungo Cesc Fabrigas.

Nyota wa Brazil aliwaepusha Barcelona aibu baada ya kufunga bao moja la kusawazisha baada ya nyota wao wa zamani, kuwafunga na kuweka Atletico kifua mbele.
"Messi alitolewa nje akihisi maumivu katika mguu wake wa kushoto baada ya kugongana na mchezaji mwingine wa Atletico"klabu ya Barcelona ileipoti jana katika mtandao wake.
Staa huyo alipata jeraha dogo Wiki jana akifanya mazoezi lakini akapona na kuweza kucheza mechi dhidi ya Levante ambapo walishinda 7-0
Umuhimu wa Messi kwa Barcelona ulijulikana msimu uliopita alipokosa mechi za nusu fainali ya ligi ya mabingwa bara Ulaya dhidi ya Bayern Munich.
Barca walitwangwa jumla ya Mabao 7-0 nyumbani na ugenini.

Mchimba Riziki Sports

WANAUME WAWILI WAKUBALIANA KUMWOA MWANAMKE MMOJA NI HUKO MJINI MOMBASA

KATIKA HALI YA KUSTAAJABISHA WANAUME WAWILI WA UMRI WA MAKAMO,KUTOKA KISAUNI MOMBASA NCHINI KENYA KATIKA HALI YA KUSTAABISHA WALIKUBALIANA KUMWOA MWANAMKE MMOJA NA KUAHIDI KUISHI PAMOJA BILA KUWA NA WIFU WOWOTE KABISA KATIKA NDOA YAO. WALIAMUA KLUFANYA HIVYO BAADA YA KUGUNDUA KWAMBA WALIKWISHWA SHIRIKIANA MWANAMKE HUYO KWA ZAIDI YA MIAKA MINNE. KAMANDA MMOJA WA POLISI ALISEMA YEYE AMESTAAJABISHWA NA HALI HIYO KWANI YEYE AMEZOEA KUSKIA WATU KUPIGANA ENDAPO WATAGUNDUA KAMA WANASHIRIKI MWANAMKE MMOJA. NAE MWANAMKE HUYO ALIPOULIZWA KAMA YUKO TAYARI KUMUACHA MPENZI WAKE YEYOTE ALIKATAA KATA KATA NA KUSEMA HAYUKO TAYARI KUMPOTEZA HATA MMOJA KWANI AMERITHIKA NAO,MAMA HUYO MWENYE MAPACHA ALIDOKEZA ALIPOHOJIWA. WOTE HAO WATATU WALIANDIKIANA NA KUAPA KUTOTHULUMIANA BAADAE NA KILA MMOJA KUSEMA ATAKUWA MWAMINIFU KATIKA NDOA YAO. HAYA MAMBO BADO HAYAJAZOELEKA SANA KATIKA NCHI ZETU ZA AFRIKA HASA AFRIKA MASHARIKI MTINDO HUU WA NDOA NI MPYA KABISA, MTINDO HUU HUITWA POLYANDRY(MWANAMKE KUOLEWA NA ZAIDI YA MWANAUME MMOJA WAKATI MMOJA) AMBAPO SISI TUMEZOE POLIGAMY (MWANAUME KUOA WANAWAKE WENGI) NDOA HIYO ITAKUWA NA WATU WATATU (Mr Steven Mwendwa,Mr Elijah Kimani NA mke wao)

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score