Saturday, May 24, 2014

Hawa Ndio Wasamini Na Waanzilishi Wa Kundi Hatari La Boko Haramu..............

Chapa Za CIA na Boko Haramu
Randy Short mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa nchini Marekani amelituhumu Shirika la Kijasusi la Marekani CIA kwa kuhusika na uundwaji wa kundi la Boko Haram la nchini Nigeria na uungaji mkono wa kifedha kwa kundi hilo linaloendesha ghasia na machafuko nchini humo.

 Randy Short ameongeza kuwa, lengo la Marekani la kuliunga mkono kundi la Boko Haram ni kutaka kuidhoofisha Nigeria na kupunguza ushawishi wa nchi hiyo magharibi mwa Afrika.

Mchambuzi huyo wa Kimarekani ameeleza kwamba, Marekani inadhamini mahitaji ya silaha na fedha ya kundi hilo kupitia Jenerali mstaafu Khalifa Haftar aliyesomea mafunzo ya kijeshi nchini Marekani ambaye hivi sasa anaendesha operesheni za kimapinduzi nchini Libya.

Randy Short ameongeza kuwa, hatua ya Marekani ya kutaka kushiriki kwenye operesheni za kutaka kuwaokoa wanafunzi wasichana wasiopungua 250 wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haram, ni njama za nchi hiyo za kutaka kupenya na hatimaye kulidhibiti eneo la Magharibi mwa Afrika.

Chelsea Kama Ndio Timu Ya Dunia Vile...


RIO DE JANEIRO: Chelsea inaongoza kwa kuwa na wachezaji wengi zaidi katika vikosi vya timu za taifa zitakazoshiriki fainali za Kombe la Dunia.
Mashabiki Wa Chelsea Darajani.
Timu hiyo ina wachezaji 18 na kuzipiku timu nyingine kubwa kama Manchester United na Bayern Munich.

Hata Napoli ya Italia ina wachezaji wengi kuzipiku timu za Barcelona na Real Madrid.
Man United na Bayern kila mmoja ina wachezaji 16 katika vikosi mbalimbali vinavyojiandaa kwa michuano hiyo.
Brazil ambao ndio wenyeji wa fainali hizo wameita kikosini wachezaji wanne wa Chelsea ambao ni Oscar, Willian, Ramires na Davdi Luiz.
Wachezaji wengine wa Chelsea ni Frank Lampard na Gary Cahill walio katika timu ya Uingereza.
Uhispania ina Fernandos Torres na Cesar Azpilicueta wakati Ubelgiji ikiwa na Eden Hazard, Romelu Lukaku na Thibaut Courtois.
Mstaa wengine wa Chelsea kwenye vikosi vya taifa ni Samuel Eto’o (Cameroon), Andre Schurrle (Ujerumani) na Wanigeria -John Obi Mikel, Victor Moses na Kenneth Omeuro.
Kadhalika kuna Mghana Christian Atsu na Patrick van Aanholt wa Uholanzi.
Timu nyingine zenye wachezaji wengi ni pamoja na Barcelona, Real Madrid, Manchester City (13), Juventus, Arsenal, Liverpool (12), Atletico Madrid (11), Porto, Inter Milan, AC Milan, Zenit (10) na Borussia Dortmund, Paris Saint- Germain (8).


Kikosi Kamili Cha Chelsea Brazili Ndio Hiki Hapa Chini.
 Andre Schurrle
Cahill
Cesar
Christian Atsu
Eden
Samuel Etoo
Mikel Obi
Kenneth Omeuro

Lampard
Luis

Lukaku

Victor Mosess

Oscar

Patric van


Ramires


Thibaut Courtois.


Toress

Willian







Tutaongeza Mashambulizi Zaidi Kenya "Ni Faud Mohamed Khalaf" Kiongozi Wa Kundi Haramu La Al-shabab Ameyasema hayo


Kwa mara nyingine kundi la Al Shabaab limeahidi kushambulia Kenya ili kulipiza kisasi kufuatia hatua ya majeshi Kenya kushambulia ngome zake Somalia.
Wapiganaji Wa Kundi La Al-Shabab
Katika kanda ya suati iliyotolewa Alhamisi, mmoja wa viongozi wakuu wa kundi hilo Fuad Mohamed Khalaf alisema magaidi hao wataendesha mashambulizi makali nchini Kenya.

“Tumehamishia vita Kenya, wakiua msichana wa Kisomali tunaua msichana wa Kenya,” alisema Khalaf katika kanda iliyopeperusha na radio ya Andalus.
“Tunatoa wito kwa Waislamu wote nchini Kenya kupigana na serikali ya Kenya ndani ya taifa hilo kwa sababu waliua watu wengi wakiwemo watoto,” alisema.
Majeshi ya Kenya ambayo yaliingia Kusini mwa Somalia 2011 kuzima shughuli za waasi hao, yamejiunga na wanajeshi 22,000 wa Umoja wa Afrika kukomesha oparesheni za kundi hilo la Al-shabab.
Mapema wiki hii majeshi ya Kenya yalishambulia maeneo ya Jilib katika misururu ya mashambulizi yanayoendeshwa na majeshi hayo.
“Wakati maafisa na ndege zao za kivita zinapoua watu wenu, Mungu amewapa idhini ya kulipiza kisasi hivyo tutapigana vikali na Kenya,” alisema Bw Khalaf ambaye anasemekana kuwa na cheo cha pili katika kundi hilo baada ya kiongozi mkuu Ahmed Abdi Godane.
Kundi la Al Shabaab, ambalo lilikiri kuhusika katika shambulizi la Westgate mnamo Septemba 2013 ambapo watu 67 walikufa, limehusika katika misururu ya mashambulizi mengine nchini.
Waasi hao wa Kislamu pia wamekiri kuhusika katika mashambulizi yalioua maafisa kadhaa wa Kenya Jumatatu katika eneo la Mandera.

wengi zaidi wapokea mafunzo ya al-shabab

Kulingana na shirika la AFP Bw Khalaf alisema watu zaidi wamepewa mafunzo na wanachama wa Al Shabaab na kuwa kundi hilo litatuma maafisa zaidi kuendeleza mashambulizi Kenya.

“Tumetoa mafunzo kwa watu ambao ndio walivamia maafisa wa usalama huko Mandera,” alisema na kuongeza kuwa waasi zaidi watatumwa Kenya.
Serikali ya Amerika imetoa tuzo la Dola 5 milioni kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa Bw Khalaf ambaye ana asili ya Somali na Uswidi na anasemekana kuwa mfadhili mkuu wa kundi hilo.

Katanga German Muasi Aliyewafadhli Waasi Congo Ametupwa Gerezani Miaka Kumi Na Miwili

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Ijumaa ilimhukumu aliyekuwa kiongozi wa kivita wa DR Congo Germain Katanga miaka 12 gerezani kwa tuhuma za kuwapa waasi silaha.

German Katanga

Waasi hao wanadaiwa kutekeleza mashambulio ya kikatili katika kijiji kimoja mnamo 2003.
“Mahakama hii imemhukumu Germain Katanga miaka 12 gerezani,” alisema Jaji Bruno Cotte, aliyesoma hukumu hiyo, iliyo ya pili tangu kuasisiwa kwa mahakama hiyo mnamo 2003.
Kulingana na jaji huyo, miaka saba ambayo mshukiwa huyo amekaa katika mahakama hiyo itaondolewa kutoka kwenye kifungo hicho.
Katanga, aliye na miaka 36 alipatikana na hatia mnamo mwezi Machi kwa kuhusika katika ukatili dhidi ya binadamu.
Makosa mengine yaliyomkabili ni mauaji ya kikatili yaliyotekelezwa katika kijiji cha Bogoro, mashariki mwa nchi hiyo mnamo Februari 24, 2003.
Majaji hao walimpata na hatia ya kuwapa wapiganaji wa kundi la Patriotic Resistance Forces (PRFI) silaha katika msitu wa Ituri ambapo watu zaidi ya 200 waliuawa katika shambulizi hilo.
“Makovu ya ukatili huo yangali dhahiri katika kijiji hicho,” akasema Jaji Scott.
Matumizi ya mapanga katika shambulio hilo yalidhihirisha 'ukatili wa hali ya juu na kusababisha mateso makubwa kwa waathiriwa,” akaongeza.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilimwondolea mashtaka ya ubakaji, kuwafanya waathiriwa kuwa watumwa wa kingono na matumizi ya watoto kuwa wanajeshi.
Mahakama Ya ICC
Mawakili wake wamekata rufaa.

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score