Madaya Ya Heroin Yaliyokamatwa. Inasemekana ni zaidi ya Tani moja. |
Mabaharia wa meli ya HMAS Darwin waliingia kwenye boti walioishuku na kugundua madawa yaliyofichwa kwenye mifuko ya saruji.
"Madawa haya sasa yameshikiliwa na na yameharibiwa hapo jana na wanajeshi wa Australia," alisema kamanda Terry Morrison. "Inafahamika vyema kwamba madawa haya yanayasaidia makundi ya kigaidi kifedha ili waweze kufanya matendo yao ya kigaidi."
Meli hiyo ya Darwin imetumwa kwenye Pembe ya Afrika kama sehemu ya Operesheni Slipper, mchango wa Australia kwenye juhudi za kimataifa za kupambana na ugaidi, ulanguzi na uharamia kwenye eneo la bahari la Mashariki ya Kati.
Meli Iliyokuwa Imebeba Madawa Hayo. HMAS |