Thursday, April 3, 2014

Wasifu Wa 'Makaburi'

Wednesday, April 2, 2014

Zimwi La Ugaidi Nairobi... Uchambuzi Kuhusu Kuzorota Kwa Usalama Nairobi..

Wapelelezi wakitafuta ushahidi siku ya Jumanne (tarehe 1 Aprili) kwenye eneo ambapo mlipuko wa bomu ulitokea katika kiunga cha Eastleigh, Nairobi. Milipuko mengine mitatu iliyotokea karibuni kwa wakati mmoja siku ya Jumatatu iliwauwa watu sita na kuwajeruhi wengine kadhaa
Mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni kabisa katika kiunga cha Eastleigh, Nairobi, ambayo yaliuwa watu sita na kuwajeruhi wengine 25 siku ya Jumatatu (tarehe 31 Machi), yamewafanya wakaazi wa mji huo kuwa na hasira na kufikiria ikiwa kweli kuna siku serikali itakayoweza kukomesha tatizo la ugaidi linalozidi kuchipuka.


Milipuko iliyotokea takribani wakati mmoja ililenga mikahawa miwili iliyo kwenye eneo yenye watu wengi kwenye kiunga hicho cha Eastleigh barabara ya 12 second evanue, kiasi cha saa 7:30 magharibi.

Polisi walikuwa bado wanajaribu kutambua aina gani ya milipuko iliyotumika, huku kamanda wa polisi wa Nairobi, Benson Kibue, akisema moja kati ya milipuko hiyo inaweza kuwa bomu la kutengenezwa kienyeji na mashahidi wengine wakisema moja au guruneti zaidi ya moja yalirushwa.

"Tupo hapa kwenye eneo la tukio. Bila ya shaka tunashuku kuwa yalikuwa mashambulizi ya kigaidi," Kibue aliwaambia waandishi wa habari.
"Idadi ya waliojeruhiwa imefikia 25 - wako kwenye hospitali mbalimbali - na tumepata miili saba," alisema.

Wengi ya wale waliojeruhiwa walipelekwa kwenye hospitali za Mother and Child, Guru Nanak, Madina na Hospitali ya Taifa ya Kenyatta.

Mashambulizi hayo yalihusisha maguruneti yaliyovurumishwa kwenye mikahawa miwili - Sheraton na The New Kwa Mzairua Super Grill Centre - zinazotengana kiasi cha mita 300, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Starehe, Barasa Wabomba, ambaye Eastleigh iko chini yake, aliwaambia waandishi.

Mmiliki wa mkahawa ya Sheraton, Patrick Gakuyu, ambaye alinusurika akiwa amepata majeraha madogo madogo, aliwaambia waandishi kwamba mkahawa wake ulikuwa umejaa wateja ambao walikuwa wakila huku wakiangalia taarifa ya habari kwenye televisheni.

Gakuyu, aliyekuwa amechanganyikiwa kila akikumbuka tukio hilo, alisema alikuwa akichukua mahitaji ya mteja mmoja ndipo pale milio miwili mikubwa ilipoukumba mkahawa wake.
"Baada ya mlio huo, sikuona zaidi ya hapo kwa sababu chumba kilitandwa na giza na moshi zito," alisema.

Alipokimbilia kwenye mlango kujiokoa akiwa na wateja wengine waliochanganyikiwa, walishtuka kukuta kuwa washambuliaji waliufunga kwa nje. "Hatimaye tuliuvunja kwa msaada wa wasamaria wema, lakini ni hapo ndipo tulipoelewa balaa zima la mashambulizi," alisema.

"Kulikuwa na damu na vipande vya miili ya wanadamu iliyotapakaa nje ya mkahawa huo, bila ya shaka ikionesha juhudi za wateja kukimbia au kuashiria athari mbaya kabisa ya mlipuko huo," alisema. "Kulikuwa pia na viti na meza zilizovunjika zilizotapakaa kote, vile vile na vitu vya watu kama viatu na simu za mkononi."

Polisi yakamata watuhumiwa 657

Patrick Gakuyu, mmiiki wa Mkahawa wa Sheraton, akiwaelezea waandishi wa habari juu ya hali mbaya aliyoishuhudia nje ya mkahawa wake baada ya mashambulizi siku ya tarehe 31 Machi
Wakaazi wa Eastleigh wenye hasira wanataka majibu kutoka serikalini, wakivituhumu vyombo vya usalama kwa kuwa wazembe katika vita vya nchi hiyo dhidi ya ugaidi.

"Ni siku moja tu [baada] gaidi mmoja kufa kwenye nyumba iliyo kwenye eneo hilo hilo baada ya bomu alilokuwa akiliunda kumripukia," alisema Rosemary Muthoni mwenye umri wa miaka 35, muuzaji wa vitabu visivyo vipya huko Eastleigh.

"Nilitarajia vyombo vya kutekeleza sheria kuchukua tahadhari baada ya makosa ya siku ya Jumapili na kufanya msako wa mlango hadi mlango ili kuwatoa nje magaidi," aliwaambia waandishi, na kupendekeza kama walifanya hivyo, wangeweza kuzuia mashambulizi siku ya Jumatatu na kuokoa maisha ya watu wasio na hatia .

Muthoni alisema watu watatu ambao inadaiwa walikimbia kutoka eneo la tukio siku ya Jumapili katika gari nyeupe inaweza kuwa ndio walioshiriki katika mashambulizi ya mikahawa miwili siku ya Jumatatu.

"Tumechoshwa na mashambulizi haya ya kigaidi yasiyo na mwisho," alisema Joel Kariuki, mwenye umri wa miaka 25, mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya biashara katika Chuo Kikuu cha Nairobi. "Inaonekana hakuna dhamana ya usalama wetu kwa sababu kama makanisa, matatu, baa na migahawa sasa yote yanalengwa na magaidi, basi pengine vyuo vikuu vitafuatia karibuni."

"Hebu serikali ijitahidi katika kukusanya na kuchukua hatua juu ya taarifa za kiintelijensia," aliwaambia waandishi.

Polisi ilianzisha operesheni ya usalama huko Eastleigh kufuatia mashambulizi ya siku ya Jumatatu, na kuwakamata washukiwa 657, alisema Waziri kwa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa Joseph Ole Lenku.

Lenku alisema operesheni zitaendelea mpaka wahusika watakapofikishwa mbele ya sheria, na alitoa wito kwa wakaazi kushirikiana na wafanyakazi wa usalama na kujitolea kwa habari ambazo zinaweza kusababisha kukamatwa kwa watuhumiwa.

"Tendo hili la kiwoga linalofanywa dhidi ya Wakenya wasio na hatia na wapenda amani ambao walikuwa wanafanya shughuli zao za kawaida ni vya kinyama na hatua za haraka zimechukuliwa na vyombo vyetu vya usalama," alisema katika taarifa yake siku ya Jumanne.

Kushindwa vita dhidi ya ugaidi?

Mabaki ya The New Kwa Mzairua Super Grill Centre huko Eastleigh kufuatia mashambulizi ya tarehe 31 Machi. 
Shambulio la Jumatatu linafuatia tukio la tarehe 23 Machi karibu na Mombasa, ambako watu wenye silaha waliingia katika misa kanisani huko Likoni, na kuufyatulia risasi mkusanyiko huo, na kuua watu sita na kujeruhi wengine 17.

Huko Mombasa pia, polisi walikamata gari lililoonekana nchini visivyo halali tarehe 11 Machi, na kugundua wiki mkoja baadaye kuwa lilikuwa na bomba sita za mabomu zilizowekwa katika viti vya nyuma zilizofichwa ndani ya gari hilo.

"Nina wasiwasi kwamba serikali yetu inapoteza vita dhidi ya ugaidi," alisema Angela Kendi, meney umri wa miaka 48, mfanya biashara ndogo ndogo huko Eastleigh. "Mimi nimechoka kusikia vitisho vitupu kwa magaidi kutoka kwa rais, makamu wake na Inspekta Jenerali wa Polisi. Kwa nini hawawezi kuhifadhi tu maneno yao, kuchukua hatua na kuwateketeza watu hawa waovu?"

Alisema kutoa muda wa mwisho kwa magaidi badala ya kuchukua hatua dhidi yao hakujawahi kufanya kazi na inahatarisha hali ya usalama kwa gharama ya maisha, uharibifu wa mali na uharibifu wa uchumi.

Ahmed Ali, mwenye umri wa miaka 33, mwangalizi wa ghala la mavazi katika Eastleigh, anasema serikali inapaswa kukaza doria mpakani na kuvifunga vituo vyote vya kuingia Somalia ili kupata usalama wa nchi.

"Ni wazi kwamba magaidi wa al-Shabaab wamechagua kufanya mashambulizi Eastleigh kwa sababu wanajua eneo hili lina maelfu ya Wakenya wenye asili ya Somalia, na kwa hiyo wana uwezo wa kuchanganyika na sisi kwa urahisi," alisema.

Ali alisema kuwa yeye, kama Wasomali wengine, alikuwa na wasiwasi na mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa wasiokuwa Waislamu na unyanyasaji unaofanywa na vyombo vya usalama.

"Kila wakati magaidi wanapopiga, mambo kama hayo hutokea na tutoweka, kuwepo kwa uzorotaji wa usalama usio wa lazima," aliwaambia waandishi. "Natumaini wakati huu, watakwenda kuwafuata magaidi na kutokomeza janga hili kutoka kwetu."


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score