Friday, February 28, 2014

Kisirani Kasarani:UCHAGUZI WA ODM WAKUMBWA NA VURUGU

UCHAGUZI wa Kitaifa wa ODM ulikumbwa na kisirani leo hii Ijumaa katika uwanja wa Kasarani ghasia zilipozuka muda mchache baada ya shughuli za kupiga kura kuanza na kupelekea shughuli hiyo kufutiliwa mbali.

Mgombea wa wadhifa wa katibu mkuu katika ODM Ababu Namwamba Februari 28, 2014. Picha/DENISH OCHIENG 

Vurugu hizo zilizopelekea masanduku ya kura kuvunjwavunjwa na kura zilizokuwa zimepigwa kutawanywa sakafuni, zilianza pale Mbunge Maalum Bw Isaac Mwaura aliposimama juu ya meza na kulalamika kwamba jina lake halikuwepo kwenye karatasi ya uchaguzi.

Bw Mwaura, ambaye alikuwa anawania kiti cha naibu wa katibu mkuu, alisema jina lake lililokuwa liwe la sita katika karatasi hiyo liliondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na lile la Peter Ole Musei.

Alidai kwamba kulikuwa na njama ya kumuondoa katika kinyang’anyiro hicho na kuongeza kuwa alilazimika kusimama juu ya meza baada ya malalamishi yake kwa wasimamizi wa uchaguzi huo kupuuzwa.

“Nilienda mpaka kwa wanachama wa bodi ya uchaguzi na kuwaelezea kuhusu hitilafu hiyo lakini hakuna mtu aliyenisikiliza. Ndio maana nikasimama juu ya meza. Wajumbe wengi waliniunga mkono na kusimama nami,” alisema Bw Mwaura akiongeza kwamba tukio hilo halikuwa limepangwa.

Mbunge huyo kijana alisema kuwa aliwasilisha malalamishi yake hadi kwa kinara wa chama Bw Raila Odinga.

Hali ya mguu niponye ilishuhudiwa huku wajumbe wakitumia chochote walichokuwa nacho ili kujikinga na viti na vitu vingine vilivyorushwa hewani.

Maafisa wa GSU walilazimika kuingia ndani ya ukumbi wakiwa wamejihami tayari kutuliza vurumai hiyo.

Maafisa wakuu wa ODM walionekana wakijaribu kumtuliza Bw Maura ambaye alikuwa amejawa na hasira. Aidha kulikuwa na madai kwamba orodha mpya ya wajumbe ilisambazwa ili kuwapendelea baadhi ya wawaniaji.

Njama

Wajumbe waliohojiwa baada ya ghasia hizo walisema kwamba wanataka uchaguzi huo ufanywe kwa njia huru na wazi huku wakidai kwamba kulikuwa na njama ya kuwapendekeza viongozi fulani kwa lazima.

Awali mbunge wa Dagoreti Kaskazini, Bw Simba Arati  alizomewa alipoingia ukumbini hata akashindwa kuhutubu. Bw Arati alikuwa mpinzani wa kinara wa chama hicho, Bw Odinga katika wadhifa wa kiongozi wa chama.

Kufikia wakati wa kwenda mitamboni, wajumbe wote walikuwa wamefurushwa kutoka uwanjani humo na haikuwa imebainika kama kikao cha leo kitaendelea.

Uwanja huo wa Kasarani ulipata jina la 'Kisirani’ (mahali ambapo mambo huenda kombo) mnamo 2002, pale Rais wa wakati huo Daniel arap Moi, alipowatenga hadharani Katibu Mkuu wa chama cha Kanu, Joseph Kamotho na kumpendelea aliyekuwa kiongozi wa National Democratic Party (NDP), Raila Odinga.

Mwezi Oktoba mwaka huo, Bw Moi alisimama hadharani kwenye mkutano mwingine wa wajumbe katika uwanja huo wa Kasarani, na kumchagua Uhuru Kenyatta kuwa mrithi wake, badala ya aliyekuwa makamu wake, marehemu Prof George Saitoti.

Swahili Hub
Mchimba Riziki

Facebook, Instagram na WhatsApp Kusitisha Huduma Zao Uganda






Makampuni makubwa tatu ya mitandao ya kijamii maarufu kama Facebook,Instagram na WhatsApp zimetishia kwamba zinaweza kusitisha huduma zao nchini Uganda,Hayo yalisemwa mnamo tarehe 25 mwezi wa pili mwaka huu 2014.

Hayo yalikuja baada ya rais wa Uganda Mheshimiwa Yuheri Kaguta Museveni kusaini mswada uliowasilishwa kwake na bunge na kuifanya kuwa sheria ya kupingana na vitendo vya kishoga.

Mataifa makubwa yenye uwezo kiuchumi yameitishia Uganda kutowapa misaada kwa sababu ya kuruhusu sheria hiyo mpya ya kukataa ushoga, Marekani ndio iko mstari wa mbele kuikandamiza Uganda isipitishe sheria hiyo lakini Rais Museven alikaidi amri hiyo.


Hii ni mojawapo ya malalamiko kutoka kwa wamiliki wa mitandao hayo:
STATEMENT FROM FACEBOOK ON ANTI-HOMOSEXUALITY LAW
When we launched Facebook, we thought it as a platform to advance people’s rights and liberties of self expression in all form. We were equally shocked to learn that Uganda as a country had gone ahead to sign the Anti Homosexuality bill into a law.
Facebook is currently reviewing its engagement to Uganda, as we seek to come up with a voice to express our dissatisfaction. And of course, suspending our operations in Uganda is one of the options we are considering. In the event that we suspend operations in Uganda, our platforms of Instagram, Facebook and Whatsapp will be off for a time we shall deem necessary.
We strongly condemn the act of the Ugandan Government to overstep the rights of a minority. All humans are created equal and deserve a right to freedom and happiness.
Signed
Sheryl Kara Sandberg 
Chief Operations Officer (COO) At Facebook




mchimba riziki

Sunday, February 23, 2014

JE,UMESKIA JUU YA KANUNI NNE ZA KIROHO?

Kila jambo maishani lina kanuni zake. Kadhalika maisha ya kiroho yana kanuni zake za jinsi ya kushirikiana na Mungu.


1. MWENYEZI MUNGU ANAKUPENDA, NAYE ANATAKA KUKUPANGIA MPANGO WA AJABU KWA MAISHA YAKO.

UPENDO WA MUNGU 
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16

MPANGO WA MUNGU KWAKO
Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Yohana 10:10

Je, kwa nini watu wengi hawana uzima huo?
Ni kwa sababu . . .

2. MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI. Dhambi zake zimemtenga na Mungu.Kwa hiyo hajui upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yake.

MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI
Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.Warumi 3:23

Mungu alimwumba mwanadamu kwa kusudi la kushirikiana naye, lakini mwanadamu alikwenda kinyume cha mpango wa Mungu. Alichagua kumwasi Mungu badala ya kumtii. Kumwasi Mungu ni kufanya dhambi. Mtu anapoishi kinyume cha mapenzi ya Mungu anaendelea kuishi maisha ya dhambi.

MWANADAMU AMETENGANA NA MUNGU
Lakini maovu yenu yamewatenga ninyi na Mungu wenu. Isaya 59:2

Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi. Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa nija nyingi: dini, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi.

Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu . .

3. YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI. Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu.

ALIKUFA ILI ATULETE KWA MUNGU
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu.1 Petro 3:18

YESU YU HAI
Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alitufuka siku ya tatu, kama yanenavyojil maandiko.1 Wakorintho 15:3,4

YESU NDIYE NJIA YA PEKEE
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.Yohana 14:6

Mwanadamu peke yake hawezi kushirikiana na Mungu. Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu.

Sasa kanuni ya nne itakuambia jinsi uwezavyo kumjua maishani mwako . . .

4. INAKUPASA KUMPOKEA YESU AWE MWOKOZI NA MTAWALA WAKO. Ndipo utajua upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yako.

UNAMPOKEA KRISTO KWA IMANI
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.Yohana 1:12

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.Waefeso 2:8,9

INAKUPASA KUMKARIBISHA YESU, MAISHANI MWAKO:
Tazama, nasimama milangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake . . .

Kumpokea Yesu Kristo ni:


  1. Kujua wewe ni mwenye dhambi na kugeuka nafsi yako kwa Mungu na kutubu.
  2. Kumtegemea Mungu kwa kukusamehe kabisa.
  3. Kumkaribisha Yesu Kristo atawale maisha yako kwa imani, ili uwe kama anavyopenda.


Je, ni picha gani aliye mfano wa maisha yako?
Je, ni picha gani ambaye ungependa awe mfano wa maisha yako?

Yafuatayo ni maelezo ya jinsi uwezavyo kumpokea Kristo ndani ya maisha yako?

UNAWEZA KUMPOKEA KRISTO SASA
Mungu anaufahamu moyo wako. Yafuatayo katika sala hii yanaweza kukusaidia kumpokea Kristo ukiomba kwa moyo wa kweli.
Bwana Yesu Kristo, ninakuhitaji, mimi ni mwenye dhambi. Nimekubali kwamba nimejitawala maisha yangu mwenyewe, na kutengana nawe. Asante kwa kifo chako msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na kwa kunisamehe zote. Sasa nageuka na kutubu. Bwana, nakuomba uingie ndani ya maisha yangu na kunitawala kabisa. Badili maisha yangu yawe kama upendavyo wewe. Amin.
Je, sala hii ni sawa na haja ya moyo wako?

Kama sala hii ni sawa na haja ya moyo wako, basi omba sasa na umkaribishe Kristo aingie maishani mwako.

YESU YUMO MAISHANI MWAKO
Sasa, je, umemkaribisha Yesu maishani mwako? Unajuaje?
Kwa hiyo yuko wapi sasa? Kumbuka Ufunuo 3:20.
Yesu alisema ataingia katika maisha yako. Je, si kweli?
Je, unajuaje kuwa Mungu amesikia ombi lako? Mungu ameahidi kwanba lo lote tuombalo na kuamini litatendeka.

ALIYE NA YESU, ANAO UZIMA WA MILELE:
Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele na uzima huu umo katika Mwana. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu. 1 Yohana 5:11-13

Umshukuru Mungu kila siku kwamba Yesu anaishi katika maisha yako.
Uwe na hakika kwamba hatakuacha kabisa. (Mathayo 28:20). Amekupa uzima wa milele.

USIYATEGEMEE MAWAZO YA MOYO WAKO.
Unaweza kujisikia leo unalfuraha kisha kesho ukawa na huzuni. Kwa vyovyote utakavyojisikia Yesu Kristo habadiliki maishani mwako. Waebrania 13:8.


  • Ukweli wa Mungu ndio wenye uwezo wa kutuongoza.
  • Tunaunganishwa na uwezo wa ukweli kwa imani.
  • Tunapotii ukweli, hali ya kujisikia ya moyo (maoni) huongozwa vyema.
  • Tunamtegea Mungu na ukweli wake wala sio hali ya kujisikia ya moyo.

Tukifanya dhambi tunatubu na yeye anatusamehe.

Basi, usitegemee mawazo yako, bali utegemee ukweli wa Neno la Mungu kwa imani.

KWA KUWA SASA UMEMPOKEA YESU
Tangu ulipompokea Kristo mabadiliko mengi yametokea.


  1. Yesu ameingia katika maisha yako. (Ufunuo 3:20)
  2. Umesamehewa dhambi zako. (Wakolosai 1:14)
  3. Umefanyika kuwa mwana wa Mungu. (Yohana 1:12)
  4. Utazidi kujua makusudi ya Mungu kwa maisha yako. (2 Wakorintho 5:14,15,17)

Je, unafikiri kuna jambo lililo bora kuliko kumpokea Yesu katika maisha yako?

Basi, labda ungependa kumshukuru Mungu sasa kwa vile alivyokurehemu.
Tunathibitisha imani yetu tunapomshukuru Mungu kwa maombi.

Tuombe tukiwa huru.

Na sasa je?

JINSI YA KUKUA KIROHO
Kama mtoto mchanga unahitaji kukua
Utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho ukiyafuata mashauri yafuatayo kila siku:


  1. Zungumza na Mungu kwa maombi (Yohana 15:7)
  2. Soma Neno la Mungu (Matendo 17:11)
  3. Uwe mwaminifu kwa Mungu (Yohana 14:21)
  4. Mshuhudie Kristo kwa matendo yako na maneno yako (Mathayo 4:19 na Yohana 15:8)
  5. Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1 Petro 5:7)
  6. Umruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-18 na Matendo 1:8)




Biblia inatuambia kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25)

Ebu, tutumie mfano wa moto. Kuni nyingi zikirundikwa pamoja zinawaka vizuri sana, lakini ukiuondoa ukuni mmoja na kuuweka peke yake utapoa. Vile vile wewe haifai kuishi maisha ya kikristo peke yako.

Ukishirikiana na watu wengine ambao wamempokea Yesu kuwa Mwokozi wao utazidi kuwa na moto wa imani.

Uhudhurie kanisa ambapo watu wanaiamini Biblia kuwa ni kweli na Yesu anatukuzwa.

Mchimba Riziki


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score