Thursday, March 13, 2014

Klabu Nyingi Za Bara La Afrika Zinatumia Uchawi Katika Soka..... Je unaamini Katika Nchi Yetu Kuna Timu Kubwa Inayotumia? Fuatilia Hapa ujue ni Timu gani.........

Klabu nyingi za Afrika zinatumia uchawi ili kung'ara katika Ligi ya Mabingwa Afrika, CAF Champions League, baadhi ya wanasoka maarufu barani humu wamesema.
Yanga Ya Tanzania
Uchawi umezungumziwa sana katika mijadala kuhusu soka ya bara na ingawa ilikuwa imepungua, kuna dalili kuwa matumizi ya ndumba unarejea katika mashindano makubwa.

Klabu maarufu ambazo zimefana katika ligi hii zimedaiwa kushiriki shughuli hiyo hata katika ligi za nyumbani.
Tukio la kwanza lilihusu klabu ya Morocco Raja Casablanca iliyocheza dhidi ya Horoya kutoka Guinea ambapo kipa wao alinaswa akipanga vifaa visivyojulikana katika lango lake.

Hata hivyo, Horoya ilishinda mechi hiyo 5-0 kwa njia ya penalti na kuondoa timu hiyo iliyoshiriki Kombe la Klabu Bingwa Duniani.

Katika hatua hiyo, kipa wa Yanga Deo Munish alionekana akifunga goli lake kwa uzi katika mechi dhidi ya Al Ahly jijini Alexandria, Misri lakini wenyeji wakaitoa.
SHUHUDA
“Niliona kipa wa Yanga akifanya vituko kabla ya mechi kuanza. Nilikuwa na jeraha na ilibidi nitizame mechi kwa nyumba na mara hiyo nilimpigia simu maafisa wa benchi la kiufundi kuwajulisha nilichoona. Mwanasoka mwenzangu alienda kwenye lango na kuuondoa uzi huo na hatimaye tulishinda mechi,” Walid Soliman aliambia supersport.com.

Kiungo wa Al Ahly Hossam Ashour amesema kuwa anaamini nguvu za uchawi katika ufanisi wa soka.
“Ndio nina imani na matumizi ya vitu hivyo na hatukufunga dhidi ya Yanga kwa kuwa tulikuwa na wasiwasi.”

Mchimba Riziki

Wednesday, March 12, 2014

Buyern Munchin Kulimwa Zaidi Ya £50,000 Baada Ya Kuonyesha Bango Linalosomeka Kuwa Ozill Ni Shoga..

Bayern Munich huenda ikaadhibiwa vikali na Shirikisho la Soka Ulaya, Uefa baada ya mashabiki kuanika bango lililodai kuwa Mesut Ozil wa Arsenal ni shoga.


Hili ndilo bango waliloweka mashabiki wa Munchin Wakimtukana Ozill Picha kwa msaada wa 
Kalbu hiyo ya Ujerumani huenda ikakumbana na rungu la Uefa kwa kupigwa faini itakayofikia Euro 50,000 baada ya mashabiki wake kuonyesha bango linalomtusi kiungo huyo wa Arsenal..

Bango hilo lililoanikwa katika uwanja wa Allianz Arena katika mechi ya kufuzu robo fainali ya Uefa lilikuwa na maandishi 'Gay Gunners’ na mchoro wa kiungo wa Arsenal, Ozil kando yake akiwa ameinama.



Licha ya kupewa kipaumbele na kocha wake katika kikosi cha Ujerumani, viwango vya soka vya Ozil vimetiwa shauku na mashabiki na vyombo vya habari nyumbani tangu alipohamia Emirates kutoka Real Madrid.


Mnamo Disemba, Uefa ilipiga Celtic faini ya Sh6 milioni baada ya bango lililokuwa na maandishi tata kuanikwa uwanjani Celtic Park katika mechi dhidi ya AC Milan.

Atambelea Mochwari Kila Wiki Kisa Mkewe.................Soma hapa Ndani Kwa Habari Zaidi

MWANAMUME kutoka Kinango, Kwale ambaye amekatazwa na wakwe zake kumzika mkewe aliyefariki zaidi ya miaka miwili iliyopita sasa anasema amelazimika kumtembelea mochari kila wiki ili kuepuka kusumbuliwa usiku akilala.
Bw Eric Mwatela wakati wa mahojiano na wanahabari mtaa wa Jomvu, Mombasa Machi 11, 2014.


Bw Erick Guni Mwatela, mwenye umri wa miaka 28, ana kibarua cha kuzuru chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya Pwani, Mombasa ili kuona mwili wa mkewe ambaye anasema si mwili tena kutokana na muda mrefu ambao umekuwa hapo.

“Ninalazimika kwenda katika chumba hicho kwa sababu nikikosa mke wangu marehemu Francisca Wawuda hunifuata nikilala na kutaka kujua ni kwa nini nimemuacha,” akaambia Taifa Leo hapo jana.

Bi Wawuda alifariki mnamo Februari 2012 akijifungua na sasa Bw Mwatela amebaki na mwanawe wa kike aliyezaliwa siku ya kifo hicho.

Alisema alikutana na mkewe akifanya kazi katika kiwanda cha EPZ eneo la Mazeras, wakachumbiana kisha wakaoana.

“Mke wangu aliniambia yeye ni yatima. Nyanya yake pia alisisitiza hilo na dada yake mkubwa pia akasema wao yatima. Lakini niligundua ana baba nilipoenda mochari kuchukua mwili wake ili kuuzika kuzika. Watu ambao sikuwajua walijitokeza na kusema sisi ni wezi wa maiti,” akasema.

Akaongeza: “Kulizuka kizaazaa kikubwa na hata tukaenda kortini. Kinachosikitisha ni kwamba tunapozozana, mwili wa mke wangu unaendelea kuoza na gaharama ya mochari inapanda kila siku.”
Gharama ya kuhifadhi maiti hiyo sasa imefika Sh350,000.
Jadis Munga ambaye ndiye baba ya marehemu Wawuda, anasisitiza ndiye anayestahili kumzika bintiye akisema Mwatela hakulipa mahari mkewe alipokuwa hai.

Alishinda kesi kortini akini alipoenda kuchukua mwili kuuzika akapata barua ya kumzuia kuuchukua.

“Nakumbuka nyanya ya marehemu akimuuliza baba yake sababu yake kuninyima mwili ilhali yeye pia hakulipa mahari. Sijui ni kwa nini anafanya hivyo. Naomba kusaidiwa,” akasema Mwateka na kuongeza kwamba alilazimika kuziba kaburi alilokuwa amechimba kumzika mkewe.

Alisema alilipa Sh5,000 za 'kifungua mlango’ kwa nyanya ya marehemu ndipo akawapa idhini ya kuishi kama mume na mke.

Mahakama maalum

Mnamo 2011, mkewe alipata mimba lakini akapata matatizo wakati wa kujifungua. Alilazwa katika hospitali ya wilaya ya Port Reitz mjini Mombasa na baadaye akahamishwa hadi hospitali kuu ya Pwani ambako alifariki Februari 27, 2012.

Bw Mwatela anaomba serikali imsaidie kulipa deni la mochari na kuingilia kati suala hilo ili mkewe azikwe.

Anasema Kenya inafaa kuwa na korti maalumu ya kushughulikia kesi za kimila, ada na desturi za jamii za humu nchini.

“Kuna kitu ambacho kinafichwa. Ni kwa nini baba mkwe anasisitiza anataka mwili wa mke wangu ilhali aliwatoroka? Ama ni mwanachama wa chama kimoja cha jamiiya Wachonyi chenye desturi mbaya inayoitwa wahula watu?” akauliza.

Bw Munga anasema kulingana na mila ya jamii ya Wachonyi, mwanamke ambaye hajajulisha wazazi wake kwa mchumba ama mume wake huwa hajaolewa. Kwa hivyo mume hana idhini ya kumzika hadi pale atakapotimiza mila hiyo.

Hata hivyo anasisitiza kuwa hataki hata ndururu ya Bw Mwatela kwa kuwa kimila bintiye hakuwa ameolewa.

Mchimba Riziki

Monday, March 10, 2014

Mishahara Yapunguzwa Kwa Wafanyakazi Wa Umma Kenya

Rais Uhuru Kenyatta ameagiza mishahara ya wakuu wa mashirika ya serikali ipunguzwe kwa asilimia 20 na kuonya kuwa watakaokaidi agizo hilo watatimuliwa.
Rais Uhuru na Makamu Wake Ruto Wakijadili jambo 


RAIS Uhuru Kenyatta Jumatatu aliagiza mishahara ya wakuu wa mashirika ya serikali ipunguzwe kwa asilimia 20 na kuonya kuwa watakaokaidi agizo hilo watatimuliwa.
Rais Kenyatta alisema wakuu wa mashirika ya umma wanafaa kufuata nyayo za maafisa wa ngazi za juu serikalini kwa kukubali mishahara yao ipunguzwe kwa hiari.

“Maafisa ambao hawataridhishwa na agizo hilo waende mahakamani, ikiwa mahakama itaamua kuwa wafidiwe tutawalipa na kazi zao tupatie watu wengine. Kuna Wakenya wengi ambao wanataka kazi hizo,” akaonya Rais Kenyatta.

Rais Kenyatta alisema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa kongamano lililoandaliwa na Tume ya Mishahara (SRC) kujadili jinsi ya kupunguza kiasi kikubwa cha fedha zinazotumika kulipa watumishi wa umma, chini ya kauli mbiu: 'Mshahara wako mzigo Wangu’  katika jumba la KICC, Nairobi

Tangazo hilo linafuatia siku chache baada ya rais na naibu wake Bw William Ruto, mawaziri na makatibu wa wizara kutangaza kupunguzwa kwa mishahara yao kwa asilimia 20.
Tayari baadhi ya viongozi  wamekubali kukatwa mishahara yao huku wa hivi karibuni akiwa mwenyekiti wa Tume ya Mishahara (SRC) Bi Sarah Serem, ambaye jana alisema kuwa marupurupu yake yapunguzwe kwa asilimia 10.
Rais Kenyatta alidokeza kuwa tayari zoezi la kuleta mageuzi katika mashirika ya serikali limeanza ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi wazembe wanatimuliwa.
Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka huu wa fedha wa 2013/2014, asilimia 56 ya bajeti ilitumiwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wa umma na matumizi mengine ya afisini.
Hiyo inamaanisha kuwa ni asilimia 44 ya fedha ambazo zilitumika kuendeleza miradi ya maendeleo.
Asilimia saba
“Asilimia 13 ya mapato ya nchi ilitumika kuwalipa mishahara watuishi wa serikali tofauti na kiwango cha kimatifa cha asilimia saba. Serikali haiwezi kutumia kiasi hicho kikubwa cha fedha kulipa watumishi wa umma mishahara badala ya kuendeleza miradi ya maendeleo,” akasema huku akiongeza kuwa serikali itasawazisha upya mishahara ya watumishi wa umma baada ya kubainika kuwa wafanyakazi wenye ujuzi sawa wanalipwa mishahara tofauti.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na Kituo cha Kutafiti masula ya Sera (KIPPRA),  mawaziri ni miongoni mwa watumishi wa umma wanaolipwa mishahara minono zaidi isiyopungua Ksh 737,332 huku mtumishi wa serikali anayepata mishahara ya chini zaidi akipokea mshahara wa Sh 7,701.
Rais alipuuza mapendekezo ya kutaka kuongezwa kwa ushuru kuimarisha mapato ya nchi huku akisema kuwa hatua hiyo itakuwa hatari katika ukuaji wa uchumi.
“Pendekezo la kutaka tuongeze ushuru halifai kwani tutakuwa tunawafukuza wawekezaji ambao ni muhimu katika ustawi wa uchumi,” akasema.
Maafisa wa ngazi za juu serikalini wanapata marupurupu 16 ya aina mbalimbali jambo ambalo tume ya SRC inasema kuwa ni uharibifu wa fedha za umma.

Mchimba Riziki

Sheria Yaanza Kufanya Kazi Uganda Wawili Watupwa Gerezani kwa Kosa La......................

Wanawake wawili, mshtakiwa na mlalamishi, waliofika mahakamani wakiwa wamevalia minisketi walifungwa gerezani baada ya jaji kusema mavazi yao yalitatiza mahakama.

Wanawake wakiwa wamevalia minisketi.
Kampala, Uganda

WANAWAKE wawili waliofika mahakamani wakiwa wamevalia minisketi walifungwa gerezani baada ya jaji kusema mavazi yao yalitatiza mahakama.
Bi Prosy Nasuna alikuwa amemshtaki mwanamke mwingine kuhusu deni la Sh103,182.
Stakabadhi za mahakama zinaonyesha Bi Nasuna alimpeleka Bi Jane Nabukenya mahakamani kwa kwenda kinyume na makubaliano yao alipokosa kumlipa deni lake.

Hata hivyo, alipoenda Bukomansimbi kusikiza kesi yake wiki jana, yeye pamoja na mshtakiwa walijikuta wakiishia gerezani.
Awali, kulikuwepo manung’uniko na kelele wakati watu waliposema mavazi yao yalipigwa marufuku kwenye sheria ya kukabiliana na ponografia iliyopitishwa hivi majuzi.
Sheria hiyo inasema ponografia inahusu mbinu yoyote ya kuonyesha sehemu nyeti za binadamu hasa kwa minajili ya kunyegeza.
Hali hii ilimpelekea Hakimu Mkuu Catherine Baguma kuagiza wakamatwe kwa kutoheshimu mahakama.
Alisema mahakama haingeweza kuendelea na kesi hiyo ikiwa wawili hao walikuwa wamevaa minisketi.
Bi Baguma aliwahukumu wawili hao kifungo cha masaa matatu gerezani na kuahirisha kesi yao hadi Machi 13.
Mnamo Desemba mwaka jana, bunge la Uganda lilipitisha sheria ya kuharamisha minisketi ambayo inalenga kuweka wazi kosa la ponografia kwenye sheria za nchi hiyo.
Huku baadhi ya wabunge wakidai mswada huo ulikiuka haki za kibinadamu, wengi waliunga mkono Serikali na kuupitisha.
“Kwa kuidhinishwa kwa mswada huu, ndoto yangu imetimia,” Kasisi Simon Lokodo, aliye Waziri wa maadili alisema.
Hata hivyo, baadhi ya wabunge walilalamika kuwa maelezo ya mswada huo kuhusu ponografia ni pana mno na yanakiuka tamaduni za Uganda za kudumisha tofauti zilizopo katika jamii.
Mwenyekiti wa kamati ya sheria na masuala ya bunge Steven Tashoboya, ambaye kamati yake ilipigia debe mswada huo, alisema ponografia huongeza ubakaji wa watoto na wanawake.
Mashoga
Sheria hiyo inasema ponografia ni tendo lolote la kitamaduni, tabia au mawasiliano kwa njia ya mazungumzo au maandishi kikamilifu au sehemu yake, au taarifa ya habari, au burudani, au onyesho la sanaa, au picha, au video, au muziki, au densi.

Imepiga marufuku pia mchanganyiko wa hayo yote unaoonyesha sehemu za mwili wa binadamu kama vile matiti, mapaja, makalio, na sehemu za uzazi zikiwa uchi au bila mavazi ya kutosha, mbali na kuonyesha watu wakijamiiana, au kuonyesha tabia zinazolenga kunyegeza, na mienendo mingine yoyote inayolenga kuozesha maadili.

Sheria hiyo imeanza kutekelezwa siku chache baada ya Rais Yoweri Museveni kutia saini sheria inayopiga marufuku uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa jinsia moja.


Sunday, March 9, 2014

Cheki Arsenal Walivyowanyoa Everton bila Maji Kombe la FA


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score