Saturday, March 9, 2013

HATIMAE RAIS WA NNE APATIKANA NCHINI KENYA


HABARI ZA KUAMINIKA NI KWAMBA LEO RAIS WAKENYA ATATANGAZWA RASMI..
NAE NI UHURU MOIGAE WA KENYATTA.
Kwa matokeo yaliyo tolewa na Tume ya IEBC sinaonyesha ya kwamba mgombea uris kwa mrengo wa Jubelee ameweza kufikisha idadi ya kura sinazotakiwa kikatiba..Bwana uhuru amefikisha kura 6,173,433 ambayo ni sawa na asilimia {50.03}ya kura yote ilopigwa mnamo march 4 2013.Jumla ya kura iliyopigwa ni kura 12,338,667.

Nae waziri mkuu wa kenya ambae alikuwa akigombea kiti hicho cha urais kwa awamu ya tatu sasa kupitia mrengo wa Cord aliweza kujizolea kura 5,340,667 kati ya kura 12,338,667 zilizopigwa na wakenya.Bwana Raila jana aliwaalika waandishi wa habari katika kambi iliyoko mjini Nairibi mtaa wa Karen lakini akaamua kuahirisha mkutano huo mpaka leo 09/03/2013..Kwa hiyo tunatarajia leo hii kuskia bwana Raila Odinga akihutubia waandishi wa habari.




 
IEBC leo itamtangaza rais wa jamhuri ya Kenya ailiye pita kikatiba saa 11am.Wakenya wengi walianza kusherehekea ushindi huo kuanzia mida ya saa kumi usiku katika mitaa tofauti katika jiji la Nairobi.Mavuvu zela yalipulizwa sana shwange na nderemo za kila aina zilikuwa katika mtaa huu wa Eastlegh wenye wafuasi wengi wa Jubelee coarlition.

Friday, March 8, 2013

IEBC YAENDELEA KUTOA MATOKEO YA URAIS KENYA

Ni mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Kenya bwana Aissack Hassan katika harakati za kutangaza matokeo ya mshinani.
.
Leo hii kuanzia nyakati za jioni Tume hiyo itatangaza matokeo ya Urais inayosubariwa kwa hamu na mamilioni ya Wakenya na hata nje ya Kenya.katika kura zilizokwisha kutangazwa inaonekana kwamba Bwana Uhuru Kenyatta naongoza kwa kuwa na kura 5,159,344 huku akifuatiliwa na aliekuwa waziri mkuu wa Kenya bwana Raila Odinga mwenye kura 4,516,660 akifuatiwa nae Mudavadi alikwisha kukiri kushindwa katika uchaguzi huo.

 Pia siku ya jana viongozi wa mrengo wa Cord walisema lazima waende kortini kwa sababu ya kutorithika na matokeo yanayoendelea kutangazwa na tume hiyo ya IEBC.Walisema kwamba matokeo hayo yaliorudiwa kuhesabiwa yalikuwa na maneno ndani.

Endelea kufuatilia blog yetu kwa kila hatua tunayo piga kwa updates moto moto kutoka hapa nchini Kenya. 

MUDAVADI AKIRI KUSHIDWA KATIKA UCHAGUZI

Musali Muadavadi ambae alikuwa anawania urais kupitia mrengo wa AMANI.
Leo hii ametokeza mbele ya vyombo vya habari na na kutangaza kushindwa katika uchaguzi uliofanyika March 4.

Akionge mbele ya waandishi Musalia amabae alikuwa ni waziri mkuu mzaidizi katika serikali ya pamoja,amesema amekubali kwamba ameshindwa na kuwahimiza wakenya kuishi kwa amani..
Muasali aliewahi kuwa mwanachama wa ODM na mwishoni mwa mwaka jana aliamua kujitoa katika chama hicho kinacho ongozwa na waziri mkuu kwa kudai kwamba hakuna demokrasia chamani hapo.

Pia katika kuhamia chama cha UDF ambacho alikuwa mgombea urais kupitia chama hicho aliwahi kujiunga na mrengo wa JUBELEE mwanzoni mwa mwaka huu na kujiondoa baada ya kuona kwamba Uhuru na Ruto hawataki kumuachia mtu mwingine aiongoze mrengo huo wa Jubilee.

Bwana Mudavadi  ameahidi wakenya kwamba atashirikiana na Rais atakae shinda katika uchaguzi huu katika ujenzi wa taifa laKenya.Amesema pia Mrengo alioongoza yeye pamija na Eugin wa Malwa utaiheshimu serikali itakayo ingia madarakani..

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score