Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts

Friday, December 5, 2014

2017 Haitafika Bila Taji "Arsen Wenger" Anena

Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ana imani anaweza kuongoza vijana wake kunyakua taji la ligi kuu kabla ya kandarasi yake kuisha mwishoni wa msimu wa 2016/17.

Arsen Wenger

Imani yake ya msimu huu ilipigwa jeki hata zaidi na ushindi wao mwembamba wa 1-0 dhidi ya Southampton Jumatano usiku na hivyo kuzidi kumpa moyo licha ya kuwa wangali katika nafasi ya sita kwa alama 23, ikiwa ni pointi 16 nyuma ya viongozi Chelsea.

Timu hiyo imeandikisha mwanzo wao mbaya zaidi katika ligi ya EPL tangu 1982 na wamejikuta nyuma mno kwa pengo hilo kubwa la alama ikilinganishwa na muhula uliopita ambapo hadi kufikia wakati huu walikuwa uongozini kabla ya kufifia kufikia mwisho wa kampeni na kunusurika kwa kumaliza wa nne.
“Kuna ushindani mkubwa Uingereza na Chelsea wameanza vyema, hilo tunakubali. Itakuwa vigumu kuwafikia lakini kila mmoja atapigania kuwalaza sisi pia tukiwemo. Huwezi kusema kuwa harakati za kuwania taji zimekwisha baada ya mechi 14 pekee tulizocheza hadi kufikia sasa,” Wenger akasema.
“Hatukuanza vyema msimu huu ila usisahau kwamba hatukuwa na kikosi chote pamoja tangu musimu kuanza kwani ulifuatia Kombe la Dunia. Ni lazima tupambane  ili kurudia uwaniaji wa taji kwa haraka katika kila mechi,” akajitetea.

Licha ya yote, Wenger anaonekana kuwa kakalia kuti kavu baada ya mashabiki kuanza kumshurutisha aondoke kama ilivyoshuhudiwa wikendi iliyopita kwenye ushindi wao wa 1-0 dhidi ya West Brom.

Wednesday, July 30, 2014

Hatimaye Mkenya Wa Pili Atua Ligi Kuu England.... Atashiriki Michuano Mikubwa Ya UEFA

Divork Origi Na Sakfu Ya Liverpool.

London: Hatimaye, klabu ya Liverpool imemsajili mshambuliaji wa chipukizi, Divock Origi Mkenya/Mbelgiji akitokea Klabu yake ya Lille aliyojiunga nayo akiwa na miaka 15.

Mchezaji huyo mwenye miaka 19 ameukubali mkataba wa miaka mitano lakini ataendelea kubaki kwenye klabu yake huko Ufaransa kwa mkopo katika msimu ujao kabla ya kuhamia Anfield mwaka ujao 2015.

“Ninayo furaha kwa klabu kubwa kama Liverpool imenisajili,” Origi alisema.
Origi alicheza mechi zote tano za Ubegiji katika fainali za Kombe la Dunia la mwaka huu wakati wakipigana kuelekea robo-fainali na kuifungia timu yake bao dhidi ya Urusi.
Mbali na Origi, Liverpool pia imewanunua Rickie Lambert, 32, akitokea Southamptom na kiungo wa wa kati Adam Lallana, 25,  kutoka Southampton.
Kadhalika imewanasa Emre Can, 20 akitokea Bayer Leverkusen na winga Lazar Markovic, 20, akitokea Benfica.
Mlinzi Dejan Lovren, 25 akitokea Southamptom pia amehamia Anfield.
“Najua hii ni klabu yenye historia kubwa, wachezaji wakubwa  na mashabiki wengi,” aliongeza.
“Kwangu Liverpoool ni moja ya vilabu bora kabisa duniani na ninayo furaha sana kuwa sehemu ya historia hii.
Origi ambaye asili yake ni Kenya alianzia katika klabu ya Genk alichochezea babake, Mike Okoth kabla ya kuhamia Lille.


TETESI ZA SOKA ULAYA

Beki was Aston Villa Ron Vlaar, 29, atakuwa
 na mazungumzo na meneja wake Paul Lambert kuhusiana na hatma yake licha ya Southampton kumwania (Daily Mirror), QPR wanafikiria kumchukua kiungo wa Colombia Carlos Sanchez, 28, kwa pauni milioni 4 kutoka Elche (Daily Mirror), West Ham na QPR wamepanda dau kwa Marseille kumchukua Matheiu Valbuena baada ya kiungo huyo Mfaransa kukataa kuhamia Dynamo Moscow (L'Equipe), Manchester United na Barcelona bado wanamfuatilia Juan Cuadrado, 26, wa Fiorentina lakini huenda wakatishwa na bei ya pauni milioni, 32, ya kiungo huyo kutoka Colombia (Marca), Manchester United wamefikia makubaliano "ya mdomo" na kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, ya uhamisho wa pauni milioni 47 (Tuttosport), matumaini ya Manchester City kumsajili beki kutoka Morocco Mehdi Benatia, 27, yamefifia baada ya Roma kusema hakuna dalili za mchezaji huyo kuondoka (Le Figaro), meneja mpya wa Manchester United amewaonya mashabiki wake kuwa timu hiyo huenda ikasuasua katika miezi mitatu ya mwanzo wa msimu wakati wachezaji wakianza kuzoea mbinu zake (Times), Van Gaal amesema iwapo watashinda Ligi Kuu msimu ujao na kuwapiku majirani zao Manchester City, utakuwa ushindi "mtamu" zaidi (Manchester Evening News), kiungo wa Manchester City Yaya Toure, 31, amesema huenda akasalia katika timu hiyo hadi atakapoacha kucheza soka (Guardian), mshambuliaji mpya wa Barcelona Luis Suarez, 27, ambaye anatumikia adhabu ya miezi minne, amehamia katika mji wa Pyrenees kuanza mazoezi ya msimu mpya akiwa na mwalimu binafsi (Daily Mail), Didier Drogba, 36, amesema Diego Costa, 25, atakuwa mchezaji "mkali" katika Ligi Kuu ya England (Sun), AC Milan wanafanya mazungumzo wa mshambuliaji kutoka Brazil Robinho, 30 (Le Figaro), kiungo wa Arsenal Santi Cazorla,29, bado anasakwa na Atlètico Madrid. Atlètico pia wanamfuatilia Fernando Torres, 30, na winga wa PSV Eindhoven Zakaria Bakkali, 18 (AS.com), kiungo anayefuatiliwa na Liverpool, Xeridan Shaqiri, 22, huenda akaamua kubakia na klabu yake ya Bayern Munich (Tuttosport), Borussia Dortmund na Schalke wanamtaka mshambuliaji kutoka Serbia, Aden Ljajic, 22, kutoka AS Roma (Bild), Barcelona wametangaza kumsajili kiungo kutoka Brazil, Alex Varoneze Dione anayejulikana kama "Betri" kwa miaka mitatu (Mundodeportivo), Manchester United wameanza tena kumfuatilia beki wa kati wa Atletico Madrid Miranda, baada ya Atlètico kusema wapo tayari kupokea dau la pauni milioni 23 (Metro), AC Milan wanamtaka winga wa Newcastle Hatem Ben Arfa na huenda akauzwa kwa pauni milioni 12 (Daily Star), Bayern Munich wapo tayari kusubiri hadi Oktoba kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona Victor Valdez ambaye anauguza jeraha la goti, ingawa anaweza kusita kwenda kugombea namba na Manuel Neuer (Mundo Deportivo), QPR wanataka kumchukua Ronaldinho ambaye amemaliza mkataba wake na Atletico Mineiro (Globoesporte) na Chelsea wanakataa kutengeneza jezi zenye jina la kipa Thibaut Courtois, 22 na Romelu Lukaku, 22, kwa sababu wachezaji hao bado hawajapewa namba (Daily Star).

Tuesday, July 22, 2014

Mourinho Anena Juu Ya Ujio Wa Van Gaal Manchester United. Amwambia............



Kushoto Ni Jose Mourinho akimtania Kocha Man U Van Gaal Kulia.
Kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, amejitanua kifua kwamba hamwogopi  mkufunzi mpya wa Manchester United, Louis Van Gaal wakati msimu mpya unapozidi kukaribia kuanza.
Wawili hao ambao ni marafiki wakubwa waliwahi kufanya kazi pamoja katika klabu ya Barcelona, Mourinho akiwa mkalimani na mwenzake kocha.

Makocha hawa wawili wana mafanikio makubwa kwenye taaluma yao ya ukufunzi  japo hawajawahi kujipata katika ushindani zaidi ya mwaka wa 2010 walipokutana kwenye fainali ya dimba la klabu bingwa Ulaya.
Wakati huo Mourinho alikuwa akiifunza Inter Milan ya Italia naye Van Gaal akinoa Bayern Munich ya Ujerumani. Timu hizo zilikutana kwenye fainali hizo na  Mourinho akaibuka kidedea kwa kutwaa ubingwa.
Mwaka huu, watagongana vichwa kwenye Ligi Kuu ya Uingereza ambapo Van Gaal ameapa kujaribu kushinda taji katika msimu wake wa kwanza akiwa uongozini huku naye mwenzake akisisitiza wazo sawa na hilo.
“Sina wasiwasi kwamba kwa sasa yupo hapa. Mwanzo ninatamani sana kukutana na United na wala sioni cha kunipa hofu. Hii ni kwa sababu sisi sote ni makocha wazuri na ninachojua ni kuwa ataisaidi Manchester United,” Mourinho alisema.
“Van Gaal kwa mtazamo wangu ndiye aliyekuwa kocha bora wa dimba la dunia na ni mtu ninayemheshimu sana kutokana na urafiki wetu mkubwa wa siku nyingi. Ila pamoja na yote, katika ushindani kila mmoja atajisimamia,” aliongeza.
Van Gaal alianza majukumu yake mapya klabuni humo juma lililopita na tayari ameapa kuirejesha United kwenye hadhi yake ya ushindani ligini baada ya kumaliza ya saba msimu uliopita chini ya ualimu wa David Moyes aliyepigwa kalamu.
Kwa sasa Van Gaal yuko na kikosi hicho jijini Miami, Marekani anakokitayarisha kwa mechi kadhaa za kirafiki. Kwa wakati huo huo anaendelea kufanya usajili ili kukirutubisha kikosi hicho hata zaidi.

Mkataba Wa Vana Gaal
Mkufunzi huyo alitia saini kandarasi ya miaka mitatu na United na mechi yake ya kwanza ya Ligi inayoanza Agosti 16, itakuwa dhidi ya Swansea siku mbili kabla ya Chelsea kuanza kampeni yao vile vile dhidi ya Burnley iliyopandishwa daraja.
Tetesi Za Usajili
Boss wa Manchester City Manuel Pellegrini anapanga kumchukua Didier Drogba, 36, ambaye pia anasakwa na klabu yake ya zamani Chelsea (Daily Star), meneja wa Manchester United Louis van Gaal anataka kutoa pauni milioni 17 kumchukua beki mkabaji wa Ajax Daley Blind, 24 (Daily Express), United pia wameripotiwa kuwa karibu kumsajili beki wa kati wa Borussia Dortmund Mats Hummels, 25, kwa pauni milioni 16 (Daily Mail), Tottenham wameambiwa watoe pauni milioni 25 kama wanamtaka kiungo wa Real Sociedad Antoine Griezmann, 23, ambaye pia anafuatiliwa na Chelsea na Monaco (Daily Telegraph), boss wa Arsenal, Arsene Wenger amesema hatosajili mshambuliaji msimu huu na hivyo kufuta tetesi zinazomhusisha na Mario Balotelli wa AC Milan (Daily Mirror), kiungo wa Ureno Thiago Mendes, 23, ametupilia mbali uwezekano wa kurejea Chelsea na angependa kusalia Atletico Madrid miaka miaka mingine miwili (Daily Express), PSG watakwepa sheria za Fifa za fedha kwa kumchukua Angel Di Maria, kwa mkopo kwa mwaka mmoja kutoka Real Madrid. Di Maria anasakwa pia na Man United (Daily Express), Arsenal, Chelsea na Man United wanamtaka beki Reece Oxford, 15, baada ya kinda huyo kuonesha kipaji msimu uliopita akiwa na West Ham ya vijana (Daily Star), Arsene Wenger atamruhusu Thomas Vermaelen kwenda Manchester United, ikiwa tu atarhusiwa kumchukua Phil Jones au Chris Smalling (Daily Mirror), Chelsea watampa Didier Drogba mkataba wa miezi 12 wa kucheza ambao hautakuwa na kipengele cha kuwa kocha, ingawa Chelsea wapo tayari kuzungumzia hilo (Daily Telegraph), mshambuliaji wa Lille Divock Origi anakwenda Boston Marekani kuungana na Liverpool ambao wapo katika ziara ya mechi za kabla ya msimu. Atafanyika vipimo kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 10. Huenda pia akarejeshwa Lille kwa mkopo (Daily Star).



Monday, July 21, 2014

Mkenya Aliyecheza World Cup Kutua Liverpool

Liverpool inakaribia kufikia maafikiano na klabu za Southampton kumnunua beki Dejan Lovren na klabu ya Lille ili kupata saini ya mshambuliaji Mkenya Divock Origi.
Divorck Origi

Kulinganana BBC, The Reds ambao kwa wakati huu wako ziarani nchini Marekani wameripotiwa kufikia makubaliano na Lille kumsajili Origi raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Kenya kwa dau la Sh1.5 bilioni. Kwa wiki kadhaa sasa Liverpool imekuwa ikimsaka mshambuliaji huyo huku kukichapishwa ripoti kadhaa za maafikiano baina ya pande zote ila taarifa hizo hazijawahi kuwa rasmi.
Kumhusu mlinzi Lovren mwenye umri wa miaka 25, Liverpool waliwasilisha ofa ya Sh3 bilioni juma lililopita ila ilikakataliwa. Hata hivyo Lovren raia wa Croatia ameelezea nia yake ya kutaka kuhamia Liverpool hatua ambayo imeanza kuwafanya Southampton kuwaza mara mbili.
Mlinzi huyo amewasilisha barua kwa klabu hiyo ya kuwataka wamruhusu aondoke ikiwa ni baada ya kutumikia mwaka mmoja wa mkataba wake wa miaka minne nao.
Liverpool ambao watashiriki Ligi ya mabingwa msimu ujao kwa mara ya kwanza tangu 2009, wamekuwa wakikirutubisha kikosi chao na hadi kufikia sasa baada ya kuondoka kwa nyota wao Luis Suarez aliyetua Barcelona, wamefanikiwa kuwasajili wachezaji sita.

Mshambuliaji Loic Remy alijiunga nao Jumapili baada ya klbu ya QPR kukubali ofa yao ya Sh1.2 bilioni. Kando na mchezaji huyo, kocha Berndan Rodger ameanunua Adam Lallan, Rickie Lambert, Lazar Markovic na Emre Can...

Kwa tetezi nyingi za soka usikose kujiunga nasi kila mara....

Nilijaribu Kutoa Mimba Ya Ronaldo "Maria Dolores Dos Santos Averiro" Ni Mama Wa Cristiano Aliyasema Hayo Katika Uzinduzi Wa Kitabu Cha Historia Yake.


LISBON, Ureno

Maria Dolores Dos Santos Averiro Mama Yake Ronaldo

Mama yake mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo, amefichua siri kwamba alijaribu kuavya/Kutoa mimba alipokuwa akitarajia kujifungua mwanasoka huyo miaka 29 iliyopita.

Katika kitabu chake kilichozindulia siku za hivi karibuni, Dolores Aveiro anaeleza kuwa daktari wake aliyekuwa akimshughulikia wakati wa ujauzito huo, aligoma kumsaidia katika jitihada zake za kutoa mimba.

Kuona hivyo, Dolores aliamua kuifanya mwenyewe nyumbani alipoanza tabia ya kunywa pombe yenye joto na kisha kushiriki mazoezi makali kupita kiasi akiwa na wazo kwamba hatua hiyo ingepelekea mimba ya Cristiano kucharuka


“Nilitaka kutoa mimba lakini daktari hakuniunga mkono kabisa. Hivyo nilianza kunywa pombe yenye uvuguvugu na kisha kukimbia mpaka pale nilipozirai ila jitihada zote hizo za kutoa ujauzito ule haukufua dafu,” Dolores anaeleza kwenye kitabu hicho cha wasifu wake.

Pamoja na yote mama huyo anakiri kwamba baadaye mwanawe alikuja kubaini ukweli wa mambo na badala ya kuwa na machungu naye, amekuwa akimfanyia utani tu kwa tendo lake hilo ambalo huenda lingemnyima nafasi ya kuwa mwanasoka maarufu zaidi Duniani jinsi alivyo sasa.

“Alipogundua nilichojaribu kufanya, alikuja na kunieleza haya, 'mama hebu tazama, ulitaka kuniavya ila sasa ni mimi ndiye ninayekimu familia nyumbani”. Ronaldo alimwambia mama yake

Mbali Na Hayo 


Kwa wakati huo straika wa zamani wa klabu ya Arsenal na taifa la Ufaransa, Thiery Henry ameibua mjadala ambao umekuwepo kwa siku nyingi wa ni nani mkali zaidi kati ya Lionel Messi na Cristiano.
Wachezaji wote hawa ambao wameshinda mataji ya wachezaji bora duniani Ballon d’Or, Messi anayeisakatia klabu ya Barcelona akiibeba mara nne naye Cristiano akitawazwa mara mbili, wamekuwa wakiwagawanya wadau wengi.
Kulingana na Henry, kando na mambo mengine uwanjani hasa ufungaji mabao, Cristiano hana talanta na kipaji cha kweli kinachoweza kulinganishwa na kile cha Messi.

Cristiano Ronaldo


Tuesday, July 15, 2014

Huku kombe La Dunia Likiwa Limefika tamati Basi Usikose siri Hii Aliyoambiwa Gotze Kabla ya Kuingia Kwenye Mechi Yao Ya Fainali. Ambapo Gotze Alikuwa Shujaa Wa Ujerumani.

Ujerumani Katika Picha Moja 
Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew ametoboa siri kwamba alimwambia shujaa wa fainali ya Kombe la Dunia 2014 Mario Gotze aidhihirishie dunia kuwa ni bora kuliko Lionel Messi. 


Goli moja la Gotze la dakika za nyongeza ndio lilipeleka kilio Argentina huku kombe hilo likitua Ujerumani.
Na baada ya sherehe za ubingwa wa  Dunia 2014, kocha wa Ujerumani, Joachim Loew alisema kuwa alimpa  nasaha moja Gotze kabla ya kumuingiza uwanjani akitokea benchi.  
Captain Wa Ujerumani Akishangilia kombe la Dunia
Law alimwambia mchezaji huyo kuwa aingie uwanjani na kuionyesha dunia kwamba ana kiwango kikubwa kuliko mshambuliaji huyo wa Argentina.  “Nilimwambia Gotze baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha muda wa zia


Timu Ya Ujerumani Ikipokelewa Nyumbani Ujerumani



da, 'dhihirisha kwamba wewe ni mchezaji bora kuliko Messi, onyesha kuwa una kiwango kumpiku yeye, kiwango ambacho kinaweza kushinda Kombe la Dunia,” Loew aliwaambia wanahabari baada ya mechi.
mashabiki Wa Ujerumani Wakiwashangilia Mashujaa Wao 
Baada ya kazi kuwa ngumu hadi dakika za mwisho  huku  mchezo ukionekana ungeamuliwa na penalti, wachezaji wawili ambao waliingizwa kama nguvu mpya ndio walioishia kuikomboa Ujerumani.
Andre Schurrle alipokea mpira wa pembeni mwa uwanja upande wa kushoto kutoka katikati na kutimka nao huku akiandamwa na mabeki wawili wa Argentina.
Lakini maarifa yake ya kuzalisha krosi ya haraka iliyowapenya katikati madifenda, yalimfikia vyema Gotze kwenye eneo la hatari. Naye hakusita kuutuliza kwa kifua kabla ya kupiga kiki kali lililojaa katika wavu wa kipa Romero Rodriguez huku ikiwa imesalia dakika tatu pekee kabla ya mchezo kwenda hatua ya penalti.
Gari Walilotumia Timu Ya Ujerumani Wakiwa Munich
Bao hilo lilitosha kuwapa Ujerumani taji hilo kwa mara ya nne, makombe ya awali wakishinda 1954, 1974  na 1990.
Huku Ujerumani wakisherehekea ufanisi wao, Messi ambaye alituzwa kuwa mchezaji bora wa dimba hilo amewalaumu mafowadi kwa kupoteza nafasi nyingi za wazi ambazo zingewapa ubingwa badala ya wapinzani wao.

Baadhi Ya Wachezaji Wa Ujerumani Wakishangilia 
“Hatukustahili tuliyoyapata na ukweli ni kuwa mastraika walipoteza nafasi za kufunga tulizopata. Hilo linauma sana sababu si jambo rahisi kupoteza pembamba namna ile,” Messi alisema.

Wednesday, July 9, 2014

Brazili Wanyolewa Bila Maji Wembe Uliotumika Ni Chuma Cha Ujerumani.

Brazili Imeondolewa Hapo jana Katika Mechi Ya Nusu Fainali Kwa Kichapo Cha Mbwa Wa Sokoni Pale Ilipokandamizwa Mabao 7:1.
Timu Hiyo Iliyoandaa Kombe La Dunia Kwa Mbwembwe Nyingi Iliweza Kubanduliwa Na Wajerumani Usiku Wa Jana.

Umakini wa vijana wa Joachim Low ulikuwa wa kupigiwa mfano walipoiadhibu Brazil na kuwa timu ya kwanza kuwahi kushindwa kwa mabao mengi zaidi katika hatua hiyo ya nusu fainali ya kombe la dunia.
Kabla ya mechi hiyo vyombo vya habari vilikuwa vimemulika mfumo wake Luiz Felipe Scolari vikidai alikuwa ameumba timu yake kumtegemea Neymar.
Kujeruhiwa kwa Neymar Ijumaa iliyopita ilimlazimu Scolari kubadili mfumo ambao sasa haukuwa na nyota huyo.

Hebu Fuatilia Linki Ifuaatayo Kuweza Kutazama Magoli Yalivyokuwa Yakiminika.
http://www.fifa.com/worldcup/videos/highlights/match=300186474/index.html

Friday, June 27, 2014

FIFA Yalishusha Rungu La Nguvu Kwa Suarez Luis.. Hata Cheza Tena Worldcup

Luis Suarez Alipomgata giorgio-chiellin

SHIRIKISHO la soka duniani, FIFA limempiga marufuku ya mechi tisa na pia marufuku ya miezi minne straika wa Uruguay, Luis Suarez kushiriki mechi yeyote ile kwa kosa la kumng’ata beki wa Italia Giorgio Chiellini.
Kamati huru ya nidhamu ya chombo hicho ilimpata mshambuliaji huyo anayesakata soka ya kulipwa katika klabu ya Liverpool na hatia hiyo kwenye kisa kilichotokea Jumanne kwenye mechi ya mwisho ya kundi D timu hizo zilipokutana. 

Hatua hiyo inamaanisha kuwa safari ya Suarez kwenye dimba la dunia limefikia ukingoni kwani atahitajika kuhudimia marufuku ya mechi tisa ya kimataifa.
Aidha adhabu hiyo itamfungia nje ya michuano tisa ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza  punde msimu mpya utakapoanza hapo Agosti 16, 2014.
Taifa la Uruguay nalo limepewa siku tatu kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo na mawakili wa Suarez tayari wameonyesha nia ya kufanya hivyo.
Mara ya mwisho kwa adhabu kama hii kutolewa kwenye kombe la dunia ilikuwa 1994, dhidi ya beki wa  Italia, Mauro Tassotti
Tassotti alipigwa marufuku ya mechi nane za kimataifa kwa kumpiga mwenzake kumbo nzito.
Luis Surez Alipomgata Ivanovic Wa Chelsea EPL


Akijifanya kaumia alipomgata mwenzake

Alipoanza Kujua Utamu Wa Kugata Huko Ajax

Friday, June 13, 2014

Cameroon Yagaragazwa na Mexico. Yachapwa Mbele Ya Umma..

Matokeo yalivyo
Kombe la Dunia limeendelea leo usiku wakati mechi moja imekamilika mda mchache uliopita.
Timu zilizokuwa kibaruani leo hii ni Mexico Vs Cameroon.Timu zote zimecheza kwa kukamiana sasa ambapo zilitoka sare kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha pili dakika ya 69 Mexico walipata bao la kuongoza. Timu zote zilicheza mchezo wa kusoma mda mrefu. Hadi kipindi cha pili ama dakika tisini yakiisha ni Mexico 1:0 Cameroon.

Kwa matokeo hayo basi yanaacha msimamo wa wa Kundi A iki hivi
1. Brazil Pointi Tatu Na Mabao Matatu
2. Mexico pointi tatu na bao moja
3. Cameroon hawana pointi wakidaiwa goli moja na 
4. Crotia ni ya nne ikiwa haina pointi yoyote ile ikidaiwa magoli mawili.

Msimamo Katika Kundi A
Mfumo wa Cameroon ulivyokuwa
Mfumo walioutumia Mexico
Zifuatazo Hapa Chini ni baadhi ya picha ya mtanange huo wa Mexico Vs Cameroon.
Kocha Wa Mexico
Alex Song Akipambana na Washambuliaji wa Mexico
Mashabiki wa Mexico
Wachezaji wa sub wa Mexico Wakishangiilia goli Hernands yumo
Mashabiki wa Mexico Wakiisapoti timu yao
Mabeki wa Cameroon Wakifanya kazi ya ziada
Alex Song Akipambana
Mshambuliaji wa Mexico akikaza msuli 
Mashabiki wa Cameroon nao wakishangilia timu yao
Mabeki Wa Cameroon Wakimzuia Mshambuliaji wa Mexico
Song Kazini
Mshambuliaji Giovan akilalamika 
Samuel Etoo Akipiga shuti
Marudio Ya Goli lililokataliwa na refa
Mshambuliaji wa Mexico akijaribu kumtoka beki wa cameroon

Saturday, May 24, 2014

Chelsea Kama Ndio Timu Ya Dunia Vile...


RIO DE JANEIRO: Chelsea inaongoza kwa kuwa na wachezaji wengi zaidi katika vikosi vya timu za taifa zitakazoshiriki fainali za Kombe la Dunia.
Mashabiki Wa Chelsea Darajani.
Timu hiyo ina wachezaji 18 na kuzipiku timu nyingine kubwa kama Manchester United na Bayern Munich.

Hata Napoli ya Italia ina wachezaji wengi kuzipiku timu za Barcelona na Real Madrid.
Man United na Bayern kila mmoja ina wachezaji 16 katika vikosi mbalimbali vinavyojiandaa kwa michuano hiyo.
Brazil ambao ndio wenyeji wa fainali hizo wameita kikosini wachezaji wanne wa Chelsea ambao ni Oscar, Willian, Ramires na Davdi Luiz.
Wachezaji wengine wa Chelsea ni Frank Lampard na Gary Cahill walio katika timu ya Uingereza.
Uhispania ina Fernandos Torres na Cesar Azpilicueta wakati Ubelgiji ikiwa na Eden Hazard, Romelu Lukaku na Thibaut Courtois.
Mstaa wengine wa Chelsea kwenye vikosi vya taifa ni Samuel Eto’o (Cameroon), Andre Schurrle (Ujerumani) na Wanigeria -John Obi Mikel, Victor Moses na Kenneth Omeuro.
Kadhalika kuna Mghana Christian Atsu na Patrick van Aanholt wa Uholanzi.
Timu nyingine zenye wachezaji wengi ni pamoja na Barcelona, Real Madrid, Manchester City (13), Juventus, Arsenal, Liverpool (12), Atletico Madrid (11), Porto, Inter Milan, AC Milan, Zenit (10) na Borussia Dortmund, Paris Saint- Germain (8).


Kikosi Kamili Cha Chelsea Brazili Ndio Hiki Hapa Chini.
 Andre Schurrle
Cahill
Cesar
Christian Atsu
Eden
Samuel Etoo
Mikel Obi
Kenneth Omeuro

Lampard
Luis

Lukaku

Victor Mosess

Oscar

Patric van


Ramires


Thibaut Courtois.


Toress

Willian








Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score