Saturday, May 31, 2014

Mapokezi Ya Railla Odinga Yalikuwa Ya Kutisha... Maelfu Wajitokeza Kumpokea kinara Wao

Na Mathayo Ngotee

Aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Mh.Raila Amollo Odinga aliwasili leo hii 31/05/2014 akitokea nchini Marekeni alipokuwa ziarani yapata miezi mitatu.
Wafuasi wa Railla Asubuhi ya leo

Mapokezi yalikuwa makubwa na yaliandaliwa na wanachama na wafuasi wa mrengo wa CORD, ukifanyika jijini Nairobi katika bustani za Uhuru park. Mkutano huo wa kumpoke Mh.Raila ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka pande zote Kenya.

Wakati akiongea na wananchi Mh. Railla aliyazungumzia mambo mengi yaliyotokea nchini Kenya

Hotuba Ya Mh.Railla Odinga 
Mh.Raila Odinga
"Niko na furaha kubwa sana kurudi nyumbani,kwani nilikuwa Marekani yapata miezi mitatu.Nilipata nafasi kuhutubia katika Vyuo vikuu mbalimbali pia vyuo vya ufundi tofauti tofauti nchini humo.

Nimewaleteeni salamu kutoka katika nchi ya Barack Obama mdogo na nimeifikisha katika nchi ya Barack Obama mkubwa.

Nawashukuru sana watu wote walioacha kazi zao na kuja kunikaribisha nyumbani, sita wahi kuisahau hii siku katika maisha yangu. Nawashuku Stephen Kalonzo,Mosess Wetengula,Anyang' Nyogo na timu nzima ya uwongozi kwa kuiongoza upinzani vyema wakati wote nilipokuwa nje, na waliweza kuwanganisha wanaCORD na tukabaki na mungano imara.

Katika Miezi yote mitatu niliyokuwa nje Wakenya walikuwa wakiwasiliana nami wakinieleza kero zao, wengine walinipigia simu,wengine waliniandikia barua, pia wengine walitumia Twitter kunielezea kero zao.
Mtoto aliyepigwa risasi Mombasa na mama yake kuuwawa niliskia, suala la kuongezeka kwa utovu wa usalama ambao unamhadhiri mdogo na mkubwa niliskia pia. Wakenya wamekuwa wakibaguliwa kwa dini zao kama vile waislamu wa Mombasa wanavyo nyanyaswa kuitwa magaidi.

Pia kama nilipokuwa nje Pesa za wananchi ziliibwa kulipwa kampuni hewa za marafiki wa rais kwa njia ya digitali, Watalii pia waliikimbia Kenya,pia watu wengi maelfu walipoteza kazi zao.

Pia bwana Raila Odinga aliweza kuiambia serikali kuwa iandae mkutano wa mapema iliwaweze kuongelea hali ya sasa ya nchi hiyo ya Kenya. Viongozi waote wa Cord waliweza kusema kwa pamoja kuwa siku ya saba saba itakuwa ndio siku yenyewe ya mkutano huo.

Wafuasi wa Cord Katika Uwanja Wa Uhuru Park

Friday, May 30, 2014

Mtanzania Ahusishwa Kuwa Mwanachama Wa Kundi La Kigaidi La Al-Shabab Atiwa Mbaroni Na Jeshi La kenya

Mahakama ya Kenya siku ya jana Alhamisi (tarehe 29 Mei) ilimshtaki raia wa Tanzania Ramadhan Mubarak kwa kuwa mwanachama wa al-Shabaab na kwa kuwa nchini kinyume cha sheria, maafisa wa serikali walisema.

Mubarak alishtakiwa katika mahakama ya Mandera ambapo alikiri tuhuma zote, Kamanda wa Polisi wa
Kaunti ya Mandera Nuhu Mwivanda alisema.

Mahakama ilimweka rumande Mubarak katika Gereza la GK la Mandera mpaka kesi ya hukumu yake itakapo tajwa hapo tarehe 2 Juni. 

Mwivanda alisema kuwa Mubarak alikamatwa tarehe 22 Mei katika mji wa Mandera wakati "alipojipenyeza kimya kimya kutoka Somalia".

"Mubarak aliwaambia wachunguzi kuwa alikimbia Somalia baada ya kukosana na al-Shabaab," Mwivanda alisema. "Alisema kuwa kundi halikutekeleza ahadi zao ikiwa ni pamoja na fedha.

Mwivanda alisema Mubarak amekuwa akiisaidia polisi kwa kutoa taarifa juu ya shughuli za al-Shabaab na kwamba uchunguzi ulikuwa ukiendelea. 

Wakati huo huo siku ya Jumatatu, washukiwa wengine wawili wa ugaidi walikamatwa katika katika mji wa Lafey wakiwa njiani kuelekea Mandera,gazeti la The Star la Kenya liliripoti. 

Polisi walisema wanaamini Yunis Mohammed Osman, Msomali, na Mahabub Aden Adow, Mkenya,walihusika na shughuli za uhalifu katika mkoa huo.

Mwivanda alisema kuwa watu wawili hao, ambao "walionekana wa kutiliwa shaka", walikuwemo
katika basi kutoka Nairobi.

"Mmoja wa maafisa wa polisi wetu ambaye alikuwemo kwenye basi hilo alisema, kulingana na
yeye, wakati wowote basi lilipokuwa linakaribia vizuizi vya polisi, Adow alikuwa anaficha Osman
chini ya kiti," alisema.

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score