Necta |
Matokeo ya kidato cha 4 mwaka 2013 yametangazwa, ufaulu umeongezeka kwa asilimia kati ya 0.61 na 16.72 ukilinganisha na mwaka 2012.
Jumla ya watahiniwa 427,679 waliandikishwa kufanya mtihani ila waliofanikiwa kufanya mtihani ni watahiniwa 404,083.
Jumla ya watahiniwa laki 235,227 sawa na asilimia 58.25 ya waliofanya mtihani wamefaulu.
Wasichana waliofaulu ni laki 106,792 na wavulana waliofaulu ni laki 128,435.
Jumla ya wanafunzi laki 151,187 wamepata '0' (division ziro) . Wasichana ni 72,237 na wavulana ni 78,950.
Jumla ya wanafunzi waliopata daraja la 4 (division 4) ni laki 126,828, wasichana wakiwa 62,841 na wavulana 63,987.
Wavulana waliopata daraja la tatu (Division 3) ni 27,904 na wasichana ni 17,113.
Waliopata daraja la pili (Division 2) Wavulana ni 14,167 na wasichana ni 7,561.
Wavulana waliopata daraja la kwanza (division one) ni 5,030 na wasichana ni 2,549.
Shule 10 zilizoongoza ni: St.Francis Girls, Marian Boys, Feza Girls, Precious Blood, Canossa, Marian Girls, Abbey
Shule kumi zilizoongoza: Anwarite Girls, Rosmini, na DonBosco Seminary.
Zilizofanya vibaya ni: Kisima, Kitongoni, Tongani, Njechele, Lumemo, Mvuti, Tambani, Nasibugani, Ungulu, Kitonga, Singisa, Hurui, Barabarani, Nandanga, Vihokoli, Chongoleani, Likawage, Gwandi, Rungwa, Uchindile.
Watahiniwa kumi bora ni: 1. Robina S. Nicholaus (Marian Girls), 2. Magreth Kakoko (St.Francis Girls), 3. Joyceline Leornard Marealle (Canossa), 4. Sarafina W. Mariki (Marian Girls), 5. Abby T. Seembuche (Marian Girls), 6. Sunday Mrutu (Anne Marie), 7. Nelson Anthony (Kaizerege), 8.Emmanuel Gregory (Kaizerege), 9. Janeth Urassa (Marian Girls) na 10. Angel Ngulumbi (St Francis)
Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 272 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani yao.
Bonyeza Linki hii Kuona Matokeo Yote
Matokeo Bonyeza Hapa
Mchimba Riziki