Saturday, January 25, 2014

Kesi Ya Kenyatta Utata Mtupu

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Alhamisi (tarehe 23 Januari) iliahirisha kwa muda usiojulikana tarehe ya kuanza kwa kesi uhalifu ya ubinadamu inayomkabili Rais Uhuru Kenyata kutokana na maombi ya waendesha mashitaka.
"Jopo la majaji liliiondosha tarehe ya kuanza kwa kesi ya tarehe 5 Fabruari 2014," ilisema mahakama hiyo kwenye taarifa yake, ikiongeza kwamba kikao kingeitishwa kujadili ombi hilo la upande wa mashitaka.
Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, aliomba ahirisho la miezi mitatu la kesi hiyo baada ya kusema mwezi uliopita kwamba hakuwa tena na ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi.

Majaji wa ICC walibainisha zaidi kwamba kufuatia ombi hilo la muendesha mashitaka, upande wa utetezi wa Kenyatta ulituma ombi la kufutwa kwa kesi kwa hoja ya kukosekana ushahidi wa kutosha, liliripoti gazeti la Daily Nation la Kenya.
Bensouda alisema angeweza tu kuendelea na kesi hiyo mara baada ya kuridhika kwamba ushahidi mpya utatosha kuisimamisha kesi hiyo.

Mchimba Riziki

Tuesday, January 21, 2014

VIDIC:MAN U KUCHEZA UEFA NI NDOTO

NAHODHA wa Manchester United, Nemanja Vidic, amekiri kwamba hawawezi kutetea ubingwa wao wa ligi kuu msimu huu baada ya
kupokea kichapo cha mabao 3-1 kwa Chelsea.
Beki huyo wa kati aliyeshuhudia wakipoteza mechi yao ya saba ya ligi
kuu Jumapili katika uwanja wa Chelsea Stamford Bridge,alisema kwamba ni muda tu kabla ya Mei ambapo watapokonywa kombe
hilo walilolishinda mara 20.
Aidha mlinzi huyo ambaye alionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchuano huo alidokeza kuwepo na uwezekano mkubw awa wa United
kukosa kushiriki UEFA msimu ujao kwani hata kujikatia tiketi kwa kumaliza katika nafsi za nne
za kwanza ligini, utakuwa ni tatizo kwao.
“Nadhani kwa sasa tupo mbali sana kuutetea ubingwa wetu na pengine tuwazie jinsi tunavyoweza kumaliza katika nafasi ya tatu au nne.
Ni suala ambalo sio rahisi kwetu na
itatulazimu kupigana kufa kupona kuhakikisha kuwa tunashiriki shindano la msimu ujao la
klabu bingwa Ulaya,” aliungama.
Matokeo ya wikendi yaliiacha United katika nafasi ya saba ikiwa nyuma ya vinara Arsenal kwa pointi 14. Na licha ya hilo kocha wake David Moyes ana mtazamo tofauti na nahodha wake.
Mkufunzi huyo anayezidi kukumbwa na presha katika klabu hiyo, amekakana kukubali wazo
kuwa kikosi chake hakiwezi kutetea ubingwa huo akishikilia kwamba bado wana nafasi.
“Hatuwezi kufa moyo kwa wakati huu na tutapambana hadi dakika ya mwisho. Majukumu yetu ni kujaribu kumaliza wa kwanza na hilo ndilo tutakalo kuwa tukijaribu kufanya,” Moyes alisema.
Muujiza
Hata hivyo kwa upande wake mkufunzi wa Chelsea, Jose Mouriunho. Mreno huyo anahisi
kwamba kwa United kuhifadhi kombe lao basi watahitaji muujiza wa aina fulani.
“Nina uhakika kuwa David hatakwazika nikimweleza ukweli kwamba wapo nyuma ya Arsenal kwa poiti 14, 13 dhidi ya Manchester City na 12 dhidi yetu. Ikiwa watataka kuhifadhi taji lao, basi pengine itokee kwamba timu tatu zilizoko juu zidorore kwa kiwango kikubwa huku nao wakishinda.
Labda pengine wajizatiti kumaliza wanne kwa sasa,” Mourinho alitoa
mtazamo wake.
MCHIMBA RIZIKI Michezo

Wala Mbwa kutokana na UkameKenya

Kisa cha kusikitisha kimeripotiwa kutokea katika jimbo la Turkana ambapo mwanamke mmoja mkongwe alilazimika kupikia familia
yake nyama ya Mbwa kutokana na uhaba wa chakula unaokumba eneo hilo.
Hali mbaya ya ukame imesababisha uhaba wa chakula na kuwalazimu baadhi ya wakaazi ambao ni wafugaji wa kuhamahama kula nyama ya Mbwa.
Tukio hilo limeripotiwa katika eneo la Kakuma ambapo akina mama wawili walipatikana wakikaanga kitoweo cha nyama ya Mbwa.
Chifu wa eneo hilo Cosmus Nakaya
amethibitishia BBC tukio hilo ambapo, wanawake wawili walikamatwa katika eneo hilo
ambalo ni hifadhi kwa maelfu ya wakimbizi kutoka Somalia,wakikaanga kitoweo cha nyama
hiyo tayari kuwalisha watoto.
Mama Akaran Aparo, mwenye umri wa miaka 73, aliambia maafisa kuwa alilazimika kupikia familia yake nyama hiyo kwani hakutaka kuiba Mbuzi au Kuku wa mtu kisha akamatwe na kufikishwa mahakamani.
Aidha Mama Aparo aliwaambia waandishi wa habari kwamba yeye hulazimika kusafiri umbali wa kilomita 3 kutafuta chakula katika kambi ya Kakuma ingawa hurejea na kidogo sana au wakati mwingine kukosa hata hicho kidogo.
Mama huyo alisema kuwa yeye hutegemea chakula cha msaada kwani anaishi na wajukuu wake watano ambao wazazi wao walifariki.
Anasema yeye hupokea chakula cha msaada lakini hajapokea chochote tangu mwezi Septemba mwaka jana.
Jimbo la Turkana ni kame sana ingawa hivi karibuni kumekuwa na habari njema kutoka katika jimbo hilo kwani visima vya mafuta
vimepatikana pamoja na visima vya maji vilivyo chini ya ardhi.
Utajiri huu unatarajiwa kuboresha maisha ya wenyeji ingawa hadi mavuno yatakapoanza kupatikana ndipo faida zitakapoanza kudhihirika kwa wenyeji wa jimbo hilo.
Uwezo wa Serikali kutoa msaada wa chakula umekuwa ngumu "alisema mama huyo".
Sitaki wajukuu wangu wateseke "aliendelea kusema mama huyo ajuza ".
Wakati alipokuwa njiani kuelekea katika kambi ya wakimbizi Kakuma, ndipo alipokutana mbwa huyo aliyejenga makazi yake na amezaa watoto watano,ndipo pale aliwachukua watoto wawili wa mbwa huyo kwenda kuwafanya kitoweo.
Kamanda Apiro anasema "mwanamke huyo aliwakata mbwa hao shingo na kuwakaanga kiasili bila kuwachuna ngozi".
Mwanamke nwenzake na mwenye umri kama wake Bi Eregae alisema kwamba "yeye alikuwa ameshindwa kwenda kwenye mahoteli makubwa kutokana na kuthoofika na njaa ".
Aliendelea kusema "mwenzangu aliniita na kuniambia yeye yuko na chakula tunaweza kushiriki"
Shahuda mmoja Peter Lomiyana alisema "aliona mbwa wawili wakikaangwa ndipo akawaita polisi.
"Wakawa wananiuliza kwanini polisi wanatuandama wakati tulisha kula mbwa wawili"alisema afisa wa polisi Samuel Osodo.
Afisa huyo aliendelea kusema msaada wa haraka unahitajika kuwasaidia wanawake hao na watoto walionao.
Chanzo BBC.
MCHIMBA RIZIKI

Ribbery na Benzema Watupwa Mahakama Kwa Kosa La Kufanya Ngono Na Kahaba

Wacheza soka wawili mashuhuri duniani, wamefikishwa mahakamani mjini Paris Ufaransa kwa kosa la kufanya ngono na
kahaba aliyekuwa na umri mdogo.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa hivi, alisema kwamba,Franck Ribery, mchezaji wa Bayern Munich , alimtumia kama zawadi
wakati wa sherehe za siku yake ya kuzaliwa mwaka 2009.
Inaarifiwa Ribbery alimlipia msichana huyo tiketi ya ndege aweze kusafiri kutoka Ujerumani Kuja Ufaransa kumtumbuiza Ribbery wakati wa sherehe hizo.
Alisema kuwa pia alilipwa ili afanye ngono na Karim Benzema anayecheza soka yake na klabu
ya, Real Madrid.
Kahaba huyo alisema kwamba, aliwaambia wawili, hao kuwa alikuwa mtu mzima wakati
huo.
Benzema amekanusha madai ya msichana huyo.
Wachezaji hao wanaweza kufungwa jela miaka mitatu kila mmoja ikiwa watapatikana na hatia.
Mchimba Riziki Michezo

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score