![]() |
| Gaza On Fire |
![]() |
| Gaza On Fire |
The World Reporter... Contact Mchimba Riziki.. +254715323229 Whatsapp..
![]() |
| Gaza On Fire |
![]() |
| Gaza On Fire |
![]() |
| John Heche Mwenyekiti Bavicha Taifa |
![]() |
| Wanausalama Wakimsachi Mfuasi wa CORD Kabla Ya Kuingia Uwanjani |
![]() |
| Vijana Wa CORD Wakiandamana Kabla Ya Mkutano Kuanza |
![]() |
| Wanausalama Wakiwa Kila Kona Kuhakikisha Usalama Katika Uwanja Wa Uhuru Park |
Kauli ya Rais Kenyatta inakuja kupitia kwa
televisheni siku moja baada ya kundi hilo kukiri
kufanya mauaji yaliyotokea Mpeketoni Jumapili
usiku.
Kenyatta emesema kuwa kuna ushahidi kuonyesha
kuwa shambulizi hilo lilipangwa vyema na kwamba
wanasiasa walihusika nao.
Al Shabaab lilikiri katika taarifa kwa vyombo vya
habari kuwa ndilo lilifanya mauaji hayo Jumatatu
jioni.
Alisema kuwa ujasusi ulitolewa kuwa mashambulizi
hayo yangefanyika lakini hawakuchukua hatua
zozote kuzuia mashambulizi hayo.
Rais amesema kuwa maafisa waliohusika tayari
wameachishwa kazi na kwamba watashitakiwa.
Wmaesema kuwa wanachunguza wanasiasa
waliohusika na mauaji hayo.
Mauaji zaidi yalifanyika usiku wa kuamkia leo licha
ya taarifa ya Al Shabaab kusema kuwa
washambuliaji walioshambulia Mpeketo walikuwa
wamerejea salama nchini Somalia.
Uharibifu mkubwa ulishuhudiwa katika mji huo huku
washambuliaji wakichoma hoteli na kituo cha polisi
pamoja na kuteketeza magari waliyoyatumia kwa
usafiri wao.
Kenyatta amesema kuwa kuna baadhi ya
wanasiasa wanaochochea uhasama miongoni mwa
jamii.
![]() |
| Wafuasi wa Railla Asubuhi ya leo |
![]() |
| Mh.Raila Odinga |
![]() |
| Necta |
![]() |
| Kondakta aliye achiwa mtoto |
![]() |
| Tang Yong Jian ametozwa faini ya dola laki mbili na thelathini |
![]() |
| Kenya inakabiliwa na changamoto ya kuwindwa kiharamu kwa Ndovu zake |
BARAZA la Madiwani wa halmashauri ya jiji la Arusha,limemtimua Mkurugenzi wa jiji hilo, Nd. Sipora Liana na wakuu wake wa idara, katika kikao cha madiwani baada ya kumpigia kura,wakidai Mkurugenzi huyo amezidi kuwadharau na kuwakejeli.
Mwanamume wa miaka 20 amepigwa na
kujeruhiwa vibaya na wananchi baada ya
kufumaniwa akishiriki kitendo cha ngono na
mbuzi kijijini Dabasom lokesheni ya Watamu
wilayani malindi.
MWANAMUME wa miaka 20 Alhamisi alipigwa na
kujeruhiwa vibaya na wananchi baada ya
kufumaniwa akishiriki kitendo cha ngonona
mbuzi kijijini Dabasom lokesheni ya Watamu
wilayani malindi.
Moses Katana alionekana na mwenye
mbuzi huyo ambaye alipiga mayowe
yaliyowavutia wanakijiji waliomkabili mshukiwa.
Baada ya kutandikwa vya
kutosha, mshukiwa
alikokotwa hadi ofisini
kwa chifu wa Dabaso Bw
Joseph Baya Maitha,
ambapo chifu aliwataka
maafisa wake wa polisi
wa utawala waingilie kati
na kumwokoa mshukiwa
aliyekuwa akiendelea kurushiwa makonde.
Baadaye mwanamume huyo alipelekwa katika
makao makuu ya polisi mjini Malindi na
kufunguliwa mashtaka ya kufanya kitendo cha
ngono na mnyama.
Chifu Baya alisema kwamba visa vya vijana
kupatikana wakishiriki vitendo vya ngono na
wanyama vimekuwa vikiongezeka mno katika
eneo hilo, na akawatahadharisha kwamba
watakabiliwa na mkono wa sheria iwapo
watapatikana.
Msomaji wangu kwa hayo yote nakuomba jaribu kuyapitia maandiko ya Mungu ili uweze kuyakemea mapepo kama haya.
Kumbukumbu La Torati 27:21 ama soma Kumbukumbu la Torati yote 27.
Mchimba Riziki
Wakazi katika kijiji kimoja cha Kaunti ya
Kakamega, jana asubuhi walipigwa na mshangao
baada ya watu wasiojulikana kufukua makaburi
mawili na kuiba maiti.
WAKAZI katika kijiji kimoja cha Kaunti ya
Kakamega, Jumanne asubuhi walipigwa na
mshangao baada ya watu wasiojulikana kufukua
makaburi mawili na kuiba maiti.
Wanakijiji cha Shirere walisema makaburi hayo
ni ya watu wawili wazaliwa wa Ulaya waliozikwa
mahali hapo yapata miaka 70 iliyopita.
Makaburi hayo, ambayo
yamo kwenye uwanja
wazi karibu na Shule ya
Upili ya Bishop Sulumeti
yalikuwa yametelekezwa
kwa muda mrefu.
Mzee wa kijiji, Bw Andrew
Andanyi alisema mmoja
wa watu waliozikwa mahali hapo alikuwa rubani
aliyekufa kwenye ajali ya ndege.
“Makaburi haya
yamekuwepo tangu 1940 nilipokuwa mvulana,”
alisema.
Wanakijiji walisema watu wawili wasiojulikana
walitembelea mahali hapo siku mbili kabla ya
tukio hilo.
Wezi hao waliacha chupa tupu za pombe, ishara
kwamba walikunywa pombe kabla ya kufukua
maiti hizo.
Naibu wa chifu wa sehemu hiyo, Bw Morris
Mukabane alisema tukio hilo linaendelea
kuchunguzwa.
Kwingineko, vijana waliokodishwa walifukua
maiti ya mfanyabiashara wa Nakuru ambaye
mkewe na wazazi wake wanazozania mahala
atakapozikwa.
Maiti ya Evans Bari Omuhindi ambayo ilikuwa
imezikwa kwenye makaburi ya Nakuru North
dhidi ya matakwa ya wazazi wake, ilifukuliwa
Jumatatu jioni kufuatia amri ya mahakama.
Mwanaume huyo aliyeaga dunia Novemba 1
alizikwa na mkewe Bi Jesica Kanyi lakini wazazi
wa mwenda zake na mwanamke anayedai kuwa
mkewe wa pili walienda kortini kupinga hatua
hiyo.
Watoto watatu
Walidai kwamba mwili wa marehemu ulifaa
kuzikwa katika kijiji cha Ebuskami Emanake,
nyumbani alikozaliwa katika eneo la Luanda
kulingana na mila za Waluhya.
Mamake marehemu Bi Sofia Nekesa alisema
hata kama mwanawe alikuwa akiishi mjini
Nakuru na mkewe wa kwanza na watoto wao
watatu, alikuwa pia amemuoa Bi Dinah Saisi na
wakapata naye mtoto mmoja.
Bi Saisi alikuwa
akiishi na wa wazazi wa marehemu eneo la
Luanda.
Jumanne, afisa anayesimamia kituo cha polisi
cha Nakuru Central alimwambia Hakimu Mkazi
wa Nakuru, Bi Victoria Ochanda kwamba polisi
walikuwa wameufukua mwili kama korti
ilivyoagiza.
Alisema mabaki hayo yalipelekwa kwenye
chumba cha maiti cha Manispaa ya Nakuru
ukingoja uamuzi wa korti.
Chanzo Taifa Leo
Shared by,
Mchimba Riziki.
Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi
alitangaza mpango huo wakati wa Siku 16 za
kampeni ya Harakati Dhidi ya Unyanyasaji wa
Kijinsia, kampeni ya kimataifa inayolenga kuinua
uelewa kuhusu suala hili.
Takribani asilimia 45 ya wakina mama wenye
umri wa miaka kati ya miaka 15 hadi 49 waliripoti
kunyanyaswa kimwili au kijinsia katika maisha
yao, kwa mujibu wa Utafiti wa Demografia na
Afya nchini Tanzania wa mwaka 2010.
Watoto nao wako katika hatari kubwa, msichana
mmoja kati ya watatu na mvulana mmoja kati
ya saba wamenyanyaswa kijinsia, na zaidi ya
asilimia 70 walinyanyaswa kijinsia kabla ya
kufikisha umri wa miaka 18.
"Jeshi la polisi linawajibika kuboresha mwitikio
wake kwa manusura wa [ukatili wa kijinsia] na
unyanyasaji wa watoto," Inspekta Jenerali wa
Polisi Said Mwema alisema.
Mchimba Riziki
Wakili wa Tanzania na mjumbe wa Tume ya
Kupitia Katiba (CRC) Sengondo Mvungi ,
aliyekuwa amejeruhiwa vibaya mapema mwezi
huu Alipovamiwa nyumbani kwake karibu
na jiji la Dar es Salaam, alifariki siku ya Jumanne katika hospitali moja
nchini Afrika Kusini.
Kiasi cha watu sita wanaoshukiwa kuwa wezi
waliokuwa wamebeba mapanga walimshambulia
Mvungi nyumbani kwake siku ya tarehe 2
Novemba.
Alipelekewa kwa haraka kwenye
Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Muhimbili
jijini Dar es Salaam ambako alikuwa kwenye
chumba cha wagonjwa mahututi hadi tarehe 7
Novemba,
aliposafirishwa kwenda Hospitali ya
Milpark jijini Johannesburg kwa matibabu zaidi.
Polisi hadi sasa wamewakamata washukiwa tisa.
Mwenyekiti wa CRC, Jaji Joseph Warioba,
alipeleka salamu zake za rambirambi kwa
familia ya Mvungi. "Alikuwa mtafiti ambaye
daima alikuwa na hamu ya kile alichokifanya.
Nilimjua na kufanya naye kazi hata kabla ya
kuwa mjumbe wa CRC, hivyo kifo cake kwa kweli
kimeniumiza," alisema Warioba.