Luis Suarez Alipomgata giorgio-chiellin |
SHIRIKISHO la soka duniani, FIFA limempiga marufuku ya mechi tisa na pia marufuku ya miezi minne straika wa Uruguay, Luis Suarez kushiriki mechi yeyote ile kwa kosa la kumng’ata beki wa Italia Giorgio Chiellini.
Kamati huru ya nidhamu ya chombo hicho ilimpata mshambuliaji huyo anayesakata soka ya kulipwa katika klabu ya Liverpool na hatia hiyo kwenye kisa kilichotokea Jumanne kwenye mechi ya mwisho ya kundi D timu hizo zilipokutana.
Hatua hiyo inamaanisha kuwa safari ya Suarez kwenye dimba la dunia limefikia ukingoni kwani atahitajika kuhudimia marufuku ya mechi tisa ya kimataifa.
Aidha adhabu hiyo itamfungia nje ya michuano tisa ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza punde msimu mpya utakapoanza hapo Agosti 16, 2014.
Taifa la Uruguay nalo limepewa siku tatu kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo na mawakili wa Suarez tayari wameonyesha nia ya kufanya hivyo.
Mara ya mwisho kwa adhabu kama hii kutolewa kwenye kombe la dunia ilikuwa 1994, dhidi ya beki wa Italia, Mauro Tassotti