Tuesday, June 3, 2014

Siri Kubwa Yafichuliwa Na Rais Museven. Ni siri Gani Hiyo?

Na Mathayo Ngotee

Siri ya utajiri ni kuepuka wanawake, pombe na sigara, kulingana na Rais wa Uganda Yoweri
Museveni. 

Rais Museveni Jumapili alieleza kuwa aliepuka anasa hizo akiwa bado ni kijana na badala yake akahifadhi pesa zake, hali iliyomwezesha kuwa na utajiri mkubwa alio nao hivi sasa.  “Sikuwa napenda wasichana. Nilikuwa nawapungia mkono tu kwa mbali kwa kuwa sikutaka kuharibu pesa zangu kwao,” akasema.

Aliongeza ilikuwa rahisi kwake kuweka pesa kwa akiba kwa vile hakuwa mnywaji pombe wala mvutaji
sigara.

Akizungumza wakati wa kufungwa kwa kongamano ya kibiashara mjini Mbiriizi, Wilaya ya Lwengo, Uganda, rais huyo alisisitiza kuhusu umuhimu wa kuhifadhi pesa huku akisema ilimsaidia kuwa tajiri hadi sasa hahitaji kuongezwa mshahara.

Katika kongamano hiyo, alizindua vyama vya mashirika 370 vilivyo vijijini, ambavyo vinatarajiwa kuhamasisha wanakijiji kuhusu umuhimu wa kuhifadhi pesa.

Aliwaambia wananchi wa Uganda wawe na desturi ya kuhifadhi pesa ili wao pia wawe matajiri kama yeye. “Ni muhimu muwe na desturi ya kuhifadhi pesa. Ninapozungumza kuhusu kuhifadhi pesa, najua kile ninachosema kwa kuwa nilianza kuweka kwa akiba pesa tangu nilipokuwa na umri wa miaka 21. Ni pesa hizo zilizoniwezesha kuwa tajiri nilivyo hii leo,” akasema.

Alizidi kusema, “Siku hizi ninasikia watu wakijadili kuhusu kuniongeza mshahara lakini ninahitaji mshahara kufanyia nini?” 

Bw Museveni ni mmoja wa viongozi wa mataifa ya Afrika ambao wamekuwa mamlakani kwa miaka mingi zaidi. Aliingia mamlakani mwaka wa 1986 baada ya kuhusika kwenye vita vilivyopelekea kupinduliwa kwa serikali za Idi Amin na Milton Obote.

Utawala wake umekumbwa na madai ya kuwa wa kiimla, kutokana na jinsi katiba ilivyobadilishwa kumruhusu aweze kuwa mamlakani kwa zaidi ya awamu mbili ilivyotakikana awali. Mwanasiasa wa upinzani nchini humo Kizza.

Besigye amekuwa akifungwa gerezani mara kwa mara kutokana na madai ya kuchochea ghasia anapoendeleza juhudi zake za kupigania kuwepo kwa haki za kidemokrasia Uganda.

Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi uliandaliwa 2006, ingawa ulikumbwa na matukio ya ghasia huku Dkt Besigye pia akikamatwa.

Rais Museveni pia amekuwa mstari wa mbele kati ya viongozi wa Afrika wanaokashifu mataifa ya Magharibi kwa kudai yanaingilia utawala wa mataifa ya Afrika.

Sunday, June 1, 2014

Unajuwa Nini Kuhusu Freemasons? Leo Nakutajia Mitume Kumi Na Wanane Wa freemasons..

Na Mathayo T Ngotee
Charta Ya Freemasons

Freemasons au Illuminati kama inavyojulikana na watu wengi nchini Kenya Ni dini Iliyokuwa kwa kasi kubwa sana katika karne ya 21. Dini hii imesambaa kote ulimwenguni kwa kasi kubwa sana. Dini hii imewateka watu wa rika mbalimbali wenye ulafi wa utajiri.

Katika vitabu vingi vya freemasons mitume walioandikwa wametoka katika kitabu takativu cha biblia. Nadhani hili halitakuwa na ubishi ukitegemea kuwa hawa freemasons chanzo chao ni kutokana kwa kuasi dini ya ukristo na kuanzisha dini yao.

Jumba La Freemasons
Dini hii ya freemasons ilitokana na wajenzi waliokuwa wakijenga kanisa la katoliki huko Roma Italia. Dini hii imekuwa dini ya siri kuliko dini zingine zote duniani. Dini hii inaarifiwa kuwa wengi waliomo ndani ni matajiri wakutupwa pia wanasiasa wengi duniani ni wafuasi wa dini hii ya siri.

 Pia kunaarifiwa kuwa watu wengi mashuhuri ni wafuasi wa dini hii iliyoenea Afrika mashariki pia, Viongozi wengi wa afrika mashariki wameripotiwa kuwa wafuasi wa dini hii. Watu Maarufu ulaya na Afrika Wapo,Vilabu vya soka,na Wanamuziki wengi wapo katika dini hii inayojiita The Secret Group.

Katika Makala Haya Nitawataja Mitume hao Kumi na wanane wanaopendwa na kudhaminiwa zaidi katika dini hiyo ya freemasons...

Listi ya Kwanza ni wale wakuu ambao wako nane
1.Joshua
2.Waamuzi
3.Samweli Wa Kwanza
4.Wafalme wa Kwanza
5.Wafalme wa Pili
6.Isaya
7.Yeremia
8.Ezekiel

Na Mitume wengineo ni
9.. Hosea
10.Amos
11.Obadia
12.Joeli
13.Yona
14.Mika
15.Nehemia
16.Habakuki
17.Zephania na
18.MAlaki

Kwa Hivyo basi kwa hitimisho hawa ndio mitume kumi na wanane wa Freemasons. Nipende kuwaambia kwa wale wakristo msishangae kuwa kunakuwaje wawe wa kutoka kwenye biblia ni kwamba ukweli kwamba freemasons ni wakatoliki walioasi dini. Pia Biblia ni kitabu kinachotumika na freemasons.

Baadhi Ya Magazeti Ya Kenya 01/06/2014 Yaliyopewa Leo Kipaumbele

Mchimba Riziki





Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score