Thursday, May 1, 2014

Wanawake Wengi Ruksa Owa Uwesavyo...Lakini Mwanamke Asiolewe Na Wanaume Wawili.... Wabunge Wanawake wapinga Hilo.....

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya siku ya Jumanne (tarehe 29 Aprili) aliusaini kuwa sheria mswaada wa ndoa unaowaruhusu wanaume wa Kenya kuoa wake wengi kadiri watakavyo, licha ya ukosoaji mkali kutoka kwa wabunge wanawake na mashirika yasiyo ya kiserikali.


Taarifa kutoka kwa ofisi ya rais ilithibitisha kwamba mswaada huo, ambao "unaziweka pamoja sheria mbalimbali kuhusiana na ndoa", ulishasainiwa kuwa sheria.
Sheria ya Ndoa ya mwaka 2014 inatafsiri aina mbalimbali za ndoa - zikiwemo za mke mmoja mume mmoja, za mume au wake wengi, za kimila, za Kikristo, za Kiislamu na za Kihindu - na pia inatoa njia za kutengana na talaka na ulezi na matunzo ya watoto inapotokea utengano na talaka.


"Ndoa ni muungano wa hiyari wa mume na mke, ama uwe muungano wa mke mmoja na mume mmoja au wa mume mmoja na wake wengi," ilisema taarifa ya ofisi ya rais.

Mswada wa awali ulikuwa umempa mke haki ya kulipigia kura ya turufu chaguo la mume, lakini wabunge wanaume walishinda migawanyiko ya kichama na hivyo kupitisha andiko ambalo liliondosha kifungu hicho.

Wakati bunge lilipopitisha mswada huo mwezi uliopita, wabunge wanawake walitoka nje ya mkutano wa bunge baada ya mjadala mkali.

Shirikisho la Wanasheria Wanawake nchini Kenya (FIDA) limesema litafungua pingamizi la kisheria dhidi ya sheria hiyo.

Baraza la Makanisa la Kenya, jumuiya inayokusanya zaidi ya makanisa na mashirika 40 ya Kikristo nchini kote, pia limezungumza dhidi ya sheria hiyo.

"Tunajua kuwa wanaume wanaogopa ulimi wa mwanamke kuliko lolote lile," alisema mbunge Soipan Tuya wakati mswada huo ulipopitishwa, liliripoti shirika la habari la AFP.

"Lakini hatimaye ikiwa wewe ndiye kiongozi wa nyumba na ukichagua kuongeza mshirika mwengine - na wakawa pengine wawili au watatu - nafikiri inakuhitaji kuwa mwanamme wa kweli kukubaliana kwamba mke na familia yako lazima ijuwe," alisema.

Wengi wamesema kuwa sheria hiyo inatambua tu kitu ambacho tayari kipo na kimesambaa.
"Unapomuoa mwanamke wa Kiafrika, lazima ajuwe kuwa mwengine anakuja, na mke wa tatu… hapa ni Afrika," mbunge Junet Mohammed aliliambia bunge wakati wa mjadala wa mswada huo.
Wanawake hawaruhusiwi kuolewa na mume zaidi ya mmoja.

Monday, April 28, 2014

Serikali Ya Somalia Yaikemea Kenya Yasema Inataka Ufafanuzi Juu Ya....... Diplomasia Baina Ya Nchi Mbili Hizi Iko Mashakani ...

WAZIRI Mkuu wa Somalia, Bw Abdiweli Sheikh Ahmed ameitaka Serikali ya Kenya kueleza kwa nini afisa wa ubalozi wa nchi hiyo alikamatwa jijini Nairobi wiki jana. Bw Ahmed pia alionya serikali ya Kenya dhidi ya kuwanyanyasa na kuwazuilia raia wa Somalia wasio na hatia wanaoishi Kenya.
Waziri Mkuu Wa Somalia Abdiweli Sheikh Ahmed
Kuingilia kwake suala hilo kunaweza kuzua mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili kufuatia kutoelewana kuhusu msako kwa polisi unaolenga mitaa wanayoishi raia wenye asili ya Kisomali.

Mamia ya maafisa wakuu wa serikali na raia wa Somalia wakiwemo wabunge wana makao jijini Nairobi.
“Serikali ya  Somalia inataka majibu rasmi kutoka kwa serikali ya Kenya kufuatia kukamatwa kwa afisa wa ubalozi wa Somalia nchini Kenya,, Siyad Mohamud Shire, ambako ni ukiukaji mkubwa wa kanuni za ulinzi za maafisa wa kibalozi,” ili

sema taarifa  kutoka ofisi ya Bw Abdiweli.
Aliongeza: “Serikali ya  Somalia imekuwa ikiwasiliana kila wakati na serikali ya Kenya kuhusu kuzuiliwa huku na inataka kuona serikali ya Kenya ikichukua kila juhudi kuhakikisha raia wa Somalia wasio na hatia wamelindwa,”
Alisisitiza kwamba ulinzi wa raia wa Somali wasio na hatia, baadhi ambao wamezuiliwa katika kambi kwenye uwanja wa michezo wa Kasarani ni muhimu.
Alisema baadhi ya raia wa Somalia wanaozuiliwa, wanatekeleza wajibu muhimu wa kujenga uchumi wa Kenya na wanapasa kutunzwa vyema.

Balozi Wa Kenya Nchini Somalia Na Rais Wa Somalia
“Serikali zetu zina tisho sawa  kiusalama, lakini kuendelea kuwazuilia raia wa Somalia kunaibua hofu na kutoaminiana ambako kutagawanya jamii zetu,” akasema.
Hii leo, balozi wa Kenya nchini Somalia Bw Josephat Maikara aliambia waandishi wa habari kwamba Bw Shire, aliyezuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilimani Ijumaa, aliachiliwa baada ya kutambuliwa. kuwa ni balozi wa Somalia nchini.
Bw Maikara alisema kukamatwa kwa afisa huyo hakuwezi kutia doa uhusiano wa Kenya na Somalia aliosema una mizizi na hauwezi kuvurugwa na misako inayoendelea kote nchini Kenya  na hailengi raia wa nchi fulani.

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score