Friday, February 14, 2014

Auwawa Akigombania Sigara

Tanga. Uvutaji wa sigara umeleta maafa,baada ya mtu mmoja kukatwa mkono na kuuawa na mwenzake wakati wakigombea
sigara.
Katika tukio hilo lililotokea Korogwe,
Jumapili iliyopita, Februari 2, mnamo saa nne asubuhi, Idi Mkono, mwenye umri wa miaka 30 alimkata mkono Ramadhani Gudelo (35) na kumuua baada ya kutokea ugomvi uliohusu sigara.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga,
Constantine Massawe alisema kuwa Polisi Tanga wako katika msako mkali wa kumtia nguvuni Iddi Mkono (30) kwa tuhuma za
mauaji.
Kamanda Massawe ameitaka jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, badala yake wafuate taratibu na sheria zilizopo.
Wakati huo huo, watu wawili
wanashikiliwa na polisi, mkoani hapa kwa tuhuma za kukamatwa na lita 147 za pombe haramu ya gongo maeneo ya Handeni, mkoani Tanga.
Kamanda Massawe alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa watuhumiwa hao lilitokea Februari 2 mwaka huu saa 5:30 asubuhi.
Massawe aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hussen Muhadu (48), pamoja na Ramadhani Ugarawe (40), wote wakazi wa Chanika Handeni.
Alisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Aidha Kamanda Massawe aliwaonya wananchi kuchukua tahadhari na matendo ya uhalifu wa aina yoyote ambao unaweza
kusababisha kuvunja sheria, huku akionya kuwa kwa yeyote atakayekiuka sheria zilizowekwa atashughulikiwa kwa mujibu
wa sheria na taratibu zilizowekwa.
Source Mwananchi

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score