VIONGOZI mjini Nakuru wameteta vikali baada ya kichinjio cha nyama ya punda kujengwa huko Naivasha. Hata hivyo, kunao waliosifu hatua ya kujenga kichinjio hicho wakisema ni biashara mwafaka.
Punda |
Naibu Gavana wa Nakuru John Ruto alipinga vikali uwepo wa kichinjio hicho huko Maraigushu.
Mbunge wa Naivasha John Kihagi naye alisema hatua hiyo chafulia Naivasha jina.
Bw Ruto alisema mkutano wa
washika dau akiwemo Mkuu wa Bora Afya wilayani Naivasha na Mkuu wa Idara
ya Matibabu ya Mifugo wataitwa ili kuelezea ni kwa nini walikubali ombi
la kujengwa kwa kiwanda hicho ambacho kitagharimu Sh15 milioni.
Kichinjio hicho ambacho
kinamilikiwa na wawekezaji kutoka China na Kenya kiko tayari kufunguliwa
baada ya wiki mbili zijazo mara tu serikali itakapotoa vibali vya
kusafirisha nyama hiyo kwenda Uchina.
“Hii itachangia wizi wa punda na
kisha kuuzwa hapo huku wasafirishaji nyama wakibeba mizoga ya punda bila
kujali kwani sasa itakuwa halali,” alilalamika mbunge wa Naivasha John
Kihagi.
Lakini Mkurugenzi wa kiwanda hicho John
Kariuki alipinga madai hayo akisema tayari wameweka makubaliano na
wafugaji wa punda huko Baringo, Nakuru, Laikipia na Samburu na hivyo basi
wako tayari kuanza kazi hiyo ambayo itawapa watu 30 kazi huku wengine
100 wakiajiriwa kama wafanya kazi na madereva humo.
Mbunge wa Molo Jacob Macharia
alifurahia biashara hiyo akisema sasa Wakenya watapata nafasi ya
kubadili mawazo potovu kuhusu nyama ya punda ambayo imekuwa ikiuzwa
kisirisiri katika maduka mbali mbali ya nyama, hasa ile ya nyama choma
na chemsha.
Bw Kihagi alisema huenda
akaelekea mahakamani kupinga ufunguzi rasmi wa kiwanda hicho akisema
kinaharibia wananchi na wanabiashara wa nyama jina huko Naivasha na
hivyo hakifai kufunguliwa kamwe.
Nafasi za kazi:
Lakini kiwanda kimepata idhini
kutoka kwa serikali huku nia yake ikiwa ni kuchinja punda na hatimaye
kusafirisha nyama hiyo hadi Uchina ambako ulaji wa punda ni kawaida.
Nyama Ya Punda |
Wazo hilo pia lilipata kuungwa
mkono na Mwakilishi wa Chama cha Wanabiashara Bw Njuguna Kamau ambaye
alisema Kenya inahitaji viwanda vingi ili kuongeza nafasi za kazi kote
nchini.
0 maoni:
Post a Comment