Saturday, March 23, 2013

KILA LA HERI STARS TUPO NYUMA YENU

 Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inashuka kwenye Uwanja wa Taifa kesho kuanzia saa 9:00
 alasiri tayari kuwavaa Morocco katika mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia,
zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.
Tanzania haijawahi kucheza fainali za Kombe la Dunia zaidi ya kuishia hatua za awali, lakini kama mikakati ikiandaliwa kikamilifu, nafasi hiyo ipo na inaweza kufika mbali.
Kama ilivyo kwenye msimamo, Tanzania inashika nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast ikiwa na pointi tatu, ikiwa ni pointi moja nyuma ya vinara hao wa pili kwa soka Afrika.
Morocco kabla ya mchezo wa kesho ina pointi mbili baada ya sare mbili wakati Gambia ni ya mwisho ikiwa na pointi moja.
Ushindi wa timu hiyo, utafufua na kutia chachu nafasi ya Tanzania kufika mbali katika fainali hizo za Kombe la Dunia kupitia Kanda ya Afrika.
Kinachotakiwa ni kwa wachezaji kucheza kwa nguvu, ari, moyo na mshikamano kuhakikisha wanashinda mchezo huo, huku kila mmoja kwa nafasi yake akiomba dua ya kheri na mafanikio kwa Taifa Stars.
Lazima Morocco washangazwe na soka ya Tanzania. Haiwezekani kila siku Nigeria, Ghana au Cameroon kama tuliwamudu Zambia na Cameroon katika mechi za kirafiki, kwa nini leo isiwe Morocco?
Vijana wa Kim Poulsen wafahamu kuwa Watanzania wako nyuma yao kuwashangilia, na watakuwa na nguvu zaidi kwa kuwa watakuwa kwenye uwanja waliozoea.
Ni uwanja ule ule walioifunga Zambia, ni uwanja huo huo walioifunga na Cameroon, hivyo hali hizo wanazijua, sasa ni ushindi kwa Morocco. Morocco ni timu ya kawaida sana na wanafungika kama wengine.
Kinachofurahisha zaidi ni kwamba, kwanza wachezaji wetu watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani ambao wanaweza kufanya lolote mbele ya mashabiki wao huku wakishangiliwa.
Wachezaji wetu watakuwa wanacheza katika uwanja na hali ya hewa walioizoea ambayo pia wanaweza kufanya lolote. Kumekuwa na tatizo la wachezaji wetu kucheza chini ya kiwango ama kucheza bila malengo, sasa ni wakati wa kutengeneza mipango.
Mara nyingi mipango inavurugika kutokana na kuwepo kwa hali mbaya ya hewa, kucheza kwenye baridi kama Ethiopia au kuchezea uwanja mbovu, lakini kwa Uwanja wa Taifa, Uwanja wa Uhuru, ni viwanja ambavyo si vigeni kabisa kwa wachezaji wetu.Wachezaji wetu wako nyumbani, ni nafasi ya wadau kutoa motisha kwa wachezaji ambayo ni wazi itakuwa chachu ya ushindi kwao. Lakini vilevile, isiwe wakaacha kucheza kwa nguvu kwa sababu ya kukosa chachu ya motisha

 Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inashuka kwenye Uwanja wa Taifa kesho kuanzia saa 9:00 alasiri tayari kuwavaa Morocco katika mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia, zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.
Tanzania haijawahi kucheza fainali za Kombe la Dunia zaidi ya kuishia hatua za awali, lakini kama mikakati ikiandaliwa kikamilifu, nafasi hiyo ipo na inaweza kufika mbali.
Kama ilivyo kwenye msimamo, Tanzania inashika nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast ikiwa na pointi tatu, ikiwa ni pointi moja nyuma ya vinara hao wa pili kwa soka Afrika.
Morocco kabla ya mchezo wa kesho ina pointi mbili baada ya sare mbili wakati Gambia ni ya mwisho ikiwa na pointi moja.
Ushindi wa timu hiyo, utafufua na kutia chachu nafasi ya Tanzania kufika mbali katika fainali hizo za Kombe la Dunia kupitia Kanda ya Afrika.
Kinachotakiwa ni kwa wachezaji kucheza kwa nguvu, ari, moyo na mshikamano kuhakikisha wanashinda mchezo huo, huku kila mmoja kwa nafasi yake akiomba dua ya kheri na mafanikio kwa Taifa Stars.
Lazima Morocco washangazwe na soka ya Tanzania. Haiwezekani kila siku Nigeria, Ghana au Cameroon kama tuliwamudu Zambia na Cameroon katika mechi za kirafiki, kwa nini leo isiwe Morocco?
Vijana wa Kim Poulsen wafahamu kuwa Watanzania wako nyuma yao kuwashangilia, na watakuwa na nguvu zaidi kwa kuwa watakuwa kwenye uwanja waliozoea.
Ni uwanja ule ule walioifunga Zambia, ni uwanja huo huo walioifunga na Cameroon, hivyo hali hizo wanazijua, sasa ni ushindi kwa Morocco. Morocco ni timu ya kawaida sana na wanafungika kama wengine.
Kinachofurahisha zaidi ni kwamba, kwanza wachezaji wetu watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani ambao wanaweza kufanya lolote mbele ya mashabiki wao huku wakishangiliwa.
Wachezaji wetu watakuwa wanacheza katika uwanja na hali ya hewa walioizoea ambayo pia wanaweza kufanya lolote. Kumekuwa na tatizo la wachezaji wetu kucheza chini ya kiwango ama kucheza bila malengo, sasa ni wakati wa kutengeneza mipango.
Mara nyingi mipango inavurugika kutokana na kuwepo kwa hali mbaya ya hewa, kucheza kwenye baridi kama Ethiopia au kuchezea uwanja mbovu, lakini kwa Uwanja wa Taifa, Uwanja wa Uhuru, ni viwanja ambavyo si vigeni kabisa kwa wachezaji wetu.Wachezaji wetu wako nyumbani, ni nafasi ya wadau kutoa motisha kwa wachezaji ambayo ni wazi itakuwa chachu ya ushindi kwao. Lakini vilevile, isiwe wakaacha kucheza kwa nguvu kwa sababu ya kukosa chachu ya motisha

0 maoni:

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score