Saturday, March 23, 2013

TOURE YAYA AITIKISA MANCITY

  Yaya Toure ameishtua klabu yake ya Manchester City kwa kusema atakuwa tayari kuondoka Etihad, labda kama atapewa mkataba mwingine kabla ya Jumamosi...Nipewe mkataba mwingine, vinginevyo naondoka, alisema Toure kiungo tegemeo la Man City. 


Kiungo huyo wa Ivory Coast amekasirishwa na ukimya wa mkataba wake mpya ambapo mazungumzo yamekwama kwa muda wa miezi sita sasa.
Wakala wa Toure, Dimitri Seluk, alikiri kwa kusema: Kama atasaini mkataba mpya ndani ya siku nne au tano, hiyo sawa. Kama hilo halitatimia, hakutakuwa tena na muda wa kusubiri na tutaanza mazungumzo na klabu nyingine mara moja. 

Tunataka watu wafahamu kinachoendelea kwenye klabu ili uamuzi wake wa kuondoka kama hatapewa mkataba mwingine basi iwe wazi,alisema. Leo ni Jumanne (juzi), kama mpaka Jumamosi hakutakuwa na mazungumzo ya mkataba mpya, tutasema asante, Yaya ataondoka City Mei, alisema wakala huyo. 

    Aliongeza kwa kusema:Sidhani kama ataendelea kubaki Manchester City. Siyo sababu ya pesa, anataka kuondoka kwa sababu kadhaa ndani ya klabu. Yeye ni mchezaji tegemeo kubwa Manchester City, lakini haoni kama anaheshimika na wafanyakazi wa klabu. Roberto Mancini peke yake ndiye anamuheshimu Yaya.


Kiungo huyo wa zamani wa Timu ya Barcelona ya Hispania (29), ndiye mchezaji anayelipwa pesa nyingi.
Man City inamlipa mshahara wake kwa wiki ni Pauni 220,000 tangu atue kutoka Barcelona. 

 Lakini wakala wake Seluk anasisitiza kwa kusema kwamba hajaomba kuongeza pesa zaidi, lakini hafurahishwi na mambo yanavyokwenda ndani ya klabu. 


Kuna mambo hafurahishwi nayo, anataka kwanza yawekwe vizuri.
Kwa sasa Toure, yuko na kikiso chake cha timu ya Taifa Ivory Coast kinachocheza mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 dhidi ya Gambia mwishoni mwa wiki hii.

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score