Sunday, March 10, 2013

UHURU MWOIGAE KENYATTA NDIE RAIS WA KWANZA CHINI YA KATIBA MPYA YA KENYA ILIYOITHINISHWA 2010

Rais Uhuru Mwoigae Kinyatta ndie mshindi wa kiti hicho mjue vizuri Uhuru ni naini katika medali za kisiasa.
Mh.Uhuru alizaliwa tarehe 26 october 1961. Yeye katika serikali iliyopita alikuwa ni makamu Waziri mkuu wa kenya.Katika  kupitia chama cha serikali hiyo iliyoingia madarakani 2008 Uhuru alikuwa pia ni Mp wa Gatundu South unity.

Uhuru ni mtoto wa mwaasisi wa nchi hii ya Kenya hayati Jommo Kenyatta aliyekuwa Rais wa jamhuri ya Kenya 1964-1978. Huyu Kenyatta ametokea katika kabila kubwa nchini Kenya la wakikuyu.
Uhuru alisoma shue moja nchini Kenya St.Mary,s school na baadaye kuondoka na kwenda kusomea siasa na utawala nchini Marekani katika chuo cha Amherest College.

Aliwahi kuteuliwa kama mbunge mteule na aliekuwa Rais wa pili Arap Moi mnamo mwaka 2001 na kufanya waziri katika kipindi hicho kifupi na baadae akawani urais kupitia chama cha KANU 2002 na alishindwa kwa kupata kura asilimia 30% tu na hapo alieshinda ni Rais aliepita mh.Mwai Kibaki..

Kenyatta alikuwa waziri wa finance mwaka 2009-2012. Pia Rais huyu mteule wa Kenya anashutuma ya kesi ya ICC kuhusiana na fujo na rabsha zilizotokea hapa Kenya mwaka wa 2007 na 2008.
Rais Uhuru aliithinishwa hivi janakuwa yeye ndie rais wa Nne na Rais wa kwanza chini ya Katiba mpya iliyoithinishwa na Wakenya mnamo mwaka 2010.




0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score