Wednesday, September 11, 2013

MAWAKILI WA AFRIKA MASHARIKI WASIMAMA KIDETE KUITETEA TANZANIA NA BURUNDI KUTOTENGWA (EAST AFRICA COMMUNITY)


CHAMA cha mawakili wa eneo la Afrika Mashariki kimewaandikia barua Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Katibu Mkuu wa Jamii ya Afrika Mashariki Dkt Richard Sezibera kikionya dhidi ya kutengwa kwa Tanzania kutoka kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Rais wa Chama cha Mawakili wa Afrika Mashariki (EALS) Bw James Mwamu Jumatano alionya kwamba kuendelezwa kwa mpangilio wa utangamano wa Afrika Mashariki unaosisitiza Kenya, Uganda na  Rwanda kama muungano wa mataifa matatu na washikadau wa eneo la Afrika Mashiriki huenda kukaathiri mshikamano wa mataifa wanachama.


Mataifa ya Tanzania na  Burundi yanaonekana kutengwa katika makongamano ya miundo msingi muhimu ya kimaendeleo yaliyoandaliwa majuzi nchini Kenya  na Uganda.


“Historia ina ushahidi tosha wa visa kama hivyo vilivyowahi kutokea kudhihirisha kwamba kutengwa kwa namna hiyo hatimaye kutazua tuhuma, kuzorotesha uhusiano baina ya mataifa wanachama, kurudiwa kwa juhudi na ushindano ulio na  uharibifu,” alisema Bw Mwamu katika barua yake ya Agosti 30.


Bw Mwamu alisema nchi za Tanzania na  Burundi zinapaswa kujumuishwa katika juhudi mpya za kuimarisha miundomsingi ya eneo ili kupata manufaa zaidi kwa mataifa hayo matano ambayo ni wanachama. Said Mr Mwamu: “Ni kutokana na haya ndiposa Chama cha Mawakili Afrika Mashariki  kinawarai Wastahiki, kama Rais na Viongozi wa kisiasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mtawalia, kutia juhudi zote katika kujumuisha taifa la Tanzania na Burundi katika jamii ya Afrika Mashariki.”


Kufurushwa

Nchi za Rwanda na Tanzania zimetofautiana kuhusu hatua ya hivi majuzi ya utawala wa Tanzania ya kuwafurusha wahamiaji, iliyolenga wahamiaji wasio halali hususan kutoka Rwanda waliokuwa wakiishi eneo la  Kagera.


Rais Museveni ndiye mwanachama wa muungano wa Jamii ya Afrika Mashariki na amehudhuria rasmi makongamano mawili kuhusiana na miundomsingi ambayo vilevile yalihudhuriwa na Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya na  Paul Kagame wa Rwanda.


Msemaji wa Rais Jakaya Kikwete Salva Rweyemama alieleza shirika la habari la Nation kupitia rununu kuwa kiongozi wa Tanzanian hakualikwa katika makongamano yote mawili kuhusiana na miundomsingi yaliyofanyika Mombasa na  Uganda.

MCHIMBA RIZIKI 

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score