Thursday, September 5, 2013

Kenya kupigia kura kujitoa ICC kabla ya kesi

Bunge la Kenya liliitwa siku ya Jumanne (tarehe 3 Septemba) kuzungumzia juu ya kumaliza uwanachama wa nchi hiyo kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kabla ya kesi dhidi ya uhalifu wa kibinadamu inayomkabili Naibu Rais William Ruto kuanza mjini The Hague wiki ijayo, liliripoti shirika la habari la AFP.Naibu Spika Joyce Laboso alitoa agizo ya "kikao maalum cha bunge" kukutana siku ya Alhamisi.

Hata hivyo, hata kama Kenya itaamua kujitoa kwenye ICC - ambayo itakuwa ni nchi ya kwanza kufanya hivyo - hakutaathiri kesi hizo kwani taratibu za kisheria tayari zimeanza. Ombi maalum la kujitowa pia litahitaji kuwasilishwa, hatua ambayo inaweza kuchukua miezi kadhaa.

Wabunge wanatarajiwa kujadiliana na kupigia kura uwezekano wa kujitoa kwenye Mkataba wa Rome wa ICC, kufuatia ombi kutoka kwa kiongozi wa Jubilee katika baraza la Seneti, Kithure Kindiki.

"Sheria yoyote humu nchini au ya kimataifa inaweza kufutwa au kurekebishwa," alisema Asman Kamama, mmoja ya wabunge wapatao 30 wanaouunga mkono azimio la Kindiki. "Si jambo la laana na tunataka kuwa kigezo barani humu."

Kesi ya Ruto inakuja ikiwa ni miezi miwili mbele ya ile ya Rais Uhuru Kenyatta, ambaye anakabiliwa na mashitaka matano ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwemo mauaji, ubakaji, ukatili, kuwalazimisha watu kuhama makaazi yao na matendo mengine yasiyo ya kiutu.

Wote wawili Kenyatta na Ruto wamesema watashirikiana kikamilifu na mahakama hiyo. Wanakana mashitaka dhidi yao.

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score