Monday, September 2, 2013

Watu saba wauza madawa ya kulevya wakamatwa Nairobi Wamo Watanzania wawili,Wahindi Wawili Na Wakenya Watatu.



Polisi ya Kenya imewakamata Watanzania wawili, Wakenya watatu na Wahindi wawili kwa tuhuma ya kutengeneza madawa aina ya crystal methamphetamine jijini Nairobi,
 gazeti la The Standard la Kenya liliripoti Jumapili (tarehe 1 Septemba).

Watuhumiwa walikamatwa kwa kumiliki kilogramu 50 za madawa haramu na yanakadiriwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 2 (dola milioni 1.2),gazeti la The Citizen la Tanzania liliripoti.

Watanzania Rumishaeli Mamkuu Shoo, miaka 27, na January Gabriel Liundi, miaka 30, walikamatwa Alhamisi katika gari lililobeba kifaa cha kutengenezea madawa ya kulevya na malighafi za madawa.
 Washukiwa kutoka Kenya na India walikamatwa katika Eneo la Biashara la Cape, katika majengo ambayo yamebadilishwa kuwa maabara ya kutengeneza madawa ya kulevya, kwa mujibu wa Naibu mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai Gideon Kimilu.

Inaaminika washukiwa hao ni sehemu ya ushirika ambao unatengeneza madawa ya kulevya nchini Kenya na kuyasafirisha kwenda Afrika Kusini.
Watuhumiwa Walifikishwa mahakamani leo Jumatatu.

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score