Tuesday, March 18, 2014

Mombasa Kenya Ni Hatari: Njama ya mashambulizi yatibuliwa Kenya,Mombasa

Polisi mjini Mombasa pwani ya Kenya wamewakamata watu wawili waliokuwa na mabomu waliyoyatengeneza ndani ya gari lao:

Mji wa Mombasa umekuwa ukishuhudia machafuko yanayosababishwa
 na vijana wanaokumbatia itikadi kali za dini
Kwa mujibu wa polisi washukiwa hao mmoja raia wa Kenya na mwingine msomali, walikuwa wanajiandaa kufanya mashambulizi katika eneo lisilojulikana.

Inaarifiwa polisi waliwakamata baada ya kupata taarifa kuhusu njama yao.

Vyombo vya habari vinasema kuwa usalama umedhibitiwa mjini humo kufuatia tukio hilo.

Mchimba Riziki

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score