Thursday, May 1, 2014

Wanawake Wengi Ruksa Owa Uwesavyo...Lakini Mwanamke Asiolewe Na Wanaume Wawili.... Wabunge Wanawake wapinga Hilo.....

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya siku ya Jumanne (tarehe 29 Aprili) aliusaini kuwa sheria mswaada wa ndoa unaowaruhusu wanaume wa Kenya kuoa wake wengi kadiri watakavyo, licha ya ukosoaji mkali kutoka kwa wabunge wanawake na mashirika yasiyo ya kiserikali.


Taarifa kutoka kwa ofisi ya rais ilithibitisha kwamba mswaada huo, ambao "unaziweka pamoja sheria mbalimbali kuhusiana na ndoa", ulishasainiwa kuwa sheria.
Sheria ya Ndoa ya mwaka 2014 inatafsiri aina mbalimbali za ndoa - zikiwemo za mke mmoja mume mmoja, za mume au wake wengi, za kimila, za Kikristo, za Kiislamu na za Kihindu - na pia inatoa njia za kutengana na talaka na ulezi na matunzo ya watoto inapotokea utengano na talaka.


"Ndoa ni muungano wa hiyari wa mume na mke, ama uwe muungano wa mke mmoja na mume mmoja au wa mume mmoja na wake wengi," ilisema taarifa ya ofisi ya rais.

Mswada wa awali ulikuwa umempa mke haki ya kulipigia kura ya turufu chaguo la mume, lakini wabunge wanaume walishinda migawanyiko ya kichama na hivyo kupitisha andiko ambalo liliondosha kifungu hicho.

Wakati bunge lilipopitisha mswada huo mwezi uliopita, wabunge wanawake walitoka nje ya mkutano wa bunge baada ya mjadala mkali.

Shirikisho la Wanasheria Wanawake nchini Kenya (FIDA) limesema litafungua pingamizi la kisheria dhidi ya sheria hiyo.

Baraza la Makanisa la Kenya, jumuiya inayokusanya zaidi ya makanisa na mashirika 40 ya Kikristo nchini kote, pia limezungumza dhidi ya sheria hiyo.

"Tunajua kuwa wanaume wanaogopa ulimi wa mwanamke kuliko lolote lile," alisema mbunge Soipan Tuya wakati mswada huo ulipopitishwa, liliripoti shirika la habari la AFP.

"Lakini hatimaye ikiwa wewe ndiye kiongozi wa nyumba na ukichagua kuongeza mshirika mwengine - na wakawa pengine wawili au watatu - nafikiri inakuhitaji kuwa mwanamme wa kweli kukubaliana kwamba mke na familia yako lazima ijuwe," alisema.

Wengi wamesema kuwa sheria hiyo inatambua tu kitu ambacho tayari kipo na kimesambaa.
"Unapomuoa mwanamke wa Kiafrika, lazima ajuwe kuwa mwengine anakuja, na mke wa tatu… hapa ni Afrika," mbunge Junet Mohammed aliliambia bunge wakati wa mjadala wa mswada huo.
Wanawake hawaruhusiwi kuolewa na mume zaidi ya mmoja.

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score