Friday, May 30, 2014

Mtanzania Ahusishwa Kuwa Mwanachama Wa Kundi La Kigaidi La Al-Shabab Atiwa Mbaroni Na Jeshi La kenya

Mahakama ya Kenya siku ya jana Alhamisi (tarehe 29 Mei) ilimshtaki raia wa Tanzania Ramadhan Mubarak kwa kuwa mwanachama wa al-Shabaab na kwa kuwa nchini kinyume cha sheria, maafisa wa serikali walisema.

Mubarak alishtakiwa katika mahakama ya Mandera ambapo alikiri tuhuma zote, Kamanda wa Polisi wa
Kaunti ya Mandera Nuhu Mwivanda alisema.

Mahakama ilimweka rumande Mubarak katika Gereza la GK la Mandera mpaka kesi ya hukumu yake itakapo tajwa hapo tarehe 2 Juni. 

Mwivanda alisema kuwa Mubarak alikamatwa tarehe 22 Mei katika mji wa Mandera wakati "alipojipenyeza kimya kimya kutoka Somalia".

"Mubarak aliwaambia wachunguzi kuwa alikimbia Somalia baada ya kukosana na al-Shabaab," Mwivanda alisema. "Alisema kuwa kundi halikutekeleza ahadi zao ikiwa ni pamoja na fedha.

Mwivanda alisema Mubarak amekuwa akiisaidia polisi kwa kutoa taarifa juu ya shughuli za al-Shabaab na kwamba uchunguzi ulikuwa ukiendelea. 

Wakati huo huo siku ya Jumatatu, washukiwa wengine wawili wa ugaidi walikamatwa katika katika mji wa Lafey wakiwa njiani kuelekea Mandera,gazeti la The Star la Kenya liliripoti. 

Polisi walisema wanaamini Yunis Mohammed Osman, Msomali, na Mahabub Aden Adow, Mkenya,walihusika na shughuli za uhalifu katika mkoa huo.

Mwivanda alisema kuwa watu wawili hao, ambao "walionekana wa kutiliwa shaka", walikuwemo
katika basi kutoka Nairobi.

"Mmoja wa maafisa wa polisi wetu ambaye alikuwemo kwenye basi hilo alisema, kulingana na
yeye, wakati wowote basi lilipokuwa linakaribia vizuizi vya polisi, Adow alikuwa anaficha Osman
chini ya kiti," alisema.

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score