Thursday, July 17, 2025

Je Nini Chanzo Cha Kauli Mbiu Ya ONE TERM (WANTAM) Nchini Kenya?

Kauli mbiu ya "One Term" au "WANTAM" imeibuka kama wito wa kisiasa unaoashiria kutoridhika kwa wananchi na utawala wa sasa wa Rais William Ruto, wakitaka asihudumu kwa muhula wa pili Mpaka mwaka 2027. Hii inaashiria mabadiliko makubwa katika siasa za Kenya kuelekea uchaguzi wa 2027.


Zifuatazo Ni Sababu Za Kauli Hii Kuhusu Siasa Za Kenya Kuelekea 2027

17 July 2025
Na Mathayo Tajiri Mollel.
Arusha Tz.

🔗. Kukosekana kwa Uaminifu kwa Serikali ya Ruto.
HIi inaweza kuwa sababu kuu, wananchi wengi wamepoteza imani na serikali kutokana na ahadi nyingi zilizoahidiwa na serikali ya Kenya Kwanza (KK) ambazo Mpaka Sasa mpango wa utekelezaji hamna, ongezeko la ushuru, na ukandamizaji wa maandamano ya amani. Hali hii imeongeza wito wa kauli hii ya "One Term" miongoni mwa wapiga kura wengi Nchini Kenya.

🔗. Uasi wa Kizazi cha Gen Z.
   Vijana wa kizazi cha Gen Z wamekuwa mstari wa mbele katika maandamano ya kidijitali na ya mitaani, wakipinga ukandamizaji wa haki za kiraia na ukosefu wa fursa za kiuchumi. Hii inaonyesha mabadiliko ya nguvu za kisiasa kuelekea kizazi kipya. Serikali ya Kenya imekuwa ikitafuta njia ya kuongea na vijana wa kizazi cha Gen-z bila mafanikio kwa kuwa vijana wamegura na kukataa maongezi yoyote na serikali.

🔗. Uwezekano wa Wapinzani Wapya
   Kando na vijana wa kizazi cha Gen-z kuibuka wakiwa na nguvu kubwa katika kuendesha mabadiliko haya ya serikali Nchini Kenya, kuna Majina mapya kama Jaji Mkuu Mstaafu David Maraga, Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Fredi Matiangi, yameanza kutajwa kama wagombea wa urais, wakiahidi uadilifu na mageuzi ya kweli. Hii inaweza kuvuruga hesabu za kisiasa za vyama vikuu katika uchaguzi mkuu Wa 2027. Pia itachochea kauli ya (WANTAM) Kupata nguvu zaidi ikididiza ndoto za rais Ruto Kuendelea na awamu ya pili.

🔗 Uteuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC)
   Rais Ruto ameteua makamishna wapya wa IEBC, hatua inayozua wasiwasi kuhusu uhuru wa tume hiyo na uadilifu wa uchaguzi ujao. Hili nalo litaendelea kuibua mjadala mkubwa mno ambao utaamsha hasira ya vijana kuendelea kuimba wimbo wa (WANTAM).

🔗 Mgawanyiko Ndani ya UDA
   Chama tawala cha UDA kinakabiliwa na migawanyiko ya ndani, hasa baada ya Rais Ruto kumfukuza aliyekuwa Naibu wake Rigathi Gachagua na wandani wake wote, hali imeweza kudhoofisha chama tawala cha UDA na itaadhiri sana kampeni zao za 2027. Kwa sasa Bwana Rigathi Gashagua ameanzisha chama chake kipya kinachoitwa DCP ambacho kinaungwa mkono sana Central Kenya na kwingineko.


🔗 Uhamasishaji wa Vijana na Makundi Maalum
   Mashirika ya kiraia yanahamasisha vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kujiandikisha kupiga kura na kugombea nafasi za uongozi. Hili ni jukumu ambalo wakenya wengi wamelichukulia kwa uzito mkubwa sana ili kutimiza ahadi waliyojiwekea ya (WANTAM).


Kuna mazungumzo kuhusu mageuzi ya kikatiba kabla ya 2027, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya mfumo wa utawala na ugatuzi(serikali ya majimbo), ambayo yanaweza kuathiri mwelekeo wa siasa za kitaifa.

Kwa ujumla, siasa za Kenya kuelekea 2027 zinaonyesha mabadiliko makubwa, huku wananchi wakitaka uwajibikaji zaidi, usawa, na uongozi wa kweli. Kauli mbiu ya "One Term" ni ishara ya kutoridhika kwa wananchi na wito wa mabadiliko ya kweli katika uongozi wa taifa.

Mathayo Mollel
+254721700996
+255758768243

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score