Friday, March 8, 2013

IEBC YAENDELEA KUTOA MATOKEO YA URAIS KENYA

Ni mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Kenya bwana Aissack Hassan katika harakati za kutangaza matokeo ya mshinani.
.
Leo hii kuanzia nyakati za jioni Tume hiyo itatangaza matokeo ya Urais inayosubariwa kwa hamu na mamilioni ya Wakenya na hata nje ya Kenya.katika kura zilizokwisha kutangazwa inaonekana kwamba Bwana Uhuru Kenyatta naongoza kwa kuwa na kura 5,159,344 huku akifuatiliwa na aliekuwa waziri mkuu wa Kenya bwana Raila Odinga mwenye kura 4,516,660 akifuatiwa nae Mudavadi alikwisha kukiri kushindwa katika uchaguzi huo.

 Pia siku ya jana viongozi wa mrengo wa Cord walisema lazima waende kortini kwa sababu ya kutorithika na matokeo yanayoendelea kutangazwa na tume hiyo ya IEBC.Walisema kwamba matokeo hayo yaliorudiwa kuhesabiwa yalikuwa na maneno ndani.

Endelea kufuatilia blog yetu kwa kila hatua tunayo piga kwa updates moto moto kutoka hapa nchini Kenya. 

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score