Friday, March 8, 2013

MUDAVADI AKIRI KUSHIDWA KATIKA UCHAGUZI

Musali Muadavadi ambae alikuwa anawania urais kupitia mrengo wa AMANI.
Leo hii ametokeza mbele ya vyombo vya habari na na kutangaza kushindwa katika uchaguzi uliofanyika March 4.

Akionge mbele ya waandishi Musalia amabae alikuwa ni waziri mkuu mzaidizi katika serikali ya pamoja,amesema amekubali kwamba ameshindwa na kuwahimiza wakenya kuishi kwa amani..
Muasali aliewahi kuwa mwanachama wa ODM na mwishoni mwa mwaka jana aliamua kujitoa katika chama hicho kinacho ongozwa na waziri mkuu kwa kudai kwamba hakuna demokrasia chamani hapo.

Pia katika kuhamia chama cha UDF ambacho alikuwa mgombea urais kupitia chama hicho aliwahi kujiunga na mrengo wa JUBELEE mwanzoni mwa mwaka huu na kujiondoa baada ya kuona kwamba Uhuru na Ruto hawataki kumuachia mtu mwingine aiongoze mrengo huo wa Jubilee.

Bwana Mudavadi  ameahidi wakenya kwamba atashirikiana na Rais atakae shinda katika uchaguzi huu katika ujenzi wa taifa laKenya.Amesema pia Mrengo alioongoza yeye pamija na Eugin wa Malwa utaiheshimu serikali itakayo ingia madarakani..

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score