Tajiri wa Urusi afariki
Kilichosababisha kifo cha tajiri Boris Berezovsky, mwenye umri wa miaka 67, bado hakijajulikana.
Tajiri huyo alikuwa akisakwa mno nchini Urusi, na anafahamika kuwa mpinzani mkali wa RaisZamani alikuwa na mamlaka na ushawishi sana katika bunge la Kremlin, lakini yote hayo yalididimia mara tu alipoingia Bw Putin, na Berezovsky alikimbilia Uingereza kuanza maisha ya uhamishoni mwaka 2000.
Awali idara ya polisi ya Thames Valley ilitangaza kwamba ilikuwa katika hatua za kuchunguza kifo cha mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 67, katika eneo la Ascot, Berkshire.
Mwaka uliopita, Bw Berezovsky alishindwa katika kesi ambayo aliwasilisha madai ya kutaka kulipwa pauni bilioni tatu, dhidi ya tajiri anayemiliki klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich.
Bw Berezovsky alidai alitishwa na Bw Abramovich, kiasi cha kuuza hisa za kampuni kubwa ya mafuta nchini Urusi, Sibneft, kwa kiwango kidogo mno cha fedha, ikilinganishwa na thamani halisi ya hisa hizo.
Madai hayo yalikataliwa moja kwa moja na hakimu wa masuala ya biashara mjini London, na ambaye alisema Bw Berezovsky si shahidi wa kuaminika.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya kimataifa, Richard Galpin, alisema watu mbalimbali walimueleza kwamba Bw Berezovsky alisongwa na mawazo kufuatia kushindwa katika kesi hiyo, na kuandamwa na matatizo mbalimbali ya kifedha.
Tajiri huyo mkuu inasemekana alipoteza kiasi kikubwa cha mali katika miaka ya hivi karibuni, na akiwa katika hali ya kulipa gharama mbalimbali za kesi nyingi alizoziwasilisha mahakamani.
Boris Berezovsky alikuwa kati ya kundi dogo la matajiri wakuu wa Urusi, na ambao walifurahishwa na kuangamia kwa siasa za kikomunisti, na wakitumia
waliowafahamu katika madaraka ya juu kwa misingi ya kujitajirisha haraka.
Huku mamilioni ya raia wa Urusi wakitumbukia katika umaskini, Berezovsky aliingia katika biashara, na kuuza magari, na pia kununua hisa katika kituo kikuu cha matangazo ya televisheni nchini Urusi.
Aliwekeza pia katika shirika la ndege la Aeroflot, na vile vile katika kampuni ya mafuta.
Vile vile wakati huo alikuwa ni rafiki mkuu wa rais wakati huo, Boris Yeltsin, na uhusiano huo ukampa mamlaka mno katika bunge la Urusi.
Lakini Vladimir Putin akawa ni rais tofauti kabisa, akiwa kiongozi wa Kremlin ambaye hakutaka hata kidogo kuelezewa namna ya kuiongoza Urusi.
Ndipo hapo Berezovsky alipopoteza ushawishi wake katika Kremlin, na kutoroka hadi mjini London.
Source BBC
0 maoni:
Post a Comment