Saturday, April 20, 2013

KIKITWE HUKO UHOLANZI



Rais Jakaya Kikwete amewataka wawekezaji katika sekta ya kilimo cha maua, mbogamboga na matunda kutoka nchini Uholanzi kuja Tanzania kuwekeza katika ukanda wa nyanda za juu kusini ambazo amesema zina kila sifa ya kuchochea maendeleo ya wawawekezaji na wananchi kutokana na hali na mazingira husika.
Dkt. Kikwete ametoa wito huo katika mazungumzo yake na wawekezaji katika sekta ya kilimo cha matunda, mbogamboga na mbegu, mazungumzo yanayolenga kuvutia uwekezaji katika maeneo ambayo bado hayajatumika kikamilifu.
Ziara ya Rais Jakaya Kikwete nchini Uholanzi imemfikisha katika vitalu vya wazalishaji wa mbegu za miti, kilimo cha mboga na matunda mazao ambayo kwa hali ya hewa na mazingira ya tanzania yanastawi na kutumika kama chakula pia yanaweza kutumiaka kuliingizia taifa kipato kupitia fedha za kigeni.
Baada ya kupata maelezo juu ya uzalishaji wa mazao hayo, Rais Kikwete alipitishwa katika vitaru vya miche na kupewa maelezo juu ya uzalishaji wenye tija na jinsi ya kuondokana na magonjwa yanayoshambulia mazao.
Ulipotimu wakati wa Dkt. Kikwete kuzungumzia maonyesho hayo, akakiri kuwa maonyesho hayo yamekuwa masomo ya ziada ambayo kwa maelezo mepesi yanajulikana kama ‘tuition’.
Dkt. Kikwete amesema wawekezaji katika sekta ya kilimo wanaweza kubadili pato la taifa.
Rais Kikwete anaendelea na ziara yake na anakusudia kukutana na kufanya mazungumzo na mke wa mtoto wa Malkia, Princess Maxima.


SOURCE TBC

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score