Saturday, September 21, 2013

Alshabab wakiri kutekeleza utekaji Wa Westgate

Wapigani wa Somalia Alshabab wamekiri jioni hii kuwa wao ndio waliiohusika katika shambulizi lililotokea leo mapema hapa Nairobi saa 11:50.Wapiganaji hao waliandika katika mtandao wao wa Twitter kwamba wamefanya hivyo kwa sababu ya kulipisha kizazi ya majeshi ya Kenya kuingilia Somalia kuwathibiti wao.


Mujahideen waliingia ndani ya jengo hilo la kibiashara leo mchana na mpaka sasa bado wapo ndani ya jengo hilo la Westgate.na waliingia humo kupambana na ma-Kafiri wa Kenya ndani na waliingia ndani ya himaya yao walisema kundi hilo la Jihad Somalia

Wakenya kazi yao sasa ni kuwasubiri ama kuangalia nini kitafanywa na Majeshi yao ndani Westgate kwani mpaka sasa Majambazi hao bado wanasadikika kuwa wamo ndani ya Jengo hilo na kuna raia wanaoshikiliwa na kundi hilo baya kwa usalama.

Al-shabab pia wamejitapata kuwa watu waliowaua ni 100 na sio 30 kama ilivyoripotiwa na Kenya Red Cross lilisema kundi hilo.

Kwa upande wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya wao wamesema watu waliouwawa ni 30 na waliojeruhiwa ni 60 hadi kufikia muda huu.Ambapo bado watu wanaokolewa .

Ikumbukwe kwamba Majeshi ya Kenya yaliingia nchini Somalia miaka miwili iliyopita  kupambana na Al-shabab,na mpaka sasa majeshi hayo ya Kenya yamebaki katika nchi ya Somalia kama majeshi ya Umoja wa Afrika na ilihaidi kuisaidia Somalia, pia majeshi hayo yanaungwa mkono na Umoja wa Kimataifa.


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score