Wednesday, September 18, 2013

Wabunge walimana makonde Nigeria kuhusu siasa za chama cha PDP Kujigawa





LAGOS, Nigeria

WABUNGE katika bunge la Nigeria Jumanne walilimana mangumi na mateke baada ya kundi moja lililojitenga kutoka kwa chama kinachotawala kuruhusiwa kuingia bungeni.

Kituo cha kibinafsi cha runinga cha African Independent Television pamoja na Channels TV vilionyesha picha za mbunge mwanamke aliyejawa na hasira akimchapa mwenzike usoni huku mbunge mwingine mwanamume akionekana akichukua kiti na kumchapa mwenzake.

Wabunge wengine walionekana wakiwapiga wenzao ngumi. Vurugu hizo zilianza baada ya kuwasili kwa Kawu Baraje, mwenyekiti wa kikundi kilichojitenga kutoka kwa Chama cha Peoples Democratic Party (PDP) ambaye aliambatana na magavana wanaomuunga mkono.

Spika wa bunge la wawakilishi, Aminu Tambuwal, aliwaambia wabunge kwamba Baraje alikuwa ameomba ruhusa kuwahutubia wafuasi wake katika hafla ya ufunguzi wa bunge.

Lakini kuwasili kwa kundi hilo kuliwakasirisha wabunge wa chama halisi cha PDP. Kelele zilianza, Baraje alipokuwa akiwahutubia wabunge. Chama cha PDP kina viti 23 kati ya 36 katika bunge hilo.

Chama hicho ambacho kimekuwa mamlakani tangu 1999, kimejipata pabaya katika siku za hivi majuzi. Kimekumbwa na mgawanyiko na upinzani mkubwa.

Chama hicho kinatazamwa kama kitaweza kukabiliana na tofauti zilizoko na kuchukua tena urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanywa 2015.

Mgawanyiko umedumu kwa miaka kadha huku wanachama wengine wakipinga ushindi wa Rais Goodluck Jonathan.

By Mchimba Riziki

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score