Tusome
Isaya 40:6-8 na Zaburi 8:3-8. Sikiliza sauti ya mtu asemaye, “Lia kwasababu
wote wenye mwili ni majani ambayo hukauka na maua yanayonyauka, bali Neno la Mungu
litasimama milele.”
Mwanadamu
maisha yake ni mafupi, kwahiyo acha maringo, majivuno, kujisifu kwaajili ya
pesa yako au mali
zako, bali jisifu kwaajili ya utukufu wa Mungu.
Mwanadamu ni mavumbi, na kumbuka tutarudi mavumbini. Huu ni muda wako wa
kufanya kazi ya Mungu kabla hujarudi mavumbini kwani hujui ni saa ngapi na lini
utakuwa mavumbi.
Kuna watu baada ya kupata mafanikio wanaanza kujidai na kuringa kutoka na
kidogo ambacho Mungu amempa. Mafanikio yako siyo kwaajili ya wewe kuonyesha
kiburi na kuwalingia wengine. Mungu amekupa hayo mafanikio ili ufanye kazi
yake.
Mungu alikupenda wewe mwanadamu na kukupa upendeleo mkubwa ukifananisha na wanyama wakubwa kama tembo na simba aliowaumba. Iweje leo umsahau Mungu na kuona wewe ndio kila kitu hapa duniani. Kumbuka upo kwa neema ya Mungu.
ACHANA JEURI NA DHARAU
Ewe mwanadamu achana na jeuri, kiburi havitakusaidia lolote na kumbuka ni wapi Mungu amekuokota. Ulikuwa huna kitu na ulikuwa mwaminifu kwa Mungu, lakini leo unamdharau Mungu wako baada ya kufanikiwa. Na wengine wanamdaharau Mungu kutokana na kutopata kile ambacho walikuwa wakikiomba kwa muda mrefu bila mafanikio. Kumbuka uvumilivu wako unaweza kukuwezesha kufanikiwa kwa kile unachokihangaikia. Duniani na mahali pa kupita, ukae katika hofu ya Mungu
KUTUMIA KIPAWA CHAKO KATIKA KAZI YA MUNGU
Mungu anataka kutumia kipawa alichokupa kwaajili ya kazi yake. Mungu amegawa kipawa kwa kila mtu, na anatamani kitumike katika kazi yake. Unaweza ukawa ni mzuri katika uandikaji, uimbaji, utungaji, mbunifu, uombaji, mshauri, mtu wa kucheza na kompyuta n.k. Kwahiyo Mungu antaka hivyo vipawa katika nyumba yake.
Wimbo: “Sio mimi ninaishi, bali Yesu ndani yangu, Yu hai Yu hai Yu hai”
Kumbukeni
wanadamu kuwa tulizaliwa uchi na tutarudi uchi. Unapozaliwa duniani unakuwa
huna nguo yoyote kutoka kwa Mungu na baada ya kuzaliwa unapata nguo kutoka kwa
ndugu na jamaa zako ili zikusitiri. Unapofika muda muda wako wa kutoweka hapa
duniani nguo zako na mali
zako unaziacha na wengine wanaaza kuzitumia. Kwahiyo tuache kujivunia na
vinavyoonekana hapa duniani havitatusaidia lolote siku ya hukumu. Vitu vyako
vifanye kazi ya Mungu Baba.
Mungu alikupenda wewe mwanadamu na kukupa upendeleo mkubwa ukifananisha na wanyama wakubwa kama tembo na simba aliowaumba. Iweje leo umsahau Mungu na kuona wewe ndio kila kitu hapa duniani. Kumbuka upo kwa neema ya Mungu.
MASENGENYO MAKANISANI
Makanisani na majumbani kumejaa masengenyo, ambayo yanataka kudondosha kanisa na kuwavunja moyo watu kufika kanisani. Maneno magumu yamekuwa yakizungumzwa na wanadamu makanisani yenye kuleta machafuko ya kutenganisha kanisana. Makanisa yamekuwa yanakosa waumini kutokana na maneno yako machafu.

KUTOMLILIA MUNGU BAADA YA MAFANIKIO
Watu hawapendi kumlilia Mungu baada ya kupata mafanikio. Mungu amewabariki kwa kumiliki magari, kujenga nyumba nzuri, kuwa na ofisi nzuri, kuoa au kuolewa, lakini wamemsahau Mungu aliyewapa. Waswahili wanasema hujafa hujaumbika. Kumbuka kulikuwa na watu wenye majina makubwa sana kama Price Diana lakini sasa hayupo dunia na historia yake inasaulika. Untafika muda wako wa kutoweka hapa duniani na watu watakusahau, na kama hukufanya kazi ya Mungu, naye Mungu atakusahau katika ufalme wake.
Watu hawapendi kumlilia Mungu baada ya kupata mafanikio. Mungu amewabariki kwa kumiliki magari, kujenga nyumba nzuri, kuwa na ofisi nzuri, kuoa au kuolewa, lakini wamemsahau Mungu aliyewapa. Waswahili wanasema hujafa hujaumbika. Kumbuka kulikuwa na watu wenye majina makubwa sana kama Price Diana lakini sasa hayupo dunia na historia yake inasaulika. Untafika muda wako wa kutoweka hapa duniani na watu watakusahau, na kama hukufanya kazi ya Mungu, naye Mungu atakusahau katika ufalme wake.
ACHANA JEURI NA DHARAU
Ewe mwanadamu achana na jeuri, kiburi havitakusaidia lolote na kumbuka ni wapi Mungu amekuokota. Ulikuwa huna kitu na ulikuwa mwaminifu kwa Mungu, lakini leo unamdharau Mungu wako baada ya kufanikiwa. Na wengine wanamdaharau Mungu kutokana na kutopata kile ambacho walikuwa wakikiomba kwa muda mrefu bila mafanikio. Kumbuka uvumilivu wako unaweza kukuwezesha kufanikiwa kwa kile unachokihangaikia. Duniani na mahali pa kupita, ukae katika hofu ya Mungu
KUTUMIA KIPAWA CHAKO KATIKA KAZI YA MUNGU
Mungu anataka kutumia kipawa alichokupa kwaajili ya kazi yake. Mungu amegawa kipawa kwa kila mtu, na anatamani kitumike katika kazi yake. Unaweza ukawa ni mzuri katika uandikaji, uimbaji, utungaji, mbunifu, uombaji, mshauri, mtu wa kucheza na kompyuta n.k. Kwahiyo Mungu antaka hivyo vipawa katika nyumba yake.
MANENO
MAKALI MAKANISANI
Watu wamekuwa wakihama makanisa kutokana na maneno yako makali yenye kuvunja moyo. Umekuwa ukiwasengenya waumini wenzako na kuwasemea maneno mabaya kwa marafiki zako. Msichana akipendeza kanisani, yanaanza maneno kuhusiana na kupendeza kwake. Maneno hayo yanapomfikia mhusika yanamvunja moyo na kuamua kuhama kanisa na wengine kuacha kabisa kufika kanisani. Unavyofanya hivyo unamkosea Mungu wako.

KUWAONEA WAPOLE MAKANISANI
Tusome Isaya 54:17, Kuna watu wamekuwa wakionewa kutokana na upole wao. Kuna watu ambao ni wapole na hawawezi kuongea maneno mabaya na wwamekuwa waaminifu katika kazi ya Mungu. Kutokana na upole wao, kuna hawa wanadamu wanakuja na kuwasemea maneno mabaya na kuwarudisha kiimani.

WANADAMU NI
MAREHEMU WATARAJIWA
Mwanadamu ni nani mpaka Mungu akukumbuke. Sisi ni marehemu watarajiwa au walemavu watarajiwa. Kuna watu wanapata maumivu makali sana majumbani mwao na wengine wako mahospitalini, lakini wewe bado uko hai na huna tatizo lolote, sasa kwanini unapenda kumuuzi Mungu wako ambaye anauwezo wa kukufanya lolote na usimfanye lolote.

MSHUKURU
MUNGU NA KAA KATIKA UWEPO WAKE.
Unapaswa
kama mwanadamu kumshukuru Mungu na kukaa katika uwepo wake na kuwa na hofu ya
Mungu. Kukaa katika uwepo wa Mungu ni kumtafakari Mungu kwa yale anayofanya
kwako na kwa wengine. Kukaa katika hofu ya Mungu ni kujaribu kufanya yale Mungu
anataka ufanye na kuachana na maovu yote kwa kumuogopa Mungu wako.
USIDHARAU
HUDUMA YA MTU KATIKA KAZI YA MUNGU
Kila mtu
ana njia yake ya kumtumikia Mungu kwahiyo usimseme mtu katika huduma yake
anayofanya kwaajili ya utukufu wa Mungu. Wewe angalia huduma yako kama inaenda sawasawa na mapenzi ya Mungu. Kusiwe na
masengenyo, kuvunjiana mioyo, wivu, mashindano katika kazi ya Mungu.
Wimbo,
“Dunia ni maua,
hunyauka, utaacha vya dunia, utaenda peke yako”
TUJIADHARA
KATIKA NYAKATI HIZI ZA MWISHO
Tupo katika nyakati za mwisho, ambazo ni hatari tujiadhari. Kuna vikwazo vingi vinavyosababisha wanadamu kutotamani kazi za Mungu na pengine kupuuzia pale tunaposikia habari njema kutoka kwa Mungu. Kama mwana wa Mungu na unayetamani kufika mbinguni, usiangalie ya wanadamu bali weka mawazo yako yote na akili yako kwa Mungu, utaona matokeo yake.

TENGENEZA
KIROHO CHAKO
Unatakiwa
kutengeneza kiroho chako kwa kuhudhuria ibada zote, kuimba, kusoma Neno la
Mungu. Tusiwe watu kama wa mataifa ambao
hawamjui Mungu.
HOFU KWA
WATOTO WA MUNGU KANISANI
Watu wanakuwepo katika nyumba ya Bwana lakini wanakuwa na hofu na maneno mabaya yanayotoka katika nyumba ya Bwana. Kanisa sio kila mtu ni mwema, kuna wengine ni wabaya sana na wapo kanisani. Kazi yao ni kuhakikisha jina la Kristo linarudi nyuma kwa kuwakwaza watu wa Mungu.

FAIDA ZA
UNYENYEKEVU
Kila mtu anayemnyenyekea Mungu na kufanya vile Mungu anataka hubarikiwa. Hakuna cha kujivuniania duniani. Hapa duniani kuna habari mbaya sana kwa mfano kifo. Kuepuka na hofu hiyo ni kufanya yaliyo mema ili hata ukifa siku ya mwisho utamuona Mungu na kufurahi naye.
Roho zetu
ziko mikononi mwa Mungu, kwahiyo tusiangalie ya kesho ila tuseme, “Mungu
akipenda, tutaonana kesho”Kila mtu anayemnyenyekea Mungu na kufanya vile Mungu anataka hubarikiwa. Hakuna cha kujivuniania duniani. Hapa duniani kuna habari mbaya sana kwa mfano kifo. Kuepuka na hofu hiyo ni kufanya yaliyo mema ili hata ukifa siku ya mwisho utamuona Mungu na kufurahi naye.
Wimbo: “Sio mimi ninaishi, bali Yesu ndani yangu, Yu hai Yu hai Yu hai”
Tumwabudu Mungu, Tumtukuze Mungu, Tumtumikie Mungu.
Wimbo, “Tengeneza maisha yako, utakufa utaviacha”
MUNGU AKUBARIKI
KWA MSAADA WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD
NA MCHUNGAJI DR.GETRUDE RWAKATARE.......
0 maoni:
Post a Comment