Thursday, April 24, 2014

Mourinho achanganyikiwa Ni kutokana na mechi mbili ngumu mbele yake.. Kikosi chake kinamajeruhi wengi..Tizama alichokisema Mreno huyo.


KOCHA wa Chelsea Jose Mourinho yuko kwenye njia panda kuhusu wachezaji atakaotumia kwa mechi dhidi ya Liverpool Jumapili na Atletico Madrid Jumatano ijayo.
Kocha Wa Chelsea
Jose Mourinho
Hii ni kutokana na kuwa wanasoka wanne watakosa mechi ya marudiano dhidi ya Atletico Madrid juma lijalo ya kufuzu kwa fainali ya Uefa. Baada ya kutoka sare 0-0 nchini Uhispania Jumanne ni lazima Chelsea washinde uwanjani Stamford Bridge katika mechi ya marudiano la sivyo ikose kufuzu kwa fainali.

Hata hivyo jitihada hizo huenda zikavurugwa na hatua ambako kipa nambari moja Petr Cech na difenda John Terry waliumia katika mechi ya Jumanne na watakosa mechi ya marudiano. Nao Frank Lampard na John Obi Mikel walipata kadi za manjano na vile vile watakosa mechi hiyo.
Kocha Mourinho ametisha kuchezesha timu dhaifu dhidi ya Liverpool Jumapili ijayo ili kuokoa nafasi zake kufika fainali ya Uefa.
Mbali na wanne hao, Chelsea pia itakosa huduma za straika Samuel Eto’o na kiungo shupavu Eden Hazard ambao pia wana majeraha.
“Msimu wa Cech umeisha kwani atachukua muda mrefu kupona na kwa Terry, itatulazimu tucheze hadi fainali ili apate nafasi nyingine ya kuonja soka ya Uefa,” Mourinho alisema baada ya mechi hiyo.
Vijana hao watakutana na Liverpool yenye ari kuu ya kushinda taji kwa mara ya kwanza tangu 1990.
Chelsea inashikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa alama 75, tano nyuma ya Liverpool ambayo ina alama 80 huku zikiwa zimesalia mechi tatu pekee msimu kumalizika.

Msimamo Wa Ligi kuu England Ulivyo kwa sasa.

 1. English Premier League
  Standings
  #
  Team
  GP
  W
  D
  L
  GF
  GA
  GD
  PTS
  1
  35
  25
  5
  5
  96
  44
  52
  80
  2
  35
  23
  6
  6
  67
  26
  41
  75
  3
  34
  23
  5
  6
  91
  35
  56
  74
  4
  35
  21
  7
  7
  62
  41
  21
  70
  5
  35
  20
  9
  6
  57
  34
  23
  69
  6
  35
  19
  6
  10
  51
  49
  2
  63
  7
  34
  17
  6
  11
  56
  40
  16
  57
  8
  35
  13
  10
  12
  50
  45
  5
  49
  9
  35
  14
  4
  17
  39
  54
  -15
  46
  10
  35
  11
  11
  13
  39
  49
  -10
  44
  11
  35
  13
  4
  18
  28
  41
  -13
  43
  12
  35
  10
  7
  18
  38
  48
  -10
  37
  13
  35
  9
  9
  17
  47
  51
  -4
  36
  14
  34
  10
  6
  18
  34
  43
  -9
  36
  15
  34
  9
  8
  17
  35
  49
  -14
  35
  16
  34
  6
  15
  13
  41
  54
  -13
  33
  17
  35
  8
  8
  19
  28
  56
  -28
  32
  18
  35
  7
  9
  19
  31
  65
  -34
  30
  19
  35
  9
  3
  23
  35
  77
  -42
  30
  20
  34
  7
  8
  19
  33
  57
  -24
  29

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score