Saturday, April 26, 2014

Tani Moja Ya Heroin Yakamatwa Na Wanajeshi Wa Austrilia Katika Pwani Ya ....................


Madaya Ya Heroin Yaliyokamatwa. Inasemekana ni zaidi ya Tani moja.
Jeshi la Wanamaji la Australia lilikamata magunia 46 ya heroin yenye thamani ya dola milioni 290 (shilingi bilioni 25 za Kenya Sh) kutoka kwenye meli iliyokuwa ikisafiri katika Upwa ya Kenya, lilitangaza Shirika la Habari la Australia jana siku ya Ijumaa (tarehe 25 Aprili).


Mabaharia wa meli ya HMAS Darwin waliingia kwenye boti walioishuku na kugundua madawa yaliyofichwa kwenye mifuko ya saruji.

"Madawa haya sasa yameshikiliwa na na yameharibiwa hapo jana na wanajeshi wa Australia," alisema kamanda Terry Morrison. "Inafahamika vyema kwamba madawa haya yanayasaidia makundi ya kigaidi kifedha ili waweze kufanya matendo yao ya kigaidi."

 Meli hiyo ya Darwin imetumwa kwenye Pembe ya Afrika kama sehemu ya Operesheni Slipper, mchango wa Australia kwenye juhudi za kimataifa za kupambana na ugaidi, ulanguzi na uharamia kwenye eneo la bahari la Mashariki ya Kati.
Meli Iliyokuwa Imebeba Madawa Hayo. HMAS

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score