Thursday, May 15, 2014

Tokomeza Boko Haramu. Ni Oparesheni Iliyoingiliwa Mataifa Màkubwa. Kuwatafuta Wasichana....

Serikali ya Nigeria imethibitisha habari za kuanza operesheni ya kijeshi inayosaidiwa na vikosi vya kimataifa kwa ajili ya kuwatafuta na kuwaokoa zaidi ya wasichana 200 wa shule waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram. 

Habari zinasema kuwa jeshi la Nigeria linasaidiwa na askari maalumu wa Canada, timu ya wataalamu wa kijeshi wa Marekani, Uingereza, Ufaransa n.k, kwenye operesheni hiyo.

Maafisa wa Pentagon wamearifu kuwa, Marekani inatumia ndege  za kijasusi zisizo na rubani  na vifaa vinginevyo vya kijeshi katika operesheni hiyo ya kuwatafuta wasichana wa Nigeria waliotekwa nyara.

Hayo yanajiri huku Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds akiarifu kwamba, Rais Goodluk Jonathan wa Nigeria amesema wazi kuwa hawatazungumza na kundi la Boko Haram kuhusiana na kubadilishana wafungwa na wasichana hao waliotekwa nyara

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score