Saturday, May 24, 2014

Katanga German Muasi Aliyewafadhli Waasi Congo Ametupwa Gerezani Miaka Kumi Na Miwili

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Ijumaa ilimhukumu aliyekuwa kiongozi wa kivita wa DR Congo Germain Katanga miaka 12 gerezani kwa tuhuma za kuwapa waasi silaha.

German Katanga

Waasi hao wanadaiwa kutekeleza mashambulio ya kikatili katika kijiji kimoja mnamo 2003.
“Mahakama hii imemhukumu Germain Katanga miaka 12 gerezani,” alisema Jaji Bruno Cotte, aliyesoma hukumu hiyo, iliyo ya pili tangu kuasisiwa kwa mahakama hiyo mnamo 2003.
Kulingana na jaji huyo, miaka saba ambayo mshukiwa huyo amekaa katika mahakama hiyo itaondolewa kutoka kwenye kifungo hicho.
Katanga, aliye na miaka 36 alipatikana na hatia mnamo mwezi Machi kwa kuhusika katika ukatili dhidi ya binadamu.
Makosa mengine yaliyomkabili ni mauaji ya kikatili yaliyotekelezwa katika kijiji cha Bogoro, mashariki mwa nchi hiyo mnamo Februari 24, 2003.
Majaji hao walimpata na hatia ya kuwapa wapiganaji wa kundi la Patriotic Resistance Forces (PRFI) silaha katika msitu wa Ituri ambapo watu zaidi ya 200 waliuawa katika shambulizi hilo.
“Makovu ya ukatili huo yangali dhahiri katika kijiji hicho,” akasema Jaji Scott.
Matumizi ya mapanga katika shambulio hilo yalidhihirisha 'ukatili wa hali ya juu na kusababisha mateso makubwa kwa waathiriwa,” akaongeza.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilimwondolea mashtaka ya ubakaji, kuwafanya waathiriwa kuwa watumwa wa kingono na matumizi ya watoto kuwa wanajeshi.
Mahakama Ya ICC
Mawakili wake wamekata rufaa.

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score