Wednesday, May 7, 2014

Uchaguzi mkuu Afrika Ya Kusini.

Uchaguzi mkuu nchini Afrika Kusini, utafanyika leo Jumatano.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni, ushindani mkali utakuwa kati ya wagombea watatu kutoka vyama vya ANC, chama cha upinzani cha muungano wa kidemokrasia na chama cha wapigania uhuru na uchumi.

Kuna jumla ya wagombea elfu nane na 651, ambao wanatoka katika vyama 45 vya kisiasa, watakaochuana katika uchaguzi huo.

Uchaguzi mkuu nchini Afrika Kusini hufanyika kila baada ya miaka mitano.

Mbali na Rais, katika uchaguzi huo huchaguliwa pia wawakilishi wa wananchi katika bunge linaloundwa na wajumbe 400 na wawakilishi 90 wa baraza la kitaifa la mikoa tisa ya nchi hiyo.

Zaidi ya watu milioni 25 yaani karibu nusu nzima ya wananchi wa Afrika Kusini, wamejiandika kushiriki katika uchaguzi huo.

Afrika Kusini ina jumla ya watu milioni 53 ambapo asilimia 80 kati yao ni watu weusi, na asilimia 9 pekee ikiwa inaundwa na watu weupe.

Hii ni katika hali ambayo matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanyika nchini humo yanaonyesha kuwa, chama tawala cha ANC kitashinda katika uchaguzi mkuu huo utakaofanyika hivi leo, kwa kujipatia asilimia 63 ya kura zote kiwango ambacho kiko chini ya asilimia tatu ikilinganishwa na kura za uchaguzi wa mwaka 2009..

Endelea kufuatilia Mchimba Riziki itakuletea matokeo hayo.

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score