Thursday, June 19, 2014

Jela: Jela Ni Mahali Kila Mtu Anaogopa Lakini Kwa Wakazi Wa Hindi Lamu Iliwabidi Wakimbilie Kutafuta Usalama Hapo Jana

HALI ya taharuki ilighubika kijiji cha Hindi hapo
Jumanne baada ya uvumi kuenea kwamba watu
wasio wa kawaida walionekana wakizurura mjini
humo.
Wengi wa wakazi walilazimika kuhama majumbani
mwao na kukimbilia katika jela ya Hindi wakitafuta
usalama.
Shughuli za kibiashara
zilisitishwa kwa takriban
masaa sita huku wenye
maduka na vituo vya
mafuta wakilazimika
kufunga biashara zao kwa
kuhofia usalama.
Chifu Mkuu wa eneo hilo,
Bw Abdalla Shahasi, alilazimika kuitisha mkutano
wa dharura mjini Hindi ili kutuliza hali.
Vikosi vya askari wakiwemo GSU na askari tawala
ilibidi wasambazwe mjini Hindi na viungani mwake
ikiwemo Ndeu na maeneo ya karibu ambapo
wavamizi walidaiwa kuonekana.
Baadhi ya wakazi pia walihama mijini mwao na
kukimbilia misituni na familia zao mara tu baada ya
taarifa za kuonekana kwa wavamizi kuwafikia.
“Watu walianza kuhama wakihofia usalama baada
uvumi kuenezwa eti watu wasio wa kawaida
walionekana karibnu na Hindi. Maduka yalifungwa
kwa muda. Ilibidi niitishe mkutano. Ninawasihi
wakazi wasiwe na shaka. Tayari polisi wameshika
doria na Hindi ni salama,” akasema Bw Shahasi
kwa njia ya simu.
Wakazi aidha wametakiwa kuwa makini na kupiga
ripoti haraka iwapo watashuhudia tendo au mtu
yyeyote wanayeshuku kuwa tisho kwa usalama.
Aidha wageni wote wanaoingia Hindi na viungani
mwake pia wametakiwa kujisajili kwenye afisi ya
chifu kwanza huku wakionywa kutopuuza sheria
hiyo.
Eneo la Hindi ni takriban kilomita 45 kutoka
Mpeketoni ambapo watu zaidi ya 50 waliuawa
katika shambulizi la Jumapili usiku huku zaidi ya
nyumba 30 na magari zaidi ya 20 yakiteketezwa.

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score