Tuesday, June 17, 2014

Kauli Ya Rais Kenyatta Baada Ya Mashabulizi Mfululizo Lamu

Kauli ya Rais Kenyatta inakuja kupitia kwa
televisheni siku moja baada ya kundi hilo kukiri
kufanya mauaji yaliyotokea Mpeketoni Jumapili
usiku.
Kenyatta emesema kuwa kuna ushahidi kuonyesha
kuwa shambulizi hilo lilipangwa vyema na kwamba
wanasiasa walihusika nao.
Al Shabaab lilikiri katika taarifa kwa vyombo vya
habari kuwa ndilo lilifanya mauaji hayo Jumatatu
jioni.
Alisema kuwa ujasusi ulitolewa kuwa mashambulizi
hayo yangefanyika lakini hawakuchukua hatua
zozote kuzuia mashambulizi hayo.
Rais amesema kuwa maafisa waliohusika tayari
wameachishwa kazi na kwamba watashitakiwa.
Wmaesema kuwa wanachunguza wanasiasa
waliohusika na mauaji hayo.
Mauaji zaidi yalifanyika usiku wa kuamkia leo licha
ya taarifa ya Al Shabaab kusema kuwa
washambuliaji walioshambulia Mpeketo walikuwa
wamerejea salama nchini Somalia.
Uharibifu mkubwa ulishuhudiwa katika mji huo huku
washambuliaji wakichoma hoteli na kituo cha polisi
pamoja na kuteketeza magari waliyoyatumia kwa
usafiri wao.
Kenyatta amesema kuwa kuna baadhi ya
wanasiasa wanaochochea uhasama miongoni mwa
jamii.

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score