Ujerumani Katika Picha Moja |
Goli moja la Gotze la dakika za nyongeza ndio lilipeleka kilio Argentina huku kombe hilo likitua Ujerumani.
Na baada ya sherehe za ubingwa wa Dunia 2014, kocha wa Ujerumani, Joachim Loew alisema kuwa alimpa nasaha moja Gotze kabla ya kumuingiza uwanjani akitokea benchi.
Captain Wa Ujerumani Akishangilia kombe la Dunia |
Law alimwambia mchezaji huyo kuwa aingie uwanjani na kuionyesha dunia kwamba ana kiwango kikubwa kuliko mshambuliaji huyo wa Argentina. “Nilimwambia Gotze baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha muda wa zia
Timu Ya Ujerumani Ikipokelewa Nyumbani Ujerumani |
da, 'dhihirisha kwamba wewe ni mchezaji bora kuliko Messi, onyesha kuwa una kiwango kumpiku yeye, kiwango ambacho kinaweza kushinda Kombe la Dunia,” Loew aliwaambia wanahabari baada ya mechi.
mashabiki Wa Ujerumani Wakiwashangilia Mashujaa Wao |
Baada ya kazi kuwa ngumu hadi dakika za mwisho huku mchezo ukionekana ungeamuliwa na penalti, wachezaji wawili ambao waliingizwa kama nguvu mpya ndio walioishia kuikomboa Ujerumani.
Andre Schurrle alipokea mpira wa pembeni mwa uwanja upande wa kushoto kutoka katikati na kutimka nao huku akiandamwa na mabeki wawili wa Argentina.
Lakini maarifa yake ya kuzalisha krosi ya haraka iliyowapenya katikati madifenda, yalimfikia vyema Gotze kwenye eneo la hatari. Naye hakusita kuutuliza kwa kifua kabla ya kupiga kiki kali lililojaa katika wavu wa kipa Romero Rodriguez huku ikiwa imesalia dakika tatu pekee kabla ya mchezo kwenda hatua ya penalti.
Gari Walilotumia Timu Ya Ujerumani Wakiwa Munich |
Bao hilo lilitosha kuwapa Ujerumani taji hilo kwa mara ya nne, makombe ya awali wakishinda 1954, 1974 na 1990.
Huku Ujerumani wakisherehekea ufanisi wao, Messi ambaye alituzwa kuwa mchezaji bora wa dimba hilo amewalaumu mafowadi kwa kupoteza nafasi nyingi za wazi ambazo zingewapa ubingwa badala ya wapinzani wao.
0 maoni:
Post a Comment